Tuipende Tanzania nchi Tuliyo Zaliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuipende Tanzania nchi Tuliyo Zaliwa

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by X-PASTER, Dec 15, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Tuipende Tanzania nchi Tuliyo Zaliwa

  Kuna mlima mrefu, kwa sifa twajivunia
  ukiwekwa kwenye safu, urefu kuukadiria
  Hapawi ulinganifu, Africa yote pia
  Tuipende Tanzania nchi tuliyo zaliwa

  Unavilele viwili, majina nawatajia
  mawenzi ni cha awali, hapa nawahesabia
  Kibo kilele cha pili, jamani nawaambia
  Tuipende tanzania nchi tuliyo zaliwa

  Naacha mlima ule, na vilele vyake pia
  kusudi nisongembele, kwenye mbuga kuingia
  nifike hapa na pale, nichungue kila njia
  tuipende tanzania nchi tuliyo zaliwa

  Kuna nyoka wa kudhulu, na sokwe wenye mikia
  na mbega walio huru, miti waiparamia
  na ndege wengi wazuri, wa rangi za kuvutia
  tuipende tanzania nchi tuliyo zaliwa

  Mbuga na misitu hii, na nisiyo watajia
  huwavuta watalii, kila mwaka kutujia
  Nao hawavulii, milima kuisifia
  tuiepende tanzania nchi tuliyo zaliwa

  source: Tujifunze Lugha Yetu Kitabu cha tano
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Shairi linatafakarisha ... !! The Good Tz I Knew!!!
   
 3. Utotole

  Utotole JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2014
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 6,344
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Sina budi kuisifu, nchi yetu Tanzania,
  Kwa shairi maarufu, na vina kupangilia,
  Nipange na kusanifu, shairi kuwaimbia,
  Tuipende Tanzania, nchi tuliyozaliwa

  Nifikapo Serengeti, au mikumi kwa nia,
  Kwa jitihada na dhati, wanyama kuangalia,
  kuna makundi ya nyati, nyumbu na pundamilia,
  Tuipende Tanzania, nchi tuliyozaliwa.
   
 4. Utotole

  Utotole JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2015
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 6,344
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye source angalia vizuri. Nadhani shairi hili linapatikana kitabu cha darasa la sita (if I am not mistaken). na kwa mujibu wa mpangilio wa vitabu vya Tujifunze lugha yetu, darasa la sita tulikuwa tunatumia kitabu cha 8. Hii ni kwa sababu kulikuwa na vitabu viwili (cha kwanza na cha pili) kwa darasa la kwanza, kisha cha tatu na cha nne kwa darasa la pili. Kuanzia darasa la tatu kitabu kimoja kimoja.
  Kitabu cha Tano--darasa la tatu
  Kitabu cha sita---darasa la nne
  Kitabu cha saba--darasa la tanoK
  itabu cha nane---darasa la sita, na
  kitabu cha tisa---darasa la saba

  Wakati nasoma mimi...inawezekana mpangilio ulikuwa tofauti wakati mwingine. Tufahamishane.

  Generally, imiss those books. I am looking for them and will definitely buy them so i can re-read them and relive the memory. yeyote mwenye idea wapi naweza kuvipata vitabu hivi ataufahamishe.
   
Loading...