Tuipe ladha Jamiiforums kwa kuboresha ujengaji wa hoja kwenye Majukwaa mbalimbali

Mausingizii

Member
Jul 14, 2022
82
67
Wasalaam wana JF ,

Nimekuwa nikifuatilia mada mbalimbali kutoka katika forums hii pendwa kwa muda kidogo, ama kwa hakika JF hutupatia maarifa na uelewa katika nyanja tofauti tofauti kama kisima cha maarifa.

Bila shaka utofauti wa forum hii ni nyingine unakuja katika uwasilishaji wa hoja zenye uthibitisho hali inaiyopiku mitandao mingine ya kijamii inayobobea kwenye porojo na uvumi tu.

Lakini ninasikitishwa kuona jukwaa hili kwa sasa limekuwa likijikita kujibu na kuainisha mambo pasipo hoja badala yake mihemko, matusi na lugha za hovyo zimekuwa zikitawala.

Hali hii inapoteza mvuto kwani jukwaa la Great thinkers ndilo limeweza kusalia katika uwasilishaji wenye mashiko, licha ya idadi ndogo ya machapisho ikilinganishwa na majukwaa mengine .

Hebu turejeshe mvuto kwa kujikita katika kujenga hoja ili kurejesha ladha na mvuto zaidi kwa wasomaji wake.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom