Tuijadili PCCB: Kwanini tuendelee kuwa nayo?

PCCB na DPP wanakanganyana sana; one needs to be merged into the other, vinginevyo kuviacha kama vilivyo vinatoa hisia kwamba hata masuala la ufisadi/rushwa nayo yanahitaji 'checks and balance'

Usemacho JF Senior Member Expert kina ukweli haswaaa...dhana ya "checks and balance" niilewavyo mimi ni kwa mihimili mikuu mitatu ya dola yaani Bunge, Mahakama na Executive...kwamba Bunge liisimamie Serikali inapotekeleza majukumu yake na vice versa...lakini kilichopo kati ya DPP na PCCB ni kusimamiana kwa vyombo ambavyo vyote vipo chini ya Executive Branch...ikimaanisha ndani ya Executive branch vyombo vinasimamiana vyenyewe suala lililopotosha dhana ya "checks and balance"...PCCB kwenye katiba mpya tuwape mamlaka ya kusimama wenyewe na wawe na Mahakama za Makosa yao ya rushwa nakuhakikishia kila mtenda maovu ataenda jela...
 
Uchaguzi ndani ya CCM uligubikwa na rushwa ya kutisha.Mbona hakuna hatua zozote zilichukuliwa na TAKUKURU?.Hawa wanakula tu
kodi za Watanzania,bora Ifutwe.
 
Kama tulivyopata kushuhudia kwenye Chaguzi zinazoendelea za Magamba Party, rushwa imekuwa ikitolewa bila kificho kiasi kwamba mpaka Kiasi kinachotumika katika baadhi ya maeneo kinajulikana, kwa mfano Milioni 300 zimetumika kummaliza Makongoro Nyerere a.k.a "Mzee wa Site" na zile zilizotumika kuwamaliza watu wa aina yake kama akina Kusila, Sumaye n.k.

Pamoja na mambo hayo kuonekana yanafanyika wazi wazi lakini mpaka leo hatujasikia mtu yeyote aliyekamatwa na PCCB akishiriki kwenye vitendo hivyo vya rushwa ukiachilia mbali yale yaliyosemwa mwaka 2010 kwenye kura za Maoni za CCM ambapo "Mheshimiwa" Suleiman Nchambi, yeye aliwatumia watu hao hao wa PCCB kuwagawia Wapiga kura rushwa, Sasa hapa kuna haja gani ya kuendelea kuwa na hili dubwana PCCB ambalo halina lolote zaidi ya kutafuna pesa ya kodi zetu?

Je wananchi wakichoshwa na kuamua kutoa hukumu wenyewe, watalaumiwa kweli? Nani wa kulaumiwa?
 
Mbona kila mara tumewasikia wakisema "mwenye ushahidi atuletee" kana kwamba tayari wako kwenye mchakato wa kumtetea mtuhumiwa....wakati mwingine ushahidi uko wazi kabisa.....cha kushangaza wao wamepewa rasilimali ya kutafutia ushahidi hawapati.......iweje yule asiye na rasilimali ndiyo awapelekee ushahidi....kama yeye ndiyo kazi yake......kama ikiendelea kufanya kazi kisiasa.....basi itaendelea kuwa taasisi ya kutetea na kudumisha rushwa....
 
Ninaamini, na nitaendelea kuamini kwamba kabla ya maamuzi ya haki ya watz kuamua kuunda serikali mpya ya watu wapya, wimbo wa takukuru utabakia huohuo labda zitaongezeka chorous mpya hapa na pale.
Inshaalah , na watumie, wafiche tutawaumbua . Malawi bwana mkubwa anaaibika.
 
Ivunjwe haraka kama ilivyovyunjwa "Scorpion" Ya hapa kwa Madiba. Tangu scorpion ivunjwe uchumi wa RSA umekua sana. Ni hasara kwa taifa letu.Tena hii iko Ofisi ya Rais...haki ya Mungu ivunjwe haraka.

 

Mtanzania, hii isipovunjwa haraka ni hatari. .....Dr E.H kama nitakuwa nimekuvunjia heshima nisamwehe ila ndo ukweli. Naamini utapata ajira kivingine.
 
Tukusanye ushahidi wa kuisambaratisha Takukuru. Policia wafanye kazi zao, Takukuru ya nini wakati haina meno kuwangata wezi?

 

Sikia nikwambie jembe langu yani hata ishitaji kufungua hii Attachment,hakuna watu ambao hawana kazi nchi hii kama hawa unaowaita PCCB!!

Sikia nikwambie kama ni rushwa katika nchi hii hawa ndio wanaoongoza kwa kula rushwa na hata wao wanalijua hilo,sema wanajifanya kutosikia kilio cha watu kama sisi.

Natamani sana siku moja itokee ofisi zote za PCCB ziungue moto na ikiwezekana wote waungiliemo ndani,sema hili ombi langu haliwezi kukubalika lakini kama inawezekana naomba iwe hivyo,hakuna watu wachafu kama hawa,mi kwanza nashangaa wanapigiwa kelele wakina EL,sijui na akina nani wengine wale halafu hii mijitu inachwa

Sikia kwanza inakula mishahara mikubwa halafu haina kazi.swain.
 

Uchaguzi ndani ya CCM uligubikwa na rushwa ya kutisha.Mbona hakuna hatua zozote zilichukuliwa na TAKUKURU?.Hawa wanakula tu
kodi za Watanzania,bora Ifutwe.
Kuna mdau mmoja katika blogu yake aliwahi kuandika makala ndefu kumuomba rais aivunje TAKUKURU kama ilivyovunjwa Scorpion ya SA ili kupunguza matumizi makubwa na yasiyo na tija kwa taifa letu...Alishauri hivyo kwani hiyo ni Taasisi ndani ya Ikulun na bado infanya madudu. Inaegemea upande wa siasa kuliko kutekeleza majukumu yake ya kiserikali.
 
Mkuu Bw. Hosea ameteuliwa na Kiongozi wa CCM, wala Rushwa wakubwa ni CCM sitegemei lolote kutoka kwa Taasisi hii chini ya uongozi wa CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…