Tuige mfano wa vyuo hivi.

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,122
3,722
Wana jukwaa hili la elimu ningependa wote tuige mfano wa hivi vyuo hapa Tanzania ambavyo havijihusishi katika kunadi uwezo wa vyuo vyao huku wahitimu wao waking'ara kitaifa na kimataifa katika utendaji kazi wao,vyuo hivyo vya kuigwa ni ARDHI,SUA,SUZA(STATE UNIVERSITY OF ZANZIBAR),MUHAS NA HKMU(HUBERT KAIRUKI).
 
HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,122
3,722
That true mkuu,kuna hawa vijana wa udsm,IFM,IAA na mzumbe,hadi wamekua kero humu jf

haina haja ya kujitutumua katika taasisi yako ya elimu ya juu,cha msingi ni kupata maarifa na kwenda kuyafanyia kazi kwa maslahi ya taifa kwa ujumla bila kujali huyu tulisoma nae IAA,MUCCOBS au TEKU.
 
Gavanor

Member
Oct 15, 2011
60
3
haina haja ya kujitutumua katika taasisi yako ya elimu ya juu,cha msingi ni kupata maarifa na kwenda kuyafanyia kazi kwa maslahi ya taifa kwa ujumla bila kujali huyu tulisoma nae IAA,MUCCOBS au TEKU.

ila madogo wanakera sana,wangejua wenzao pia tumesoma kwenye hvyo vyuo vyao wanavyoviita bora na hadi leo tumepigwa benchi kwenye soko la ajira,hata wasingethubutu kuleta mabishano ya vyuo humu jf.
 
Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
we unafikili basi watoto? Ni swala la kutojitambua na inaonyesha elimu zao hazijawajenga kabisa.

wanafunzi wengi wa mikoani wanaona fahari kufika dar. Wanajihisi umaarufu sana kusoma udsm kwakuwa hawajui vyuo vingine.
 
Lyceum

JF-Expert Member
Oct 1, 2009
1,043
567
Suala sio chuo bali ni alichopata huko alikosoma. Kuna watu wanajifanya wamesoma vyuo bora ila ukimpa kazi ya kufanya anatafuta visingizio. Oh naumwa, oh nina mgonjwa oh naharisha. Full aibu. Tunawaona mitaani huku
 
Job K

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
9,321
7,080
Suala sio chuo bali ni alichopata huko alikosoma. Kuna watu wanajifanya wamesoma vyuo bora ila ukimpa kazi ya kufanya anatafuta visingizio. Oh naumwa, oh nina mgonjwa oh naharisha. Full aibu. Tunawaona mitaani huku

Mkuu utanivunja mbavu!!

Eti naharisha! Kisa ameogopa kazi? Yaani kuna hivi vyuo wanavyoviita bora yaani hakuna lolote! Kuna siku tumemwita mwananchi mmoja kwenye "interview" kutoka chuo hicho maarufu yaani alitutia aibu (wa-TZ) ni mwisho, ukizingatia tulikuwa na ma-boss kutoka Kenya yaani ilikuwa kituko niliona aibu utafikiri mimi ndo nilikuwa mhusika! Mtu hawezi hata kuunga sentensi ikaeleweka?

Nafikiri wakati umefika waache majigambo! Hawaioni mijamaa ya SUA imetulia lakini ikiingia kwenye mzigo ni kazi kweli kweli!
 
umaarufu wao uko kwenye migomo na sifa za kijinga tu..
 
Mopalmo

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
533
136
Hata sisi Tia hatuna makuu ila wakaulizie wahasibu kwenye idara mbalimbali watapata stori, kizuri chajiuza bana huu msemo haupitwi na wakati
 
nyambari

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
355
169
Mimi sidhani kama chuo ndo kinamfanya mtu awe mwajibikaji mzuri katika kazi, hapa ni mtu mwenyewe kujitambua na kujua uwezo wako ukoje hivyo sioni umuhimu wa kuvisifia baadhi ya vyuo hapa tz
 
HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,122
3,722
Mimi sidhani kama chuo ndo kinamfanya mtu awe mwajibikaji mzuri katika kazi, hapa ni mtu mwenyewe kujitambua na kujua uwezo wako ukoje hivyo sioni umuhimu wa kuvisifia baadhi ya vyuo hapa tz

umuhimu hakuna wala haina faida kusifia chuo,chuo kikiwa na uwezo wa kukidhi utoaji shahada na stashahada na kikikubalika na tume ya vyuo vikuu Tanzania basi hapo ni swala lako mwanafunzi kutumia nafasi yako na mapungufu katika vyuo vyetu vya serikali ni yaleyale kwa wote hakuna penye uafadhali.
 
NIMIMI

Senior Member
Apr 2, 2011
170
16
Mimi sidhani kama chuo ndo kinamfanya mtu awe mwajibikaji mzuri katika kazi, hapa ni mtu mwenyewe kujitambua na kujua uwezo wako ukoje hivyo sioni umuhimu wa kuvisifia baadhi ya vyuo hapa tz

leo Nyambari nimeyapenda madesa yako. Tujadili mstakabali wa kulikomboa Taifa linaloangamia kwa wasomi kukosa maarifa zaidi kukaa na kutunishiana misuli kwa mitaa juu ya vyuo tulivyosoma utadhani ndilo suluhisho la kuikomboa nchi yetu ambayo wanafaidi wachache ni ukosefu wa Taaluma. Maendeleo ya nchi hii hajaletwa na waliosoma Udsm, Sua, mzumbe, Muhas, teku, Herbert kairuki, Ifm, tia, Iaa nk bali na wote ambao hawakusoma na waliosoma katika vyuo vyetu. Hayo mambo ya nilisoma Ilboru nikawa T.O hatuhitaji. Tunataka umechango gani hasi kwa maendeleo ya Taifa. Mbona WAHASIBU Wengi ndo wezi kuhujumu pesa za Halmashauri zetu ambazo ni kodi za wananchi ambao ni walalahoi (CHEAPJOHNS) je tuvilaumu vyuo walivyopitia wahasibu hao kama IAA, TIA, IFM nk? Yepi mawazo yako juu ya hili? Nawasilisha
 
NIMIMI

Senior Member
Apr 2, 2011
170
16
umaarufu wao uko kwenye migomo na sifa za kijinga tu..

hiyo ndio kazi ya wasomi kama ambao hawajasoma wanaona matatizo na wanahoji kwa migomo, iweje kwa wasomi wanaliona jambo tena kwa serikali iliyokiburi kama yetu wasomi wasigome kwa maslahi ya wengi. Funga domo lako kama hupendi vijana wagomee mambo ya msingi. Au umetumwa humu? Uende ukawaeleze kwamba kwasababu tuliwapa muda kutatua matatizo yetu juu ya swala la mikopo hadi sasa kimya kesho kutwa tunagoma kuwashinikisha watupatie mkopo. Ukishindwa kaa chini ulie. Unaona furaha wanafunzi kurejea kwao kwa kukosa mikopo ya kuendelea na Elimu ya Juu? You look shaby shame on you.
 
HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,122
3,722
leo Nyambari nimeyapenda madesa yako. Tujadili mstakabali wa kulikomboa Taifa linaloangamia kwa wasomi kukosa maarifa zaidi kukaa na kutunishiana misuli kwa mitaa juu ya vyuo tulivyosoma utadhani ndilo suluhisho la kuikomboa nchi yetu ambayo wanafaidi wachache ni ukosefu wa Taaluma. Maendeleo ya nchi hii hajaletwa na waliosoma Udsm, Sua, mzumbe, Muhas, teku, Herbert kairuki, Ifm, tia, Iaa nk bali na wote ambao hawakusoma na waliosoma katika vyuo vyetu. Hayo mambo ya nilisoma Ilboru nikawa T.O hatuhitaji. Tunataka umechango gani hasi kwa maendeleo ya Taifa. Mbona WAHASIBU Wengi ndo wezi kuhujumu pesa za Halmashauri zetu ambazo ni kodi za wananchi ambao ni walalahoi (CHEAPJOHNS) je tuvilaumu vyuo walivyopitia wahasibu hao kama IAA, TIA, IFM nk? Yepi mawazo yako juu ya hili? Nawasilisha

hilo kweli mkuu,maendeleo ya nchi hii yataletwa na wote namaanisha wasomi(skilled labour) na wale wachini ambao takwimu zinaonesha wanaishi chini ya dola 1,wote katika nafasi tulizopo tunalipa kodi ambazo zinawezesha baadhi yetu kutunisha vifua na kusema nasoma mzumbe ila isinge kuwa kodi chuo kingefungwa,wakulima wanatuzalishia vyakula na nijukumu letu kusoma na kuboresha kilimo nchini kiwe cha kisasa na kikidhi mahitaji,wataalamu wa ardhi na majengo taifa linawategemea.Mungu atubariki wasomi Tanzania katika jitihada ya kulihudumia taifa letu.
 
nzitunga

Senior Member
Oct 31, 2010
193
52
Ukifikiri jina la chuo ndilo linakupa elimu na wala si juhudi yako umeliwa! Na pole sana!
Tusimsifu wala kumlaumu mtu kwa chuo chake, tumpime yeye mwenyewe! Sometimes hata tusiangalie GPA, kuna vyuo wanazigawa kama njugu! Always, tupime uwezo wa mtu
 
ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
vumilieni kwani kusoma huko ndo nini? la muhimu unachapa mzigo maisha yanaendelea
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom