Mji wa Moshi ulioko katika mkoa wa Kilimanjaro Kaskazini mwa Afrika unasifika kwa usafi. Waliotembelea mji huo wanatuhadithia kwamba, mji huo ni msafi licha ya udogo wake na bustani zake zina mandhari ya kuvutia. Sifa nyingine ni kwamba, wahusika wameweza kudumisha sheria za usafi katika mji huo na hivyo kumfanya kila mwananchi kufahamu jukumu lake. Kwa nini miji kama Dar na mingineyo isiige mfano huu. Utakuta mtu yuko ndani ya daladala akimaliza kunywa maji yake ya uhai anarusha chupa ile barabarani, akimaliza kuandika tarakimu na vocha yake ya simu anaitupa popote alipo, matokeo yake Dar leo imejaa vyupa vya maji, manailoni na makaratasi ya vocha hapo bila kujali taka zingine zilizozagaa kwa wingi. Maeneo ya katikati mwa Jiji kidogo kuna juhudi za usafi zinafanyika lakini maeneo mengine ya jiji hili yanasikitisha. Moja ya haiba ya mtu ni usafi hebu kila mtu na aazimie kuanzia leo kwamba, hatatupa taka ovyo na tuone jiji letu litakuwa katika hali gani.Kutokana na mazoe mabaya hata sehemu ambazo kuna madebe ya taka mtu utamuona anatupa taka chini.