Tuiangalie kaspersky antivirus 2010

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Kampuni ya Kaspersky imekuwa ni miongoni mwa makampuni makubwa ya Kutengeneza programu za masuala ya Ulinzi na usalama wa computer kama Antivirus na Internet Security na ni miongozi mwa kampuni chache za ulaya ya mashariki kujipatia soko kubwa la bidhaa hizi sehemu mbalimbali duniani .

Bidhaa ninayoitaja leo hii ni Kaspersky Antivirus 2010 , kwa ufupi unaweza kuiita KAV2010 ni moja ya antivirus nzuri katika soko mpaka hapa siwezi kusema bora kuliko zote kwa sababu hivi antivirus zinapishana kwenye vitu vingi tu lakini kujua hilo mpaka ujaribu kutumia wewe mwenyewe .

Pamoja na kwamba Kaspersky wanazifanya bidhaa zao ziwe bora zaidi na kwa bei nzuri bado kuna wahalifu ambao wanajaribu kuharibu soko na bidhaa hizi kwa kutengeneza Leseni bandia na kuuzia watu wengine na wengine hata kuuza kwa watu lakini pindi unapoitumia computer hiyo kwenye mtandao basi ndio utajua kama leseni hiyo ni halali au la .

Wakati una weka programu hii kwenye computer kuna hatua chache ambazo inabidi uwe nazo makini sana ili unapoanza kuitumia chochote kikitokea usilaumu wala kushituka baada ya kukubaliana na maelezo ya mtumiaji kuna Kaspersky Security Network Data Collection ukikubaliana na huduma hiyo ina maana kampuni ya kaspesky itakuwa inakusanya baadhi ya taarifa toka kwenye computer yako jinsi unavyotumia antivirus hiyo kwa ajili ya kuboresha soko lao na bidhaa zao zingine nakushauri usikubaliane na huduma hii kwa sababu inawezekana taarifa hizo kwenda kutumika kwenye masoko mengine au wahalifu wanaweza kuingilia baadhi ya taarifa hizo na kukudhuru .

Kitu kama hicho ni sawa na spynet ambayo iko kwenye windows defender hii ni antivirus ya Microsoft windows hata hivyo unaweza kuendelea na installation ya KAV2010 kama ukikataa au ukikubali ukishamaliza kuweka antivirus hii sio lazima uzime na kuwasha upya computer yako tofauti na matoleo ya nyuma ambayo yalikulazimisha kufanya hivyo .

Pamoja na hayo yote kwenye KAV2010 kuna vitu kama File Antivirus ambayo inapambana na matishio yanayojulikana ya virus , Mail antivirus hii inakulinda dhidi ya Email zako , Webantivirus Hii inakulinda dhidi ya mitandao , Im antivirus hii inaweza kulinda mashambulio dhidi ya mawasiliano ya papo kwa hapo kutumia yahoo au msn messenger , AntiPHIshing hii ni dhidi ya mitandao na wizi wa njia ya mtandao .

Vitu vingine ambavyo viko kwenye toleo hili ni Virtual Keyboard , rescure disk kwa wale wanaopenda kutengeneza disk za kurepair computer zao pindi zinapoleta shida , Browsertune up hii inahusika na browser yako unayoitumia kutembelea mitandao , kuirekebisha na kusahihisha baadhi ya vitu katika utendaji wa kazi , privacy cleaner hii inasaidia sana kam aunataka kufuta vitu na mengine ambayo hutaki yajulikane unapomaliza kutembelea mitandao , windows settings troubleshooting Utility , hii inakusaidia kuangalia Settings kwenye computer yako kama automatic updates inafanya kazi na vingine vingi , Spacial Game Mode hii ni kwa ajili ya wale wanaocheza games kupitia mtandao , Browser Helper hii ni sawa na Link scan kwenye AVG 9.0 au WebAdvisor kwenye Mcafee hii inaweza kukusaidia kujua kurasa na tovuri unazotembelea kama ni salama au la ,kwenye hili yao KAV 2010 wanatakiwa wajitahidi sana kwa sababu kuna baadhi ya tovuti inashindwa kuzitambua kama si salama au la .

Kwa Wale wanaotumia computer ambazo hazijaunganishwa kwenye mtandao wanashida moja ya ziada haswa kwenye upande wa antivirus ni pale wanapotaka kuupdate antivirus zao bila mtandao wakati mwingine hizi updates zinaweza kuwa zimeaharibika au zina tatizo fulani kwahiyo ikashindwa kufanya kazi au ikaleta matatizo mengine kwenye computer hiyo .

Tatizo hili limeleta usumbufu sana mpaka watu wanaamua kubadili antivirus mara kwa mara unapoongelea Kaspersky antivirus 2010 moja ya kitu kizuri ambacho inauwezo wa kufanya tofauti na zingine ni uwezo wa kurudisha antivirus yako ilivyokuwa kabla ya kuweka update mpya kama uliweka ikaleta matatizo kwenye computer yako au kifaa chako .

Ikumbukwa pia huduma hii ipo pia kwenye computer zile zenye windows huduma hii inaitwa SYSTEM RESTORE na hata baadhi ya programu nyingi siku hizi za kushugulika na ufundi wa computer zimekuja na utility ambayo inauwezo wa kufanya kazi hiyo ,tofauti yake ni kwamba kuna baadhi ya virus wanaweza kuharibu files zinazohusiana na SYSTEM RESTORE na kufanya mtu asiweze kutumia programu hiyo atakapotaka kutumia .

Aina hii mpya ya Kaspersky 2010 inauwezo wa kufanya kazi katika computer zilizowekwa windows XP , Vista , 7 itafanya kazi kwenye Biti 32 na 64 lakini ukiwasha computer kwenye safe mode haitoweza kufanya kazi kwenye Biti 64 antivirus nyingi haziwezi kufanya kazi kwenye safemode lakini kuna nyingine kama mcafee virus scan 7.0 mpaka 8.7 hizi zinauwezo wa kufanya kazi kwenye safe mode lakini kama unataka kuitumia kuscan na kuondoa virus tu .

Computer ikiwa kwenye safe mode haitoweza kuwasha programu nyingi lakini itawezesha zile muhimu kwa ajili ya utumiaji wa computer kama mouse , keyboard na vitu vya kuchomeka kama flashdisk na CD ukiwa kwenye safe mode unauwezo wa kurekebisha baadhi ya matatizo ya computer yako kwa kutumia baadhi ya programu zinazofanya kazi kwenye safemode au zingine ambazo ni za system yenyewe kuna wakati pia computer inaweza isiwake kwa njia za kawaida bali ni safemode tu .

Hayo ni maelezo mafupi kuhusu KAV2010 Kaspersky 2010 kama unaona kuna lolote limesahaulika au la kuongezea karibu katika mjadala zaidi kwenye sehemu ambapo utakuta maelezo haya na kama unapenda kuitumia popote ,itumie tu si lazima uweke jina langu tumia unavyotaka .
Na kabla hujaamua kuweka antivirus kwenye computer yako hakikisha computer yako haina matatizo mengine yanayoweza kusababisha antivirus hiyo isiingie virus au hata ikiingia isiweze kufanya kazi kama inavyotakiwa ifanye mambo hayo ni kuhakikisha operating system yako haina shida yoyote nyingine na ina memory ya kutosha kuweza kutumia antivirus hiyo bila kuwa slow , harddrive inatosha na antivirus hiyo uwe umenunua kihalali .

Mchana Mwema

Usisahau Kutembelea

www.naombakazi.com Kwa nafasi za kazi

www.wanabidii.net Kwa majadiliano Mbali mbali

www.askmaro.blogspot.com kwa Maelezo mbalimbali kuhusu programu na makala .

Yona F Maro
 
Back
Top Bottom