KKKT aliondoka analo Dk. Samson Mushemba. Baada ya hapo ni vurugu vurugu tupu. Tumaini University Dar es Salaam iko hovyo hovyo, Iringa imejitoa kwenye mwamvuli wa Tumaini nayo inasifika sana kwa UKABILA, Tumaini Mbeya hali ni hiyo hiyo, Kule Kagera sina hata haja ya kueleza. Stefano Moshi University nayo ni kama Kata ya Sharibwani kule Machame, Sebastian Kolowa ndio kabisaaaaaaaaaaa, Mke wa askofu ndiye mkuu wa chuo, akiamua anatimua akiamua anakuwa yeye ndo mhasibu mradi vurugu tu. Lutheran Junior Seminaries ziko hoi bin taaban. Sharika na Dayosisi ni vilio na manung'uniko tu! Daah!