Tuhuma za upendeleo kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Tumaini Makumira

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,632
40,790
Zipo tuhuma za chini kwa chini na hali ya kutokuridhika na namna ambavyo mkuu wa chuo cha tumaini makumira alivyotoa nafasi kwa mwanae wa kiume kupata mafunzo ya elimu ya juu kwa level ya masters na phd kwa sasa ukiacha wakufunzi wengine wenye sifa.

Mwanae huyo anayepata mafunzo ya juu huko marekani alikua mmoja wapo wa wakufunzi wasaidizi mara tu baada ya kumaliza shahada ya kwanza.

Baadhi ya wakufunzi waliopo na waliondoka wanasema kwamba nafasi hiyo ilitolewa pasi na kuzingatia vigezo na kwa upendeleo, ukizingatia kwamba makamu mkuu wa chuo ni baba mzazi wa mkufunzi msaidizi aliyepata nafasi hiyo.
 
Ni nani anayemtuhumu chini kwa chini na kwanini afanye chini kwa chini

Anyway nitacomment baada ya huyo Mkuu wa Chuo kuja hapa na kujibu tuhuma
 
1.hizo nafasi ni za ushindani?
2.ni scholarship ya course gani?
3.kwa nini unadhani hakuwa na vigezo vya kupata hiyo scholarship?
4.je akidai anajilipia 50% ya ghalama atakuwa amekosea?
 
Arudishwe nchini na mchakato uanze upya!wanao lalamika wapeke malalamiko yao sehemu stahiki manake hawa ndio wanakuja kua madoctor na maprofesor wanaolialia na hawaisadii nchi! Rejea yule mkuu wa wilaya huko morogoro nk
 
KKKT aliondoka analo Dk. Samson Mushemba. Baada ya hapo ni vurugu vurugu tupu. Tumaini University Dar es Salaam iko hovyo hovyo, Iringa imejitoa kwenye mwamvuli wa Tumaini nayo inasifika sana kwa UKABILA, Tumaini Mbeya hali ni hiyo hiyo, Kule Kagera sina hata haja ya kueleza. Stefano Moshi University nayo ni kama Kata ya Sharibwani kule Machame, Sebastian Kolowa ndio kabisaaaaaaaaaaa, Mke wa askofu ndiye mkuu wa chuo, akiamua anatimua akiamua anakuwa yeye ndo mhasibu mradi vurugu tu. Lutheran Junior Seminaries ziko hoi bin taaban. Sharika na Dayosisi ni vilio na manung'uniko tu! Daah!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom