Tuhuma kwa watu walioaminiwa na Rais 100%, Rais anajifunza nini?

Nibozali

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
572
1,055
Habari wakuu,

Leo nimeamua kuja na ushauri kwa Rais wangu mh Dr. Pombe M. Baada ya kuona juu ya namna viongozi aliowaamini 100% wakigeuka na kumuaibisha katika nyadhifa alizowapatia.

1. Nikianza na Makonda
Makonda ni miongoni mwa watu walioaminiwa na Rais wetu kama viongozi wachapakazi jambo lililopelekea kukabidhiwa jumkum La kuongoza jiji LA Dar

Nini ambacho Rais wangu alikosea na sasa kinamgarimu?
Mara tu Rais wangu alipomteua Makonda aliudhihirishia umma kuwa makonda ni kiongozi ambaye kwa namna yoyote hana chembe wala harufu ya uongozi mbaya kwa maana ya rushwa, uzembe uvivu. Alisikika mara kadha akimtolea mifano katika ziara zake za ndani na nje ya mkoa Wa dar. Suala hili linamgharimu kwa sasa pamoja na tuhuma chafu zinazomkabili Makonda kwa sasa zinamfanya Rais wetu aendelee kubaki kimya kwa sababu anashindwa apite njia ipi kuja kuudhihirishia umma Wa watanzania aliouaminishia kuwa kiongozi huyo hakuna kama yeye

Atawaambia nini watanzania na atattumia njia gani? Ndio maana ameendelea kukaakimya ili kuficha Aibu ambayo inaweza kuibuka.

2. Harrison Mwakembe
Huyu nae sina haja ya kueleza sana lakini kwa ufupi ni miongoni mwa watu walioaminiwa na Rais kwa masuala ya sheria lakini kinyume chake ni kama mzee huyu hakuwahi kuingia darasa LA sheria kwani anafanya ujingsujinga tu kwa nafasi aliyopewa suala linalopelekea watu kuhoji usomi wake Wa sheria.

3. Muhongo
Huyu amendelea kuwa mpiga madili kama ilivyo kawaida take

Ushauri kwa Rais
Weka akiba ya maneno pindi unapowapa motivation wale viongozi wanaokuwa wamekufurahisha kwa utendaji wao. Elewa kuwa asilimia kubwa ya viongozi tulionao ni wapiga dili, watakuaibisha kama inavyotokea sasa hivi. Wengi wanajaribu kutengeneza ukaribu mkubwa kwako ambao unasababisha ushindwe kutoa maamzi sahihi kwa kumuonea aibu au huruma kama ujanja aliotumia makonda. Pale hauna namna na hatachukua hatua zozote zaidi ya kumtetea maana ukichukua hatua sahihi dhidi yake maneno yako uliyoyasema kuhusu yeye kipindi cha nyuma yatakuhukumu

Ni hayo tu
 
Mwakyembe ndiyo amedhalilika sana mahakamani kwenye ishu ya TLS kapigwa Kata funua na Lissu, huku kwenye kufunga ndoa mpaka vyeti vya kuzaliwa kapigwa za kichwa na Magufuli sasa hivi yupo hoi
 
Hii inaonyesha sub-standard kwa serikali ya Magufuli..


Mbona wengine walipigwa chini fasta.

Mf:
Anne kilango
Marehemu mzee kabwe

Na wingine....


Magufuli is proving failure!
 
Hili la Mwakyembe ndio limeniacha hoi, kuanzia tamko mpka katazo............binafsi sikuelewa kabisa maana ya kuwa na vyeti vya kuzaliwa na masuala ya ndoa, hii Nchi mbona ina mambo mengi ya msingi yanayohitaji kusimamiwa zaidi ya ndoa, Mwakyembe ajitafakari, kama nia ni kumfurahisha Mkuu basi kuna kazi kubwa sana huko Serikalini.
 
Back
Top Bottom