Tufungeni mikanda kama 1980s

sikajiji

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
588
113
Tunarudishwa miaka 36 nyuma ya bidhaa adimu;

Kiafrika Mtu akishakufa siyo vizuri kuusema ubaya wake maana mwenyewe hayuko kujitetea.

Lakini anapokuwa hai, hata kama ni uhai unaosaidiwa na mitambo, bado watesi wanaruhusiwa kuusema ubaya wake ili akipona ajirekebishe.

Na asipopona basi itawabidi watesi wanyamaze kimya wawasikilize mashabiki wake wakisema uzuri wa Mwalimu wa kuwakomboa Watanzania kutoka katika minyororo ya ukoloni wa Waingereza na kuwaigiza kwenye ukoloni mwingine wa Julius Kambarage Nyerere.

Ukoloni wa kwanza haukuwa mbaya kuliko huu wa pili,ila tofauti yake ni kwamba ukoloni wa pili uliongozwa na Mwafrika kutoka Butiama, na ule wa kwanza uliongozwa na mzungu kutoka Uingereza.

Kwa hiyo tofauti ilikuwa ni viongozi wa ukoloni, na Watanzania hawakutoka katika minyororo ya ukoloni, bali walibadilika kutoka ukoloni huu kungia mwingine ambao ndio unaowatawala mpaka leo.

Kwa watu wenye mawazo kama mimi, ni heri tungebaki kama tulivyokuwa maana msaada wa kweli ungetoka popote, kuliko kujidanganya kuwa tulikuwa salama na kumbe ukweli wa mambo ni kwamba tulikuwa pabaya kuliko mwanzo.

Ilikuwa kama kukimbia mvua na kuingia kwenye kibanda cha nyasi kinachovuja. huwezi kueleza tofauti maana bado unanyeshewa.

Na mpaka leo Watanzani kama mimi hatujui tofauti ya kuwa huru na kutawaliwa.

Ikiwa kuwa huru ni kumruhusu Nyerere kujaribia mawazo yake ya siasa ya ujamaa kwenye maisha yetu na baada a miaka 30 atuambie mawazo yake yalishindwa kwa sababu alikosea, na adhabu tuliyompa ni cheo cha baba wa Taifa, basi mtanisamehe nikisema kuwa mwacheni huyo mzee apumzike kwa amani kutoka katika dunia hii, ili akapate nafasi ya kukutana na Muumba wake ambaye akiamua kumsamehe amsamehe.

Na pia akiamua kumhukumu yote ni sawa, lakini siwezi kumwomba Mungu amponye Nyerere aje kufanya nini? Ambacho hakukifanya kwa miaka yote 77 aliyoishi duniani? alitumia nusu ya maisha yake kufanya majaribio na Watanzania,na sasa Mungu atatushangaa kwamba tunamsumbua amponye.

Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu, na hawezi kukubali kushiriki utukufu wake na Nyerere.Amewaona Watanzania wanamwabudu Nyerere kuliko yeye na ameamua kumchukua ili wajue kuwa wanaweza pasipo Nyerere.

Tena Yeye Mungu pekee ndiye Baba wa vyote. lakini wanadamu wanamwita mwanadamu baba wa taifa? hiyo ni kufuru. Elimu ni nzuri, lakini ile inayotoka kwa Mungu.

Hii ya wanadamu mara nyingi inakuwa na kasoro nyingi.na wale waliyo nayo husahau kumtegemea Mungu,na kuitegemea elimu yao ambayo mara nyingi inashindwa kuwatatulia matatizo.

Elimu ya madarasani na uongozi ni vitu viwili tofauti lakini wanadamu huvutiwa sana na viongozi waliosoma wanasahau kuwa uongozi unatoka kwa Mungu.Na mara nyingi hawa viongozi waliosoma hawaongozi vizuri.

Tuna mifano mingi, lakini Nyerere ni mmoja wa hao viongozi wasomi ambao hawakuongoza vizuri.Hotuba nzuri, maneno ya kushawishi akili na kupendwa na waandishi wa habari siyo cheti cha kiongozi mzuri.

Na Nyerere anasifiwa kwa hiyo lakini ukija kwenye matendo ya zile hotuba nzuri hakuna hata kijiji kimoja cha maonyesho kuonyesha kuna msomi mmoja aliyewahi kufikiri kuhusu vijiji vya ujamaa na hiki ni kimoja ya vijiji alivyovianzisha, na watu katika kijiji hiki wanafurahia mawazo ya msomi huyo.

Lakini Tanzania nzima hakuna hata kijiji kimoja cha ujamaa kilichobaki kama maonyesho ya mawazo ya msomi Nyerere badala yake Tanzania ni moja kati ya nchi masikini duniani.

Na yote hayo ni matunda ya msomi mmoja waliyemwita Mwalimu wa umasikini.Sasa mambo yakiwa hivyo najiuliza kwa nini alipoteza muda kwenda Makerere kupata shahada ya DR. ambayo haikumsaidia kuifanya Tanzania mahali pazuri pa kuishi?

Bado nasita katika njia mbili, sijui nimpeleke mtoto wangu Makerere apate shahada kama ya Nyerere ndipo aje agombee uongozi wa Tanzaia, au tumtegemee Mungu atupe kiongozi ambaye ataongoza vizuri hata kama hana karatasi ya chuo kikuu?

Na kama Mungu anaweza kutupa kiongozi basi hata mimi niko tayari maana kile ambacho sina ni karatasi ya chuo kikuu tu.Na kama Nyerere DR. anaweza kushindwa mambo mengi hivyo, basi nina hakika siwezi kushindwa kama yeye.

Kwa Watanzania ni vizuri Nyerere aondoke ili tuwe na mawazo mapya na mbinu mpya za kuikomboa kikweli Tanzania.

Hata Musa alipokufa ,Yoshua alifanya makuu kuliko Musa Na Yoshua wa Tanzania ni mimi Faustin S. Munishi

Munishi - Nyerere Alishindwa
 
Kuandika mistari mingi sana iliyojaa lawama hakuwezi kukisaidia kizazi che leo na kile cha kesho, kukosoa kitu alichofanya mtu fulani ni tofauti na kuanzisha cha kwako mwenyewe, ndio maana nchi kama Marekani na hata Ulaya ya kaskazini mwanzilishi wa idea fulani huja kuwa tajiri kwa sababu yeye ndio anayeonyesha njia kwa wengine.

Mwalimu Nyerere alishakiri hadharani kwamba baadhi ya utekelezaji wa sera alizoziamini haukuweza kuleta tija ambayo ilitegemewa kuonekana. Kumbuka Mwalimu aliweza kuiunganisha nchi, mchagga akaja kuoa dada wa kihaya, Mhaya akaja kuoa dada wa kingoni. Mngoni akaja kuoa mzaramo, nchi ikawa ni kitu kimoja.

Kumbuka kuwa kufanikiwa kiuchumi haswa kwa nchi za kiafrika huwa hakuna muendelezo unaodumu. Libya iliyokuwa inawalipa mshahara raia wake ikaja kuhujumiwa na Marekani na Uingereza. Kina Angola na umaarufu waliokuwa nao enzi za miaka ya 80, wamekuja kufanyiwa ufisadi mkubwa na familia ya rais ambaye amedumu madarakani kwa miaka mingi.

Hata huu utulivu ambao leo hii unaonekana sio kitu ni matunda ya vision ya Nyerere na wasaidizi wake. Mwalimu Nyerere alikuwa ni binadamu mwenye kutenda dhambi lakini angalau hata katika enzi ambazo wenzetu walikuja kuingia kwenye mitego ya vita na mifarakano, yeye aliweza kujenga hoja za kibinadamu ambazo zimechangia kulifanya taifa liweze kudumu kwa muda mrefu.
 
SO WHAT?
 
Vipi bado mkimbizi Kenya? Band yako ya familia inaendeleaje? You ran away instead of staying home and fight for what you beleave halafu unatutaka tukusikilize. Tuache sisi tulioishi hata kabla ya hiyo 80s na bado tunadunda. Endelea kutumbuiza ndo talanta yako.
 
Thread mzima imejaa lawama!!! Hivi huku ni kujenga ama kubomoa???? Watu wa JF ni nooma aiisee, hawaishiwi kuponda kila lifanywalo na kiongozi.
 
Wenye kunielewa wamenielewa na hicho ndicho kitu muhimu zaidi. Kumnyooshea mtu kidole kwa shida ambazo wakati mwingine uwezo wa kuzitatua wewe mwenyewe upo, sidhani kama ni busara. Ukiamua kuwajadili marais wote waliopita hapa nchini tangu uhuru, nina uhakika hautumkuta malaika hata mmoja.
 
dole

jamii forum ni ya nini kama ndivyo. kwani humu twatafuta malaika
 
Unayo haki ya kuwakilisha maoni lakini uwe fair kwa marais wote, usitake kujenga hoja kwa kumnyooshea kidole moja kana kwamba ndio source ya taabu zote tulizonazo. Kumbuka enzi ya Nyerere wasomi walikuwa wanahesabika, kumbuka challenges za Afrika baada ya uhuru, usiilinganishe Afrika ile na hii ya sasa iliyojaa smartphones za kila aina, iliyojaa marubani wa ndege kila kona. Afrika ya awamu ya kwanza ilikuwa bado ipo gizani hatukuwa na taasisi zozote ambazo ni imara, mind you mpaka leo hii bado tunajenga aina ya maisha yenye kufuata mifumo ambayo bado hatuijui vizuri.
 
Kama tumeachiw

Tulitakiwa kujengewa msingi imara ilin tuweze kwenda mbele. Hilo halikuwepo na ndiyo tatizo lilipoanzia. Wasomi nchii hi walikuwepo ila wengi wao hawakupewa nafasi kwa kuogopa kuwa overshadowed..
The Serpent-hearted Politician
.
 
Thread mzima imejaa lawama!!! Hivi huku ni kujenga ama kubomoa???? Watu wa JF ni nooma aiisee, hawaishiwi kuponda kila lifanywalo na kiongozi.
Mtambo wa kurekebisha huu siyo kusifia
 
Kama tumeachiw

Tulitakiwa kujengewa msingi imara ilin tuweze kwenda mbele. Hilo halikuwepo na ndiyo tatizo lilipoanzia. Wasomi nchii hi walikuwepo ila wengi wao hawakupewa nafasi kwa kuogopa kuwa overshadowed..
The Serpent-hearted Politician
.
Azimio la Arusha ulikuwa ni msingi uliojengwa na Nyerere, lengo likiwa kuweka usawa miongoni mwa watu wa nchi changa. Mwaka 1992 lilivunjwa kule Zanzibar, kilichofuata mimi na wewe ni mashuhuda wake. Ufisadi na unyama wa kila aina, ni mambo ambayo yameendelea kuwepo hata baada ya Mwalimu Nyerere kuwa ameshazikwa kaburini kule butiama.
Misingi iliwekwa, vizazi vilivyofuata vikaibomoa bila aibu. Wasomi walikuwa wachache sana, teknolojia ilikuwa ndogo, enzi zile ilikuwa rahisi kukutana na mesenja posta mpya akipeleka barua kutoka wizara moja kwenda nyingine, siku hizi kwa sababu ya maendeleo ya mitandao kila kitu kinatumwa kupitia email.
Kumbuka uhalisia wa dunia kabla hujamtupia zigo la lawama mwalimu JKN.
 
Kuandika mistari mingi sana iliyojaa lawama hakuwezi kukisaidia kizazi che leo na kile cha kesho, kukosoa kitu alichofanya mtu fulani ni tofauti na kuanzisha cha kwako mwenyewe, ndio maana nchi kama Marekani na hata Ulaya ya kaskazini mwanzilishi wa idea fulani huja kuwa tajiri kwa sababu yeye ndio anayeonyesha njia kwa wengine.

Mwalimu Nyerere alishakiri hadharani kwamba baadhi ya utekelezaji wa sera alizoziamini haukuweza kuleta tija ambayo ilitegemewa kuonekana. Kumbuka Mwalimu aliweza kuiunganisha nchi, mchagga akaja kuoa dada wa kihaya, Mhaya akaja kuoa dada wa kingoni. Mngoni akaja kuoa mzaramo, nchi ikawa ni kitu kimoja.

Kumbuka kuwa kufanikiwa kiuchumi haswa kwa nchi za kiafrika huwa hakuna muendelezo unaodumu. Libya iliyokuwa inawalipa mshahara raia wake ikaja kuhujumiwa na Marekani na Uingereza. Kina Angola na umaarufu waliokuwa nao enzi za miaka ya 80, wamekuja kufanyiwa ufisadi mkubwa na familia ya rais ambaye amedumu madarakani kwa miaka mingi.

Hata huu utulivu ambao leo hii unaonekana sio kitu ni matunda ya vision ya Nyerere na wasaidizi wake. Mwalimu Nyerere alikuwa ni binadamu mwenye kutenda dhambi lakini angalau hata katika enzi ambazo wenzetu walikuja kuingia kwenye mitego ya vita na mifarakano, yeye aliweza kujenga hoja za kibinadamu ambazo zimechangia kulifanya taifa liweze kudumu kwa muda mrefu.
Uzi mrefu kwa uvivu wako wa kufiri na kusoma between the lines. "mchagga akaja kuoa dada wa kihaya, Mhaya akaja kuoa dada wa kingoni. Mngoni akaja kuoa mzaramo, nchi ikawa ni kitu kimoja." myopic reasoning
 
Azimio la Arusha ulikuwa ni msingi uliojengwa na Nyerere, lengo likiwa kuweka usawa miongoni mwa watu wa nchi changa. Mwaka 1992 lilivunjwa kule Zanzibar, kilichofuata mimi na wewe ni mashuhuda wake. Ufisadi na unyama wa kila aina, ni mambo ambayo yameendelea kuwepo hata baada ya Mwalimu Nyerere kuwa ameshazikwa kaburini kule butiama.
Misingi iliwekwa, vizazi vilivyofuata vikaibomoa bila aibu. Wasomi walikuwa wachache sana, teknolojia ilikuwa ndogo, enzi zile ilikuwa rahisi kukutana na mesenja posta mpya akipeleka barua kutoka wizara moja kwenda nyingine, siku hizi kwa sababu ya maendeleo ya mitandao kila kitu kinatumwa kupitia email.
Kumbuka uhalisia wa dunia kabla hujamtupia zigo la lawama mwalimu JKN.
wewe unatafsiri hivyo, kwa azimio hilo hilo una watu walitendewa dhulma na ni wengi. Ufisadi ulikuwepo, ndiyo maana mashirika ya umma hayakuweza kufika popote
 
Uzi mrefu kwa uvivu wako wa kufiri na kusoma between the lines. "mchagga akaja kuoa dada wa kihaya, Mhaya akaja kuoa dada wa kingoni. Mngoni akaja kuoa mzaramo, nchi ikawa ni kitu kimoja." myopic reasoning
Inategemea upeo wako una mipaka ipi. Nenda Nigeria uone kama kuna muunganiko wa watu wa makabila tofauti kama hapa Tanzania. Tembea nje ya nchi yako uone watu wanavyoishi kikabila na kibinafsi. Unaona ni myopic kwa sababu ya kukubali kifikra kubakia humu humu nchini, wenzetu wanajitambulisha kikabila sisi tunajitambulisha kitaifa, ndio pointi yangu, wenye kutazama masuala kwa undani wameelewa nimeandika nini. Vijana ambao ni matunda ya wazazi waliojitambulisha kama watanzania wanaelewa logic ya hicho kilichoandikwa.
 
wewe unatafsiri hivyo, kwa azimio hilo hilo una watu walitendewa dhulma na ni wengi. Ufisadi ulikuwepo, ndiyo maana mashirika ya umma hayakuweza kufika popote
Kaka hakuna kiongozi wa mwanzo wa Afrika ambaye hakufanya makosa, marais wote walioasisi bara hili wanayo makosa mengi tu lakini historia itawatendea haki. Wasomi wa viwango vya juu kwenye miaka ya 60,70 na 80 walikuwa wachache ndio maana mtu akimaliza form six na akaenda jeshini alikuwa na uhakika wa kupata kazi. Sasa huwezi kulinganisha Tanzania ile na hii ya sasa ambayo mtu wa form six hana heshima yoyote mbele ya mtu mwenye bachelor degree ambaye yupo mtaani anatafuta kazi.
 
Back
Top Bottom