Wapendwa najibu kilio chenu,
Napenda kuwakaribisha kwenye semina ya ujasiriamali, ambayo itafanyika Siku ya jumamosi tarehe 27/2/2010 saa 4.00 asubuhi katika ofisi za Princess Agness Foundation eneo la Sinza kwa Remi Dar es salaam. Mwezeshaji atakuwa ni Charles Nazi Mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara. Hakutakuwa na kiingilio semina itatolewa bure. Kama unapenda kununua vitabu vya ujasiriamali unashauriwa kuja na pesa kwani tutauza vitabu vya vya ujasiriamali. Kwa wale ambao watahudhuria semina hiyo nawaomba wathibitishe kwa kunitumia ujumbe kwenye simu namba 0755394701
CHARLES NAZI
Mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha Mbinu za biashara