Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,961
Kwanza kabisa nawasalimia wana JF wote.
Napenda kuwasilisha maoni yangu toka moyoni kuhusu EAC.
Utangulizi
Wazo la kuwa EAC niwazo zuri sana kuelekea Pan-Africanism (Unity is vital to economic, Social and Political an aim to "unify an uplift People of African descent).
Ili africa iweze tujitawala na kuwa na maamuzi yenyewe nilazima kuwa na umoja. Tunatakiwa sisi waafrika kujitabua na kutambuana, vilevile tusibaguane. Hii ndio silaha kuu muhimu kwetu sisi waafrica itakayo tukomboa.
Tatizo kubwa linayoikumba afrika ni tamaa, ubinafsi, uchoyo, ubaguzi na mengine yafananayo na hayo.
EAC ni muhimu sana kwetu sisi sote (Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi). Kitu kikubwa muhimu kinacho tuunganisha ni jamii zetu na tamaduni zetu zina shabihiana. Tumeingilia kimakabila, kitamaduni na katika nyanja zingine tofauti tofauti. Ilituweze kusonga mbele katika hatua ya kuelekea Pan-Africanism ni muhimu sana kuungana na kuweka pembeni unafiki na kujiona kua sisi au wao wanafaa kulika mwingine.
Matatizo ya EAC
Kunamatatizo mengi sana yamo ndani ya nchi za Africa mashariki mojawapo ni kung`ang`ania madaraka, Kutokubali ukweli (to be honest) Mf: haikuwa na maana kwa bwana Uhuru kwenyata "Japo kuwa anahaki ya kikatiba" kugombea uongozi wa ngazi ya juu, wakati anajua kuwa ni mtuhumiwa.
Tamaa ni moja wapo ya tatizo kubwa tulilonalo hapa afrika ya mashariki, viongozi wengi wanatamaa ya kutaka kujinufaisha wao wenyewe, hii inatafsiri kuwa viongozi hao ni waoga wa maisha. Mifano ipo mingi tu ya jambo hili.
Kujiona bora kuliko wengine, hili ni tatizo sugu tulinalo hapa EA, kujiona bora zaidi ya mwingine, na ukiangalia sio kweli maana jamii zetu zinaishi maisha yale yale tu. Wanapata msaada toka nchi za magharibi, wanasubuliwa na malaria, ukimwi na matatizo mengi lukuki.
Kutaka kufanya mambo haraka haraka kabla ya kuwaandaa wananchi. Kwanza tukubaliane kuwa mipaka ilipowekwa na wakoloni imetutenganisha, sasa kutaka kuungana tu pasipo kuwaandaa wanachi kisaikolojia, kimipango itakuwa kama kuandika nane kwenye maji.
Chuki binafsi baina ya viongozi. Hili nalo nitatizo moajawapo ambalo tunaliona wazi wazi, matokeo yake linahatalisha muungano na kuleta madhara kati ya raia wa nchi husika. Kusema kweli raia hawahusiki na tatizo.
Tufanye nini sasa.
1. Inatakiwa tuwe na malengo ya mda mrefu, kuhusu kuwaandaa wananchi kisaikolojia. Yawepo masomo shuleni yanayofundisha kuhusu Afrika mashariki, Mikutano mbali mbali kabla hata ya kuwa na ofisi za afrika mashariki. Hili viongozi hawalioni kabisa, Mipaka iliwekwa na wakoloni imetutenga na watu wameathirika kisaikolojia, kwa hiyo basi tuwe na lengo la mika 10 kuwaandaa wananchi, kuweka tofauti pempbeni kuwa huyu ni mkenya, mrwanda, mrundi, mganda au mtanzania. Hapa tutakuwa na jukuia imara na yenyetija.
2. Afrika mashariki ni muhimu sana kuliko viongozi waliopo madarakani sasa. Viongozi hawa watapita lakini Afrika mashariki itabaki. Sasa basi wanatakiwa wafuate misingi ya makubaliano. (Hapa nina maanisha misingi [root]). Kwamba nikitu gani cha msingi wamekubaliana? na wasimamie hicho sio kila baada ya kubadilisha uongozi makubaliano yanabadilika.
3. Kutoka kwenye poiti ya namba 1. Baada ya kufanya hivyo kutakuwa hakuna kudharauliana.
4. Ianzishwe falsafa ya afrika mashariki ambayo kila nchi itaanza kuitumia ndani ya mikaka 10 na ndipo hapo sasa tutakuwa na Afrika mashariki yenye jamii inayo fanana. Lakini kuruka ruka tu pasipo kuwa na mipango mathubuti itakuwa nikama kutwanaga maji kwenye kinu.
4. Haya mambo Economic, Polotical na mengine yatafata baada ya Social integration.
Sasa hivi tunakimbili kwenye sarafu moja, visa moja, Economical integration na mengine yanayo fanana na hayo ambayo ni upuuzi na kupoteza mda. Kitu kikubwa ni kuanza na Social integration kwanza. Jamii zetu zikiungana na kuheshimiana tayari kila kitu kitakuwa sawa.
Nina wasilisha hoja haya ni mawazo yangu unaweza ukaongezea, ukachambua zaidi, ukanitoa kasoro. Lakini lengo ni kujenga sio kubomoa.