Tufanye ni 2025 Magufuli katoka, Rais mpya kaunda tume ya kuchunguza awamu ya JPM

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,116
Kila nikiwaza nakosa majibu labda wenzangu mnisaidie. Hebu tuchukulie sasa tuko 2025 JPM katawala miaka yake 10 na kustaafu!! Kaingia rais mpya tumpe jina Abunwasi!! Abunwasi anaingia kwa makeke kuliko ya JPM Ya sasa! Anasimamisha mwenge na mbio zake na kuupeleka makumbusho! Watu tukapiga makofi kama tulivyompigia JPM wakati anaingia kwa kusitisha sherehe za uhuru na hela kujengea barabara. Mbwembwe tufanye ziishie hapo na maisha yaendelee kama sahiz hamna kiki hizo.

Baada ya hapo aunde tume kuchunguza utendaji wa awamu hii!! Kitu cha kwanza aanze kukagua hesabu za manunuzi ha ndege bombadia zile tulizo ambiwa ni mpya na tumelipa keshi!!

Mara ile tuliotaka kupigwa cha juu tukapiga kelele mpaka wametubadirishia na kutupa nyingie.

Tume ikaenda mpaka kwenye ujenzi wa reli . Ile tunaambiwa ni ya mwendo kasi japo si kweli ila ni standard gauge!! Ambayo rais wetu mtukufu kasema tunajenga na hela za ndani!

Tume ikaenda mbali zaidi na kwa kukagua ujenzi wa uwanja wa chato!!

Tume ikague mpaka hela zinazo toka ikulu kuajili watumishi wa afya bila kupitia wizarani ila kwa maagizo ya rais!!

Tume ikague mpaka zile hela za ujenzi wa barabara kwa pesa ya sherehe za muungano kule mwanza!

Tume ikague mpaka kivuko cha bagamoyo ambacho leo tumeambiwa ni cha kijeshi ukihoji ni kama kuhoji mabomu ya jeshi!

Baada ya ukaguzi huo tume ikaja na majibu na kuona kulikua na ufisadi wa kutisha . Wakatia na huruma na kumliza Abunwasi (rais wa wakati huo) mheshimiwa Abunwasi aanze kufoka!! Wale waliokua watendaji wa awamu ya tano wachukuliwe hatua. Wa kwanza kuwekwa ndani awe waziri wa uchukuzi wa kipindi hiki kwa kununua ndege za kizamani kwa bei ya mpya!! (Tume ndio imebaini) na pia kwa kujenga reli kwa bei ya kuruka. Hivi Abunwasi si atakua anamwonea waziri wa uchukuzi kwa kweli?? Hivi kuna anachokifanya waziri wa uchukuzi kama sio yote yanafanywa na JPM??

Aende kwa waziri wa afya hela za kuwaajiri wale madaktari waliotaka kwenda kenya inaonekana mmezidisha ilikuwaje? Atasemaje huyu mama kama sio kutupia mpira kwa JPM??

Nifupishe kwa kuuliza hivi kuna kitu wanafanya mawaziri wa sasa bila baraka za JPM?? Ikitokea utawala mwingie wa ndugu abunwasi uwaambie watanzania tumwache JPM apumzike kwa kazi yake iliyotukuka, hahusiki kwa lolote si itakua kuwaonea mawaziri wa sasa! Na kutufanya wajinga tunaoona yanayoendelea sasa?? Mnaotetea sasa kwamba marais wastaafu wasiguswe bali mawaziri na watendaji wengine mbona sifa zote za utendaji wa serikali hii anapewa MAGUFULI na si watendaji wake!? Kwahiyo mnataka sifa wapate marais lakin lawama wapewe watendaji!!

MAMBO YOTE MABAYA YA AWAMU ZILIZOPITA BILA KUWAHUSISHA MARAIS WALIOKUWEPO NI UPUMBAVU!

Mabaya yooote yaliopita yalifanywa kwa baraka za viongozi wakuu. Kukataza kuwataja maraisi wasitaafu haisadii ila inazidisha hasira kwetu sisi tunaojielewa!!
 
Abunwasi.. atapewa sifa nyingi sana na huyu ataonekana ametupiga sana lakini tutakatazwa tusimtaje mahali popote,kisha tutaanza kulalamika kama sasa.
 
Kama JPM akisoma huu uzi.....ataacha kuwasumbua watendaji wa awamu zilizopita!! Ni busara ndogo tu!! Chenge amejibu kuwa aliemtuma ku sign. Mikataba ile ndie huyo aliemtuma na yeye kuuza zile nyumba za umma na yeye akachukua zaidi nyumba 5 kuwapa ndugu na vimada
 
Kila nikiwaza nakosa majibu labda wenzangu mnisaidie. Hebu tuchukulie sasa tuko 2025 JPM katawala miaka yake 10 na kustaafu!! Kaingia rais mpya tumpe jina Abunwasi!! Abunwasi anaingia kwa makeke kuliko ya JPM Ya sasa! Anasimamisha mwenge na mbio zake na kuupeleka makumbusho! Watu tukapiga makofi kama tulivyompigia JPM wakati anaingia kwa kusitisha sherehe za uhuru na hela kujengea barabara. Mbwembwe tufanye ziishie hapo na maisha yaendelee kama sahiz hamna kiki hizo.

Baada ya hapo aunde tume kuchunguza utendaji wa awamu hii!! Kitu cha kwanza aanze kukagua hesabu za manunuzi ha ndege bombadia zile tulizo ambiwa ni mpya na tumelipa keshi!!

Mara ile tuliotaka kupigwa cha juu tukapiga kelele mpaka wametubadirishia na kutupa nyingie.

Tume ikaenda mpaka kwenye ujenzi wa reli . Ile tunaambiwa ni ya mwendo kasi japo si kweli ila ni standard gauge!! Ambayo rais wetu mtukufu kasema tunajenga na hela za ndani!

Tume ikaenda mbali zaidi na kwa kukagua ujenzi wa uwanja wa chato!!

Tume ikague mpaka hela zinazo toka ikulu kuajili watumishi wa afya bila kupitia wizarani ila kwa maagizo ya rais!!

Tume ikague mpaka zile hela za ujenzi wa barabara kwa pesa ya sherehe za muungano kule mwanza!

Tume ikague mpaka kivuko cha bagamoyo ambacho leo tumeambiwa ni cha kijeshi ukihoji ni kama kuhoji mabomu ya jeshi!

Baada ya ukaguzi huo tume ikaja na majibu na kuona kulikua na ufisadi wa kutisha . Wakatia na huruma na kumliza Abunwasi (rais wa wakati huo) mheshimiwa Abunwasi aanze kufoka!! Wale waliokua watendaji wa awamu ya tano wachukuliwe hatua. Wa kwanza kuwekwa ndani awe waziri wa uchukuzi wa kipindi hiki kwa kununua ndege za kizamani kwa bei ya mpya!! (Tume ndio imebaini) na pia kwa kujenga reli kwa bei ya kuruka. Hivi Abunwasi si atakua anamwonea waziri wa uchukuzi kwa kweli?? Hivi kuna anachokifanya waziri wa uchukuzi kama sio yote yanafanywa na JPM??

Aende kwa waziri wa afya hela za kuwaajiri wale madaktari waliotaka kwenda kenya inaonekana mmezidisha ilikuwaje? Atasemaje huyu mama kama sio kutupia mpira kwa JPM??

Nifupishe kwa kuuliza hivi kuna kitu wanafanya mawaziri wa sasa bila baraka za JPM?? Ikitokea utawala mwingie wa ndugu abunwasi uwaambie watanzania tumwache JPM apumzike kwa kazi yake iliyotukuka, hahusiki kwa lolote si itakua kuwaonea mawaziri wa sasa! Na kutufanya wajinga tunaoona yanayoendelea sasa?? Mnaotetea sasa kwamba marais wastaafu wasiguswe bali mawaziri na watendaji wengine mbona sifa zote za utendaji wa serikali hii anapewa MAGUFULI na si watendaji wake!? Kwahiyo mnataka sifa wapate marais lakin lawama wapewe watendaji!!

MAMBO YOTE MABAYA YA AWAMU ZILIZOPITA BILA KUWAHUSISHA MARAIS WALIOKUWEPO NI UPUMBAVU!

Mabaya yooote yaliopita yalifanywa kwa baraka za viongozi wakuu. Kukataza kuwataja maraisi wasitaafu haisadii ila inazidisha hasira kwetu sisi tunaojielewa!!
Rais Sugu
 
Back
Top Bottom