Matukio yanayotokea sasa katika nchi yetu ni mchanganyiko wa mambo mengi na la msingi zaidi nionalo

kwetu sisis watanzania kulalamika kwamba hali ngumu na viongozi hawawajibiki. Ok yawezekana kweli hawawajibiki wanakula rushwa au

wanajali maslahi yao kuliko ya nchi yao na wananchi wao.

Sasa wananchi sisi tunaolalamikia kila kitu tunawajibika vipi? Utakuta mtu yupo mitaani badala ya kuwa kwenye meza yake saa za kazi na

wakati mwingine mtu yuko kazini lakini yupo kwa sababu yupo hafanyi kazi ipaswavyo ni soga tu na matokeo yake kazi zinarundikana

hazimaliziki on time! mwisho wa siku kunakuwa kuna viporo na mwisho wa yote tunaingiza hasara katika makampuni na mashirika.

Tufanyeni kazi tuche kulalamikia kila kitu bila kazi uchumi wetu utakuwaje na maisha bora yanapatikanaje bila kukuza uchumi?