Tufanyaje ili wasichaguliwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tufanyaje ili wasichaguliwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mess, May 3, 2010.

 1. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jamani hii sio story ni kitu ambacho kimeniuma sana. Kwanza nianze na ya Dodoma. Nilienda dodoma kikazi nikakuta mmbunge mmoja amemtafuta fundi Carpenter anatengeneza mabango kama yale ya project za tanroads harafu wanaenda kuyapigilia vijijini kabisaaa ambako bara bara hazipitiki harafu wameandika kuwa ni tanroads project itaanza kujenga barabara kwa kiwango cha rami na vitu kama hivyo. Na hizo bara bara hazina tija yoyote ila ni vijijini kweli kweli. Kuna ukweli hapo au mbunge anawadanganya wanachi? Na kama kuna ukweli ni budget ya lini iliyopiytisha ujenzi huo maana ni vipande virefu zaidi ya km 60-100.

  Sasa nirudi ukonga kwa mwanangu Mahanga jamani ile bara bara ya mazizini kila siku anaifanyia kampeni mara inaenda kutokezea mbagala mara itakuwa double road yote haya husikika mara tu uchaguzi ukikaribia. Sasa anasema hakuweza kutekeleza kwa sababu wananchi wanaoishi pale mombasa eti walikataa kuhama ile pesa ikapelekwa bara bara ile ya banana kuelekea kitunda. Sasa mwaka huu kaongeza kuweka X na kuwatisha watu kuwa hii bara bara itakuwa double road yenye kiwango cha Lami ambayo itaenda mpaka mbagala. Na sasa hivi siku za week end utawaona ma surveyor wamebeba ile midarubini yao wanainama inama wanapima pima kuhamasisha wananchi. Mimi nauliza hizo plan walizonazo hawa jamaa zipo kwenye mpango gani? wa halmashauri au wa serikali? au ni wahuni tu?
  na kama wahuni tufanyeje tusiwachague?
   
Loading...