Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
Ni vigumu sana kuamini maneno ya JPM kwa kuwa bila shaka anachoahidi huwa anasahau kutekeleza na hana "aibu" kusahau kutekeleza. Huyu ndiyo John 5!!
John Anataka Wafanyakazi wasubiri Stiglers gorge ikamilike ndipo mishahara itapanda, SGR, na Flyovers zikamilike ndipo nyongeza ya mishahara itaonekana kwenye akaunti za wafanyakazi! Ni John 5 huyu huyu aliyesema anafaya uhakiki, akafukuza watumishi zaidi 9000 aliowaita wana vyeti feki, na bila shaka alituaminisha kwamba atapandisha mshahara na madaraja baada ya mambo hayo. Na kwamba wazalishaji wakubwa wafanyakazi hawa maisha yao yataboreka! Huyu ni John 5, leo anasema kwanza msubiri tujenge reli na miradi ya umeme!! Tutasubiri sana kwa kuwa John 5 hakosi sababu kila ukicha!
John 5 anajaribu kutumia lugha rahisi rahisi tu kwamba kabla ya kipindi chake kukamilika atapandisha mshahara mnono, amesahau kwamba ni miaka miwili tu imebaki na kwamba miradi anayoitaja huenda hata haitakuwa imekamilika, John 5 anaongea sana, anasahau sana, hataki pia kuunganisha mipango yake ili iendane na kauli na ahadi zake! John hana washauri au ni mgumu kupokea ushauri? Anakosea!!
John 5 anasahau kwamba pesa zinazojenga miradi hii mikubwa ni pesa za mikopo!! Tena zinajenga miradi ambayo "return on investment yake ni ya muda mrefu" tena sio "quick income generating investments". Aidha, mikopo huiva kila mara na inahitaji kuwa "serviced". Ni yeye mwenyewe anayekiri kwamba Serikali inalipa mkopo wake zaidi ya Shilingi bilioni 900 kwa mwezi! John anakusanya kiasi gani kwa mwezi? Wafanyakazi anawalipa kiasi gani kwa mwezi? John 5 atatoa wapi pesa za kulipa na kuongeza mishahara kama focus yake ni kununua ndege ambazo nazo zimeripotiwa ndani ya kipindi kifupi tu kuleta hasara zaidi ya bilioni 200? Kujenga SGR? Kujenga mtambo wa umeme wa Stiglers Gorge? Kujenga Fly-overs? Kauli ya John 5 kwa wafanyakazi ni sawa na ya mzazi tu anayetaka kumtoroka mtoto mdogo nyumbani kwa kumuahidi atamletea pipi ambayo hata akirudi atamwambia tena "mwanangu au binti yangu nilisahau, nitakuletea kesho"
Aidha, kazi kubwa tunayo kwa vyama vya wafanyakazi ambavyo navyo vimeshindwa kusimama katika utetezi wa haki za wafanyakazi ambao ndiyo wazalishaji wakubwa katika taifa hili, Vyama hivi vimegeuka ni matawi ya serikali, vinaimba wimbo wa Serikali, John 5 akimaliza kuongea anaondoka akijipiga kifua, nimemaliza kazi!! Wao wanaufyataaaa!
Kwa hali ya serikali hii inayoimba wimbo wa mnyonge, huku ndani inadhamira ya kumnyonga kabisa mnyonge huyo tusitegemee jipya kutoka kwao, wameshindwa! Wanahitaji kusaidiwa! Jinsi hali inavyozidi kusonga mbele ndivyo wanavyodhihirisha kushindwa zaidi.
Kwa serikali yoyote inayoogopa kuhojiwa na kujitengenezea mabunduki kama sehemu ya kukwepa wajibu wake kuwatisha wakosoaji, tusitegemee muujiza! Katika serikali yenye nia njema na watu wake kwa mfano; viongozi wasingekuwa mbele kukanusha taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG), kuna wakubwa wengine wanasema kabisa anawakwamisha kwenye maendeleo!! Hivi kama tuna nia ya maendeleo ni kuchota tu fedha za umma bila verification na kuheshimu sheria za nchi? Katika msingi huo nani anakwamisha maendeleo ya taifa? CAG ni jicho linalokuonesha pale pana makosa, tunapaswa kwenda vile....wewe usiyejua kitu na una malengo yako unasema unatukwamisha! Tanzania yetu ni ya vituko kweli kweli!
Wafanyakazi wa sekta ya umma poleni sana. Mtaendelea kuugulia maumivu kwa sababu mnapenda kuisifia serikali kila mara mkiamini huo ndio uzalendo! Nawakumbusha teteeni nchi yenu na si serikali, huko ndiko kudumisha uzalendo. Panapokesana mgawanyo halisi kwenye fungu(keki) la nchi/umma linalosimamiwa na serikali kwa niaba yenu, mjue kuna tatizo, tena tatizo kubwa!
Mkiiacha serikali inakuja na kauli zake za nitaleta kesho, tusubiri kesho, narudia mtasubiri milele! Tuungane katika hili kwani ng'ombe hawezi toa maziwa pasi na kulishwa!!
Siwezi kumpa benefit of doubt(bod) JPM kwa kuwa mara nyingi ameahidi sana wafanyakazi tangu kwenye kampeni 2015 na hajaona aibu kutekeleza hata moja!! Tuendelee kumuamini?