Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,175
- 48,459
Sielewi ni kwa nini Lissu amekuwa akiwaita CCM "Ma-CCM" kwenye hotuba zake nyingi, lakini hata sasa sioni kama alikuwa anakosea kuwaita ivo.
Leo Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati ya siasa ya CCM Mkoa huo, Martine Shighela amesema serikali wanataka kuzuia watanzania kutapeliwa na watu wanaochangisha michango ya matibabu ya Lissu. Kwa maelezo ya Shighela hela zinazochangishwa haziendi kwenye matibabu ya Lissu bali zinatumika kuimarisha chama (CHADEMA?)
Job Ndugai Spika wa Bunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akizungumzia matibabu ya Lisu Nairobi alisema Bunge halitahusika na matibabu ya Lissu kwa kuwa ni CHADEMA na familia ya Lissu ndiyo waliamua kumpeleka Nairobi.
Lakini akijua yote hayo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, amesema kwamba serikali iko tayari kutoa hela ili Lisu akatibiwe kokote kule na kwenye hospitali yoyote ile duniani. Hivi Ummy wakati anatoa taarifa yake hiyo hakujua kwamba msimamo wa Bunge kuhusu matibabu ya Lissu ukoje?
Lakini inavoonekana CCM wamekerwa kutokana na kuona maelefu ya watanzania wanachangia matibabu ya Lissu bila ya kutetereka. Lengo lao la kwanza ni kuzuia uchangishaji huo kipropaganda lakini ikishindikana lazima litatoka "tamko la serikali" kuzuia kumchangia Lissu.
Inavoonekana CCM imebuni njia ya kuwachonganisha CHADEMA na wananchi baada ya kuona CHADEMA wamegoma kuwapigia magoti na wanyonge wa kweli wa nchi hii wamekataa kukatishwa tamaa na CCM na badala yake kila siku wanazidi kuchangia matibabu ya Lissu.
Lengo la kukusanya dolar 50,000 lililowekwa inavoonekana muda si mrefu litafikiwa na bila shaka wanaona watu wanavyochanga na wao wanafedheheka. Hawa waliokataza Lissu asifanyiwe maombi ndiyo leo wanajifanya wanataka kulipia matibabu popote na kwenye Hospitali yoyote ile duniani, KULIKONI?