Tuelimishane namna ya kununua simu mpya but a midrange

Tuelimishane namna ya kununua simu mpya but a midrange

Kyatile

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2017
Posts
1,736
Reaction score
1,582
Salaamu,

Nikiri kwamba kuna changamoto katika kujua simu gani bora ya kununua kwa ajili ya matumizi yako. Changamoto hizi zinatokana na sababu kadhaa, mfano;

1. Uwepo wa kampuni nyingi zinazotengeneza simu.

2. Uwepo wa matoleo mengi ya simu kutoka kampuni moja ndani ya mwaka mmoja. Mfano Samsung katika mwaka 2021 tu ametoa simu kwenye serries ya S -simu 4,
serries A - simu 12,
serries F - simu 6,
serries M - simu 9, nk. Hizi tu ni jumla ya simu 31. Xiaomi, One+, realme, Oppo, Huawei, LG, Motorola nk sijawataja.

3. Kutokuaminika kwa baadhi ya makampuni. Hapa namaanisha kuna kampuni zinavyo tangaza simu zao ni tofauti na jinsi simu hizo zilivyo.

4. Uwepo wa simu feki katika soko, nk.

Sasa mtu anapotaka simu kuna sifa anakuwa anazihitaji katika hiyo simu.

Mfano kwangu mimi vipaumbele vyangu katika simu ni uwepo wa kioo cha amoled kwa ajili ya uangavu, HD resolution, battery nzuri na camera nzuri.

Changamoto ambazo nimekutana nazo ni kwamba Samsung kwenye serries ya A ana A32 lakini bei yake ni kubwa ukilinganisha na Xiaomi katika specification hizo hizo. Sasa je nataka kujua hizi simu za Xiaomi Redmi serries zinakaa katika ubora wake kwa muda mrefu au zinapoteza ubora haraka? Labda issue kama quality ya camera, battery, mwonekano wa simu, speaker, nk. Nilitaka galaxy A22 lakini baadae nikaja kugundua kumbe haina HD resolution.

Naomba mnisadie kujua kama simuza Xiaomi zinakaa katika ubora kwa muda mrefu.
 
Natumia redmi 8A 4GB RAM, 64GB ROM, bei 250K AliExpress, ni mara mia mbili kuliko Samsung A20.

Usisahau gorilla glass 5 na 5000mah battery.

Jiongeze mwenyewe.
 
Natumia redmi 8A 4GB RAM, 64GB ROM, bei 250K AliExpress, ni mara mia mbili kuliko Samsung A20.
Usisahau gorilla glass 5 na 5000mah battery.
Jiongeze mwenyewe.
Hiyo A20 ni takataka ,, samasung A32 ndo nzuri
 
IMG_0210.png

Mkuu S 8 ulighaili?
 
Huwa mimi kwenye ununuzi wa simu kitu cha kwanza ninachoangalia ni soc, ukipatia hapa then ndio unaanza kuangalia mambo mengine.

Kwenye Upper midrange simu za laki 7 mpaka 1m hivi kwa Snapdragon angalia sd 778G ni soc kali sana, Huhitaji battery kubwa hata 4000mah inatosha simu itakaa na chaji sana, alternative kwa Mediatek ni Dimensity 920/900.

Kwa simu za laki 4 na kitu hadi laki 6 hivi ambayo nahisi ni Budget yako Tafuta Snapdragon 695 ni soc nzuri sana nayo, ila ina weakness kubwa hairecord 4k video, hii soc ni efficient sana simu zake zinakaa na Charge pia ina nguvu sana compare na competition at Same price. Alternative yake ni Mediatek Dimensity 810.

Kwa laki 3 mpaka 4 hapa kama unapata Snapdragon 680 ni vyema, Otherwise Mediatek G80/G85/G88 si mbaya. Pia zipo Unisoc T606/610/700 etc nazo ni alternative nzuri.

Kwa chini ya laki 2 nusu unisoc T310 ina make sense zaidi sema simu chache sana wanatumia, Most of time ni eneo la kukimbia hakuna simu nzuri kivile, hope Samsung A03 itakuwa eneo hili (sio A03s)

Ukishapata soc of your choice sana una narrow down Choice zako. Mfano una 1m, Sd 778G ipo karibia Brand zote Samsung Ana A52s na M52, Xioami ana Mi 11 lite 5g ne, Kuna realme GT master etc. Kutokana na matumizi ndio unachagua inayokidhi, kama unakaa field wiki kadhaa huna umeme battery life itakua priority, upo dukani picha unapiga sana Camera itakuwa priority etc.
 
Camera hapana, flagship ya miaka kadhaa iliopita ina camera kali kuliko midrange ya sasa
Sawa. Inaonekana Xiaomi anatoa simu yenye feature nzuri for value of money, Sasa je, simu zake hazi_misbehave baada ya muda wa matumizi labda baada ya mwaka? Mfano simu kuanza kuwa slow, kupoteza network, kupauka au kuanza yale mambo ya Tecno ya Unfortunately Launcher stopped!, Whatsap isn't responding n.k

Vipi AMOLED anayotumia Xiaomi ktk Redmi serries iko sharp kama vioo vya Samsung?
 
Kwanza Suala la xiaomi kuuza simu za bei ya Chini ni miaka hio ya zamani, Lineup zao za mwaka huu zote bei kubwa. Pengine simu nyingi mwaka huu zikawa bei kubwa.

Software Ya Xiaomi ni nzito ila ina feature nyingi inategemea wewe mwenyewe unapenda nini.

Simu za Nokia, Oppo, Vivo, Pixel, realme, Oneplus, Motorolla etc software zao ni nyepesi ila zinamiss feature nyingi.

Simu za Samsung, Xiaomi, LG etc software zao zina features za Kutosha ila sio smooth kama hizo huko juu.

Cha muhimu ili simu isiwe slow in long term tafuta yenye ram kubwa kadri utakavyoweza na storage za UFS inasaidia kufanya simu iwe responsive.

Kuhusu Display kuna Oled/Amoled na super Amoled, ukiona hilo neno Super Amoled ujue ni Oled ya Samsung hivyo quality itakuwa nzuri.

Ukiona imeandikwa tu Amoled pengine mwengine ametengeneza, na Hata Samsung anachakachua kuna simu zake vioo vyake hatengenezi mwenyewe ana outsource kampuni za Kichina kama Boe. Cha muhimu fanya Tafiti kioo husika kimetoka wapi kama sio Super Amoled.
 
Salaamu,

Nikiri kwamba kuna changamoto katika kujua simu gani bora ya kununua kwa ajili ya matumizi yako. Changamoto hizi zinatokana na sababu kadhaa, mfano;

1. Uwepo wa kampuni nyingi zinazotengeneza simu.

2. Uwepo wa matoleo mengi ya simu kutoka kampuni moja ndani ya mwaka mmoja. Mfano Samsung katika mwaka 2021 tu ametoa simu kwenye serries ya S -simu 4,
serries A - simu 12,
serries F - simu 6,
serries M - simu 9, nk. Hizi tu ni jumla ya simu 31. Xiaomi, One+, realme, Oppo, Huawei, LG, Motorola nk sijawataja.

3. Kutokuaminika kwa baadhi ya makampuni. Hapa namaanisha kuna kampuni zinavyo tangaza simu zao ni tofauti na jinsi simu hizo zilivyo.

4. Uwepo wa simu feki katika soko, nk.

Sasa mtu anapotaka simu kuna sifa anakuwa anazihitaji katika hiyo simu.

Mfano kwangu mimi vipaumbele vyangu katika simu ni uwepo wa kioo cha amoled kwa ajili ya uangavu, HD resolution, battery nzuri na camera nzuri.

Changamoto ambazo nimekutana nazo ni kwamba Samsung kwenye serries ya A ana A32 lakini bei yake ni kubwa ukilinganisha na Xiaomi katika specification hizo hizo. Sasa je nataka kujua hizi simu za Xiaomi Redmi serries zinakaa katika ubora wake kwa muda mrefu au zinapoteza ubora haraka? Labda issue kama quality ya camera, battery, mwonekano wa simu, speaker, nk. Nilitaka galaxy A22 lakini baadae nikaja kugundua kumbe haina HD resolution.

Naomba mnisadie kujua kama simuza Xiaomi zinakaa katika ubora kwa muda mrefu.
Naomba nikurekebishe, S series ya samsung inatoka moja tu kwa mwaka.

Hizo model nne umezitoa wapi?
 
Natumia Poco x3 pro mi games sijutii hii kitu.
 
Back
Top Bottom