phojamhone
Yesterday 14:46
#1
Member Array
Join Date : 18th May 2014
Posts : 24
Rep Power : 309
Likes Received3
Likes Given0
Mke wa ndoa akimjibu mumewe hivi baada ya kuulizwa kitu, inaashiria nini?
Ndugu zanguni wanajamvi, nakuja hapa kwa jambo lililomtokea rafiki yangu live, kwanza natanguliza salamu.
Rafiki yangu kamwoa mwanamke wa kabila tofauti na yeye, mke wake mara nyingi anapenda kwenda nyumbani kwao ambapo ni kwa mama yake mzazi na kwabahati mbaya baba yake alishafariki. Kimsingi ni mke wa ndoa, huyo mwanaume anatoka mkoa wa mbali na huyo mwanamke anatumia ukaribu wa nyumbani kwao kila kukitokea tofauti kidogo anakimbilia nyumbani kwa mama yake na saa nyingine anatabia ya kujaza ndugu zake nyumbani kwao na mme wake.
Juzijuzi kafiwa na ant yake, kaenda kulala msibani wilaya ya mbali na nyumbani kwao bila kumpa taarifa mme wake, huku akiwa amewaacha watoto wenye umri wa miaka 3 na 4.5 na housegirl wa miaka 12. Mume wake yupo safarini kilometer 900 kutoka kwenye huo mkoa ilipo familia. Baada ya kurudi msibani mume kamwuliza: Mbona ulienda kulala msibani bila kunitaarifu? isitoshe watoto ni wadogo uliwaacha na nani?
Mke akamjibu:"Ungetaka hayo ungeoa kabila lako! Kuolewa na wewe siyo kuvua asili yangu au kutoka kwenye familia yangu wala ukoo wangu tambua hilo"
Naomba mwongozo wenu, hii inaashiria nini kwa wale wanaooana makabila tofauti.