Tudai midalaho ya Wagombea, ni haki yetu

Tudai midalaho ya Wagombea, ni haki yetu

Mfikirishi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
10,465
Reaction score
12,204
Wakuu; Kuna nguvu katika midahalo. Tusipuuze!

Ni wazi kwamba kila tukijaribu kuwasikiliza wagombea mbali mbali ni rahisi sana kugundua kuwa wametusahahu sisi kama wananchi wamekuja na ya kwao.

Na mara zote ya kwao si ya kwetu. Vipaumbele vyao si vyetu. Ni wazi kuwa ya kwao ni kwa faida yao wenyewe na wapambe wao.

Bahati mbaya ni kuwa wa Tanzania wengi uelewa ni mdogo kiasi kwamba hawawezi kubaini ahadi zisizotekelezeka, ahadi za hadaa na ahadi za kupotezeana muda jua lizame kesho ije.

Bahati nyingine mbaya ni kuwa wengi hawajui ipi ni ahadi na ipi ni haki na afanye nini asipoipata

Kwa muktadha huo imefikia hatua kampeni zimekuwa mithili ya sehemu za ibada. Hakuna kuhoji chochote. Kampeni zimekuwa kama vijiwe vya "praise and worship teams" ambao hata chochote atakachofanya mgombea yaani hata akikohoa kwenye microphone bado watampigia makofi, shangwe na vigelegele.

Yaani unahudhuria hicho kinachoitwa mkutano wa kampeni alafu wote waliopo pale wamevaa mavazi radmi ya chama na pengine wameletwa pale kwa juhudi za chama (kwenda kuongeza halaiki)

Hii si sahahi hata kidogo. Na bado mgombea atashupaza mishipa ya shingo na kukausha mate mdomoni akiwahutubia kijanja janja tu ilimradi muda uishe. Wengine tumeshuhudia kampeni zao zimekuwa sehemu ya burudani (fiesta/bonanza) badala ya sehemu ya kutumia muda mwingi kuwatoa wananchi "matongotongo' ili wajue walikotoka, walipo na wanapotakiwa kwenda.

In short kampeni zimekuwa ni rubber-stamp ya kudumaza nchi na wananchi wake. Kampeni zimekuwa ni sehemu za kueneza chuki, kejeli na ubaguzi. Zaidi ya yote kampeni zimekuwa ni sehemu ya kutakatisha fedha chafu, ufisadi na uhujumu uchumi. Nisiandike mengi japo kuna mengi.

Pendekezo:
Maadamu wagombea wengi wanajibizana majukwaani. Ni vizuri sasa ifike mahali tuone umuhimu wa kulazimisha midahalo hasa kwa nafasi nyeti Kama Urais. Tuwatoe wagombea wote kwenye comfort zones zao ambako wanaongea ongea tuu bila kujali usahihi wa wakisemacho waje kwenye planned sessions ambako kunahitajika busara, uwazi, usahihi, weledi na uzoefu.

Binafsi kuna ahadi naendelea kuzisikia japo zilikuwepo toka enzi za Hayati Baba wa Taifa. Na zikiwashinda kutekeleza wanaolaumiwa ni wananchi wale wale walopewa ahadi hizo.

Wasomi lisaidieni hili Taifa. Hakusomeshwa ili mtafute pesa peke yake. Mlisomeshwa ili muwe na uwezo wa kuiandalia jamii mazingira mazuri ya kuishi leo na kesho. Mlisomeshwa ili kuleta mabadiliko na kuiendeleza nchi yetu.

Tusiwaache wagombea watupande vichwani kama watakavyo. Kwamba wakisemacho wagombea ndicho hicho hicho hata kama ni fyongo.
 
Back
Top Bottom