Kauli hii ya TUCTA ndiyo niliyokuwa naisubiri wamwache tu aendelee kujikaanga mwenyewe kwa vile najua hatakuwa na majibu ya kuwaridhisha wafanyakazi, watakuwa wanamchekea tu kila apitapo. Watu wanadhani watanzania ni wajinga lakini si kiasi hicho, na mjinga akishaelimika humzidi hata mwalimu wake.Akizugumza na gazeti hili leo asubuhi Katibu wa shirikisho hilo Nicholaus Mgaya amesema kuwa hivi sasa hawatatoa maoni yoyote zaidi ya kumwacha aendelee na kampeni zake.
Heri wajikalie kimya maana vinginevyo, watakwenda mezani wakiwa na Plaster kichwani.
Hivi hili la Plaster na lenyewe kasingiziwa?
Hata hivyo alisema serikali isingeweza kuwadanganya wafanyakazi kuwa kiwango walichokuwa wakikihitaji cha Sh.315,000 kuwa hakiwezekani lakini serikali itaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kulingana na uwezo wa bajeti yake.
Plasta midomoni na plasta kichwani mimi naona ni kitu kimoja maana virungu vya FFU huwa havina macho, bora Mgaya ujinyamazie aliyelianzisha atalinywa mwenyewe.Kama haya maneno yamechapwa vyema Mkuu alisema hivi kuhusu plasta:
"Sasa hata hatujazungumza wameanza kutangaza mgomo, sasa afadhali tuzungumze kwanza maana mgomo una kasheshe zake, mkigoma hamtaachwa, askari watawapiga virungu na hata wengine kuweza kupoteza maisha, mimi naweza kuwa rahim lakini polisi mkiwafanyia fujo watawatwanga na hata mkigoma baadaye mtarudi kwenye mazungumzo mkiwa na plasta midomoni"
Nimekuwa najiuliza alimaanisha wakirudi watakuwa wamenyamazishwa au?
Don argue with a fool...Hongera Mgaya. Don' argue with a f.........l
TUCTA lakebehi kauli ya JK
Monday, 23 August 2010 11:48
Na Job Ndomba,Jijini wa Dar Leo
SHIRIKISHO la Vyama Vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) limesema kwamba kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa ni matusi kudai kuwa hajali wafanyakazi shirikisho hilo limeibuka na kudai kuwa hizo ni kampeni.
Akizugumza na gazeti hili leo asubuhi Katibu wa shirikisho hilo Nicholaus Mgaya amesema kuwa hivi sasa hawatatoa maoni yoyote zaidi ya kumwacha aendelee na kampeni zake.
"Siwezi kutoa maoni yoyote kuhusiana na kauli za kampeni alizozitoa Rais Kikwete na kwamba tumuache aendelee na kampeni zake nasi tunasubiri kupiga kura Oktoba 31, mwaka huu, " amesema katibu huyo.
Jana Rais Kikwete alisema kuwa ni matusi kuambiwa kuwa hajali maslahi ya wafanyakazi nchini wakati serikali yake imekuwa ikiboresha maslahi yao mwaka hadi mwaka.
Pia alisisitiza kwamba ataendelea kuwaheshimu wafanyakazi na serikali yake itaendelea kuboresha stahili zake na kuahidi kuboresha zaidi katika kipindi cha miaka mitano.
Sanjari na hayo Rais Kikwete alisema anataka kuweka rekodi ya kukumbukwa kwa mema yake katika uongozi wake na si vinginevyo.
Aidha akiendelea kuwaomba kura wananchi wa Jiji la Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba alisema hatendewi haki kuhusiana na maslahi ya wafanyakazi tangu alipoingia madarakani mwaka 2005 na Serikali yake ilikuwa ikifanya hivyo kulingana na nafasi.
Hata hivyo alisema serikali isingeweza kuwadanganya wafanyakazi kuwa kiwango walichokuwa wakikihitaji cha Sh.315,000 kuwa hakiwezekani lakini serikali itaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kulingana na uwezo wa bajeti yake.
To me this is a professional answer, aliposema 'siwezi kutoa maoni....tunasubiri Oct.31' unaweza fikiri hajatoa ujumbe kwa wafanyakazi kumbe ni ujumbe uliojitoshereza."Siwezi kutoa maoni yoyote kuhusiana na kauli za kampeni alizozitoa Rais Kikwete na kwamba tumuache aendelee na kampeni zake nasi tunasubiri kupiga kura Oktoba 31, mwaka huu, " amesema katibu huyo.