TUCTA kujadili kima cha chini cha mshahara 2019

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,421
BARAZA Kuu la Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (Tucta) linatarajia kukutana Aprili 2, 2019 ambapo pamoja na mambo mengine, litajadili mapendekezo ya kima cha chini cha mishahara.

Akizungumza na gazeti hili Jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya alisema kuwa, baraza hilo pia litajadili maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mbeya ambapo Rais, Dk. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Alisema kwa sasa Kamati maalumu ya kushughulikia mishahara iliweza kufanya utafiti kuhusiana na hali halisi ya maisha kwa sasa, kima cha chini cha mishahara wanaopata wafanyakazi, gharama za pango na matumizi mengine ili waweze kuleta mapendekezo yao.

“Kuna kamati maalumu ya mishahara ambayo ipo kwa mujibu wa katiba yetu, inafanya kazi ya kuangalia hali halisi ya maisha ya wafanyakazi kwa sasa, kima cha chini cha mshahara wanaopata, gharama za pango na nauli na matumizi mengine wanayokumbana nayo, wanatarajia kuwasilisha mapendekezo yao kwenye kikao cha Baraza Kuu kinachotarajiwa kufanyika Aprili 2 mwaka huu,” alisema Nyamhokya.

Aliongeza, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo, wataweza kuangalia kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa sekta zote binafsi na serikali ili waweze kuwasilisha mapendekezo yao kwa Rais Magufuli siku ya wafanyakazi.

Alisema, mpaka sasa, wafanyakazi wanapata kiasi kidogo cha mishahara ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya kila siku ukilinganisha na kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema licha ya kuwasilisha mapendekezo ya kuiomba serikali kuongeza kima cha chini cha mshahara ili uweze kufikia 750,000 kwa wafanyakazi wa serikali, lakini mpaka sasa bado wanapokea Sh 375,000.

“Wafanyakazi wa serikali wanapata kima cha chini cha mshahara kuanzia Sh 375,000 na kuendelea, huku sekta binafsi wakipata kuanzia Sh 100,000 kwa mwezi kulingana na ofisi anayofanyia kazi,” alisema.

Aliongeza, kiasi hicho ni kidogo na kwamba hakiwezi kukidhi gharama za maisha, jambo ambalo limechangia kujitokeza kwa malalamiko ya kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema, lakini pia wameiomba serikali kupunguza gharama za kodi inayokatwa kwenye mishahara yao ambayo imekua kero ya muda mrefu, jambo ambalo litasaidia kumpunguzia mzigo mfanyakazi kutokana na hali ngumu ya maisha.

http://mtanzania.co.tz/tucta-kujadili-kima-cha-chini-cha-mshahara/amp/
 
Suala la kulinganisha Mishahara kwa watu wenye sifa zinazofanana ila wanao fanya Kazi katika Idara tofauti tofauti za Serikali;
Kwa mtazamo wangu;

  • Hiyo italeta tija kama watatazama pia mfumo wa kutoa Posho kwenye idara za Serikali. Nimesema hivyo nikimaanisha zipo Taasisi ambazo mfumo wa kupewa posho unawafikia/unawapendelea zaidi kuliko wafanyakazi wengine wa level moja. Hii hufanya wengine kupelekea kujipatia ZIADA ya kwenye 25% hadi 150% ya mshahara wa kila mwezi.
  • Aina ya kazi; wapo wafanyakazi wenye fursa na muda wa kufanya na kusimamia miradi yao binafsi kulingana na nature ya kazi yao; mfano: Idara ya kilimo, Engineer wa Ujenzi nk ukilinganisha na mkufunzi wa Idara ya kilimo/Engineer.
  • Naamini kazi zote zinahitaji dedication, ila idara kama ya taaluma inamfumo mzuri wa kufuatiliwa na pia kule ndiko wanako toka wafanyakazi bora na waliopikwa vizuri hivyo nafikiri hii sector isihusishwe na hili suala badala yake Iboreshewe zaidi. Kwa hili la Elimu nafikiri tuwe makini tusije kuharibu Msingi wa nyumba, tukaishia kujivunia kuwa tumepaua kwa bati la msouth?
  • Angalizo: mimi sio Mwalimu wala sifanyi kazi idara ya Elimu!
 
BARAZA Kuu la Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (Tucta) linatarajia kukutana Aprili 2, 2019 ambapo pamoja na mambo mengine, litajadili mapendekezo ya kima cha chini cha mishahara.

Akizungumza na gazeti hili Jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya alisema kuwa, baraza hilo pia litajadili maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mbeya ambapo Rais, Dk. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Alisema kwa sasa Kamati maalumu ya kushughulikia mishahara iliweza kufanya utafiti kuhusiana na hali halisi ya maisha kwa sasa, kima cha chini cha mishahara wanaopata wafanyakazi, gharama za pango na matumizi mengine ili waweze kuleta mapendekezo yao.

“Kuna kamati maalumu ya mishahara ambayo ipo kwa mujibu wa katiba yetu, inafanya kazi ya kuangalia hali halisi ya maisha ya wafanyakazi kwa sasa, kima cha chini cha mshahara wanaopata, gharama za pango na nauli na matumizi mengine wanayokumbana nayo, wanatarajia kuwasilisha mapendekezo yao kwenye kikao cha Baraza Kuu kinachotarajiwa kufanyika Aprili 2 mwaka huu,” alisema Nyamhokya.

Aliongeza, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo, wataweza kuangalia kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa sekta zote binafsi na serikali ili waweze kuwasilisha mapendekezo yao kwa Rais Magufuli siku ya wafanyakazi.

Alisema, mpaka sasa, wafanyakazi wanapata kiasi kidogo cha mishahara ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya kila siku ukilinganisha na kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema licha ya kuwasilisha mapendekezo ya kuiomba serikali kuongeza kima cha chini cha mshahara ili uweze kufikia 750,000 kwa wafanyakazi wa serikali, lakini mpaka sasa bado wanapokea Sh 375,000.

“Wafanyakazi wa serikali wanapata kima cha chini cha mshahara kuanzia Sh 375,000 na kuendelea, huku sekta binafsi wakipata kuanzia Sh 100,000 kwa mwezi kulingana na ofisi anayofanyia kazi,” alisema.

Aliongeza, kiasi hicho ni kidogo na kwamba hakiwezi kukidhi gharama za maisha, jambo ambalo limechangia kujitokeza kwa malalamiko ya kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema, lakini pia wameiomba serikali kupunguza gharama za kodi inayokatwa kwenye mishahara yao ambayo imekua kero ya muda mrefu, jambo ambalo litasaidia kumpunguzia mzigo mfanyakazi kutokana na hali ngumu ya maisha.

http://mtanzania.co.tz/tucta-kujadili-kima-cha-chini-cha-mshahara/amp/
Hamna kitu hapo!! miaka minne kimya, eti tarehe 2 April ndio wanakutana!!! haya justification ya ada zao tu
 
Mie wakati naoa Mke wa pili 1994 nilizungumza nae Pembeni nikamwambia uwezo wangu wa kulipa Mahari Ni kiasi gani

Alichofanya kilipoitishwa kikao Cha Familia Yao kupendekeza Mahari aliwasilisha kiwango ambacho Mie naweza kulipa Kama ndio proposal yake

Iliporudi kwangu nami nikakubali Bila ya kusita Familia Yao ikaona imepata Mkwe Kweli Kweli maana siku burgain Mahari waliyopendekeza bali nililipia yote kwa mkupuo mmoja

Vilaza watasema nimetoka Nje ya Mada kwa Kuwa mjadala Ni nyongeza ya Mshahara Mie nazungumzia Posa
 
nadhani serikali ya JPM imewapa go ahead, sote tunajua TUCTA iko mfukoni mwa serikali na hayo wanayofanya ni maigizo tu, kama kima cha chini kitapanda ni kwasababu serikali imeamua na sio mapendekezo ya TUCTA.
 
Kwani mwenyekiti wa tume ya Waziri Mkuu ya kuboresha mishahara anasemaje?

Point hapo ni kuwa na scale za mishahara inayofanana no matter what. Kama Engineer II basi atalipwa sawa na Wahandisi wenzake wote wa Daraja II awe Halmashauri/Wizarani/Tanesco/Tarura/Tanroads/ N.K
 
Wataibuka na kiwango cha mshahara mnono ambacho wanajua kabisa jiwe hawezi kukubali kukitoa,na tarehe 1 siku ya wafanyakazi duniani wataumiza migongo yao na mikono yao kwa kubeba mabango makubwa yenye ujumbe wa kumsifia jiwe, mwisho wa yote wanaishia kujibiwa kuwa siwezi kuacha kufanya kazi za maendeleo nikawapandishia mshahara.
 
hakuna kitu kibaya katika maisha ya sasa kama kumdanganya mfanyakazi wa umma.TUCTA nyie pamoja na viongozi wenu mmekaa kimya 4years bila kuwa na proper reasoning na justification ya kwenda kwa mheshimiwa Rais ili aweze kuwapandisha madaraja wafanyakazi wake achana na ile general increament mie nazungumzia promotions tuu hapa ambapo kwa hesabu za fasta fasta nadhani haizidi hata 2 bilion lakini mmekuwa ni watu wa kubwabwaja tuu maneno hapa na kuwadanganya wananzengo.wallah TUCTA mtakufa kifo cha mende nyie mwaka 2020
 
Wao wakae tu watumbue pesa wanayokusanya kila mwezi 2% ya wafanyakazi lakini eti kuna mapendekezo kwa serikali hakuna la maana hapo, miaka 3 mko kimya mmekosa strategy ya kushinikiza watumishi waongezewe mishahara mnaleta porojo tupu hapa
 
BARAZA Kuu la Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (Tucta) linatarajia kukutana Aprili 2, 2019 ambapo pamoja na mambo mengine, litajadili mapendekezo ya kima cha chini cha mishahara.

Akizungumza na gazeti hili Jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya alisema kuwa, baraza hilo pia litajadili maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mbeya ambapo Rais, Dk. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Alisema kwa sasa Kamati maalumu ya kushughulikia mishahara iliweza kufanya utafiti kuhusiana na hali halisi ya maisha kwa sasa, kima cha chini cha mishahara wanaopata wafanyakazi, gharama za pango na matumizi mengine ili waweze kuleta mapendekezo yao.

“Kuna kamati maalumu ya mishahara ambayo ipo kwa mujibu wa katiba yetu, inafanya kazi ya kuangalia hali halisi ya maisha ya wafanyakazi kwa sasa, kima cha chini cha mshahara wanaopata, gharama za pango na nauli na matumizi mengine wanayokumbana nayo, wanatarajia kuwasilisha mapendekezo yao kwenye kikao cha Baraza Kuu kinachotarajiwa kufanyika Aprili 2 mwaka huu,” alisema Nyamhokya.

Aliongeza, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo, wataweza kuangalia kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa sekta zote binafsi na serikali ili waweze kuwasilisha mapendekezo yao kwa Rais Magufuli siku ya wafanyakazi.

Alisema, mpaka sasa, wafanyakazi wanapata kiasi kidogo cha mishahara ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya kila siku ukilinganisha na kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema licha ya kuwasilisha mapendekezo ya kuiomba serikali kuongeza kima cha chini cha mshahara ili uweze kufikia 750,000 kwa wafanyakazi wa serikali, lakini mpaka sasa bado wanapokea Sh 375,000.

“Wafanyakazi wa serikali wanapata kima cha chini cha mshahara kuanzia Sh 375,000 na kuendelea, huku sekta binafsi wakipata kuanzia Sh 100,000 kwa mwezi kulingana na ofisi anayofanyia kazi,” alisema.

Aliongeza, kiasi hicho ni kidogo na kwamba hakiwezi kukidhi gharama za maisha, jambo ambalo limechangia kujitokeza kwa malalamiko ya kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema, lakini pia wameiomba serikali kupunguza gharama za kodi inayokatwa kwenye mishahara yao ambayo imekua kero ya muda mrefu, jambo ambalo litasaidia kumpunguzia mzigo mfanyakazi kutokana na hali ngumu ya maisha.

http://mtanzania.co.tz/tucta-kujadili-kima-cha-chini-cha-mshahara/amp/
Hapo wanaota mchana kweupee itakuwa kama ile iliyopita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uhusiano wa TUCTA na wafanyakazi haupo kabisa ni maigizo tu, wanakula michango ya wanachama bila usaidizi wowote! watambue kuwa kama ingekuwa hiari hakuna mfanyakazi angekubali kuwa mwanachama wa hivi vyama.
Pia wapo mfukoni mwa serikali hivyo hawana utetezi wowote kwa wafanyakazi.
Wastaafu nao hawalipwi mafao yao na wao TUCTA wapo kimya huku wastaafu hao wakitaabika mtaani.
 
Mie wakati naoa Mke wa pili 1994 nilizungumza nae Pembeni nikamwambia uwezo wangu wa kulipa Mahari Ni kiasi gani

Alichofanya kilipoitishwa kikao Cha Familia Yao kupendekeza Mahari aliwasilisha kiwango ambacho Mie naweza kulipa Kama ndio proposal yake

Iliporudi kwangu nami nikakubali Bila ya kusita Familia Yao ikaona imepata Mkwe Kweli Kweli maana siku burgain Mahari waliyopendekeza bali nililipia yote kwa mkupuo mmoja

Vilaza watasema nimetoka Nje ya Mada kwa Kuwa mjadala Ni nyongeza ya Mshahara Mie nazungumzia Posa
nimekuelewa . hawa walishamalizana na mkuu mapema kabisa .hapo wanaenda kujadili mabango, na tshirt za kuvaa siku ya tukio
 
Back
Top Bottom