Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 873
TUCTA: JK amechelewa
• Yadai amechelewa kutamka nyongeza ya mishahara
na Christopher Nyenyembe
KAIMU Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama ya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicholaus Mgaya, amesema Rais Jakaya Kikwete amechelewa kutangaza kupandisha mishahara ya wafanyakazi.
Alisema kuwa TUCTA wataendelea na msimamo wao wa kutompa kura mgombea yeyote wa kiti cha urais asiyejali masilahi yao au yule aliyezikataa kura zao.
Akizungumza na Tanzania Daima, Mgaya alisema Rais Kikwete, alipaswa kuwaomba radhi wafanyakazi baada ya kuwaambia kuwa hata wakigoma kwa miaka minane serikali haitaweza kuongeza mishahara.
Alisema kuwa Agosti 21 wakati akizindua kampeni za kitaifa za CCM, Rais Kikwete alitangaza kuwa mishahara imepanda, ingawa si kwa kiwango kilichokuwa kikitakiwa na TUCTA.
Mgaya alisema Rais Kikwete alipaswa kukutana na TUCTA na kuwaomba radhi kwa matamshi ya vitisho na ya kusikitisha aliyoyatoa Mei 4, mwaka huu.
Alibainisha kuwa ameshangazwa na kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa juzi mkoani Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kuwa hakuzikataa kura za wafanyakazi.
Mgaya alisema kuwa kauli hiyo ya kukana kile alichokisema awali kuwa hazitaki kura za wafanyakazi, hawawezi kubadilishwa kwa kuwa amechelewa, alitakiwa kwanza aombe msamaha kama kauli hiyo aliitoa kwa bahati mbaya, pia alipaswa kuwa muungwana kwa kuomba radhi.
"Mimi inanitia wasiwasi sana sioni kama ana maana gani au anataka kutubadilisha, naona amekwisha kupata alichokuwa anakitaka, sasa anatumia njia ya kujikosha ili aonekane kuwa hakusema, ulimwengu mzima unajua kuwa alisema, hapo hatutabadilika, nasisitiza amechelewa," alisema Mgaya.
Alibainisha kuwa wafanyakazi walipanga kufanya mgomo wa nchi nzima Mei 5, mwaka huu kuishinikiza serikali iongeze kima cha chini na kufikia sh 315,000 lakini serikali iligoma.
"Rais Kikwete amechelewa, lazima serikali itambue kuwa tutaendelea kupigania haki za wafanyakazi mpaka matatizo yetu yatakapotatuliwa.
"Msimamo wetu uko pale pale kuwa hatutampatia kura mgombea asiyezihitaji," alisema Mgaya.
Alibainisha kuwa Rais Kikwete alipaswa kukutana na wafanyakazi kuwaeleza ongezeko hilo la mishahara kabla ya kuitangaza kwenye majukwaa ya kisiasa.
Alisema wafanyakazi wana kiu kubwa ya kusikia Rais Kikwete akifuta kauli yake ya awali ambayo ililenga kuwatisha wafanyakazi ili wasiendelee kudai haki zao.
"Haya mambo ni magumu, nilikuwa safarini nimepigiwa simu kuwa alipokuwa akihutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM pale Jangwani, alizungumzia masuala ya TUCTA na mishahara, lakini kabla hajamaliza ndipo nilipoambiwa kuwa ameanguka jukwaani," alisema.
Alibainisha kuwa alishtushwa na tukio hili ambalo linapaswa lichukuliwe kwa uzito mkubwa, hasa kwa watu wanaoratibu shughuli za rais.
"Kwa matibabu ya kiongozi huyo mkuu wa nchi, anaangaliwa na watu… uchunguzi wa afya yake nchi za nje unafanyika kutokana na kodi za wafanyakazi," alisema.
Aliongeza kuwa TUCTA ilikuwa inapendekeza viwango vizuri ili kukidhi pia afya za wafanyakazi wote.
Alisema afya ya rais inawatia wasiwasi viongozi wa TUCTA, na wanaona kuna siri kubwa iliyofichika kuhusu afya yake.
"Haiwezekani kila wakati tuambiwe kuwa rais anaanguka wakati kodi za wafanyakazi ndizo zinazotumika kumfanyia uchunguzi nchi za nje," alisema.
Aliongeza kuwa ni vema Watanzania wakaambiwa rais anaumwa nini.
Katika hatua nyingine, Mgaya alisema kuwa kuongezwa kwa kima cha chini hadi kufikia sh 235,000 ni dalili nzuri ya kuelekea kwenye viwango vinavyotakiwa. Mei 4, mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Rais Kikwete alisema kuwa serikali haina uwezo wa kuwaongeza wafanyakazi kima cha chini kuwa sh 315,000
Rais Kikwete alisema hawezi kuwadanganya wafanyakazi kuwa atawaongeza mishahara wanayotaka na yupo tayari kuzikosa kura 350,000 za wafanyakazi. Alisema kama serikali ingewatimizia hitaji hilo wafanyakazi hao, basi ingelazimika kwenda kukopa fedha na maisha ya Watanzania walio wengi yangekuwa kwenye matatizo.
Habari ndio hiyo..