TUCTA: JK amechelewa kutamka nyongeza ya mishahara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TUCTA: JK amechelewa kutamka nyongeza ya mishahara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, Aug 24, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Aug 24, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  TUCTA: JK amechelewa

  • Yadai amechelewa kutamka nyongeza ya mishahara


  na Christopher Nyenyembe

  KAIMU Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama ya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicholaus Mgaya, amesema Rais Jakaya Kikwete amechelewa kutangaza kupandisha mishahara ya wafanyakazi.

  Alisema kuwa TUCTA wataendelea na msimamo wao wa kutompa kura mgombea yeyote wa kiti cha urais asiyejali masilahi yao au yule aliyezikataa kura zao.

  Akizungumza na Tanzania Daima, Mgaya alisema Rais Kikwete, alipaswa kuwaomba radhi wafanyakazi baada ya kuwaambia kuwa hata wakigoma kwa miaka minane serikali haitaweza kuongeza mishahara.

  Alisema kuwa Agosti 21 wakati akizindua kampeni za kitaifa za CCM, Rais Kikwete alitangaza kuwa mishahara imepanda, ingawa si kwa kiwango kilichokuwa kikitakiwa na TUCTA.

  Mgaya alisema Rais Kikwete alipaswa kukutana na TUCTA na kuwaomba radhi kwa matamshi ya vitisho na ya kusikitisha aliyoyatoa Mei 4, mwaka huu.

  Alibainisha kuwa ameshangazwa na kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa juzi mkoani Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kuwa hakuzikataa kura za wafanyakazi.

  Mgaya alisema kuwa kauli hiyo ya kukana kile alichokisema awali kuwa hazitaki kura za wafanyakazi, hawawezi kubadilishwa kwa kuwa amechelewa, alitakiwa kwanza aombe msamaha kama kauli hiyo aliitoa kwa bahati mbaya, pia alipaswa kuwa muungwana kwa kuomba radhi.

  "Mimi inanitia wasiwasi sana sioni kama ana maana gani au anataka kutubadilisha, naona amekwisha kupata alichokuwa anakitaka, sasa anatumia njia ya kujikosha ili aonekane kuwa hakusema, ulimwengu mzima unajua kuwa alisema, hapo hatutabadilika, nasisitiza amechelewa," alisema Mgaya.

  Alibainisha kuwa wafanyakazi walipanga kufanya mgomo wa nchi nzima Mei 5, mwaka huu kuishinikiza serikali iongeze kima cha chini na kufikia sh 315,000 lakini serikali iligoma.
  "Rais Kikwete amechelewa, lazima serikali itambue kuwa tutaendelea kupigania haki za wafanyakazi mpaka matatizo yetu yatakapotatuliwa.

  "Msimamo wetu uko pale pale kuwa hatutampatia kura mgombea asiyezihitaji," alisema Mgaya.
  Alibainisha kuwa Rais Kikwete alipaswa kukutana na wafanyakazi kuwaeleza ongezeko hilo la mishahara kabla ya kuitangaza kwenye majukwaa ya kisiasa.

  Alisema wafanyakazi wana kiu kubwa ya kusikia Rais Kikwete akifuta kauli yake ya awali ambayo ililenga kuwatisha wafanyakazi ili wasiendelee kudai haki zao.

  "Haya mambo ni magumu, nilikuwa safarini nimepigiwa simu kuwa alipokuwa akihutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM pale Jangwani, alizungumzia masuala ya TUCTA na mishahara, lakini kabla hajamaliza ndipo nilipoambiwa kuwa ameanguka jukwaani," alisema.

  Alibainisha kuwa alishtushwa na tukio hili ambalo linapaswa lichukuliwe kwa uzito mkubwa, hasa kwa watu wanaoratibu shughuli za rais.

  "Kwa matibabu ya kiongozi huyo mkuu wa nchi, anaangaliwa na watu… uchunguzi wa afya yake nchi za nje unafanyika kutokana na kodi za wafanyakazi," alisema.

  Aliongeza kuwa TUCTA ilikuwa inapendekeza viwango vizuri ili kukidhi pia afya za wafanyakazi wote.
  Alisema afya ya rais inawatia wasiwasi viongozi wa TUCTA, na wanaona kuna siri kubwa iliyofichika kuhusu afya yake.

  "Haiwezekani kila wakati tuambiwe kuwa rais anaanguka wakati kodi za wafanyakazi ndizo zinazotumika kumfanyia uchunguzi nchi za nje," alisema.

  Aliongeza kuwa ni vema Watanzania wakaambiwa rais anaumwa nini.

  Katika hatua nyingine, Mgaya alisema kuwa kuongezwa kwa kima cha chini hadi kufikia sh 235,000 ni dalili nzuri ya kuelekea kwenye viwango vinavyotakiwa. Mei 4, mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Rais Kikwete alisema kuwa serikali haina uwezo wa kuwaongeza wafanyakazi kima cha chini kuwa sh 315,000

  Rais Kikwete alisema hawezi kuwadanganya wafanyakazi kuwa atawaongeza mishahara wanayotaka na yupo tayari kuzikosa kura 350,000 za wafanyakazi. Alisema kama serikali ingewatimizia hitaji hilo wafanyakazi hao, basi ingelazimika kwenda kukopa fedha na maisha ya Watanzania walio wengi yangekuwa kwenye matatizo.  Habari ndio hiyo..
   
 2. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kima cha chini kilichotangazwa na Kikwete ni Tshs 135,000/= tu na sio 235,000/=

  Mgaya pamoja na TUCTA shikilieni pale pale ili tabia ya rais kuropoka ropoka ovyo ovyo ikome. Ukweli kura za wafanyakazi hazihitaji. Anahitaji kukaangwa kwa mafuta yake.

   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kuchelewa kutamka sio tatizo la msingi la wafanyakazi kwa sasa kama wanavyodai TUCTA, jambo la msingi ni kiasi gani kimeongezwa ndio msingi wa majadiliano.
   
 4. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,605
  Likes Received: 4,707
  Trophy Points: 280
  Mbayuwayu msumari umeukalia huo lazima ukuchome,tabia ya kuropoka uiache, mananeno utamke mwenyewe halafu unayakana, au ndiyo athari za ugonjwa wako wa kuanguka ,maana ukizinduka baada ya kuanguka hukumbuki uliongea nini.
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  katika bajeti ya mwaka huu Kima cha chini kiliongezwa hadi 135,000 lakini baada ya majadiliano kuendelea kimeongezwa tena hadi 260,000/- ingawa TUCTA walitaka kiwe 350,000/=
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hivi kweli mtashangaa mkisikia zaidi ya nusu ya wafanyakazi wamempigia kura kikwete?

  ujumbe wa tucta wenyewe unaweza hata usiwafikie wafanyakazi wote.
   
 7. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  The Workers of Tanzania have found their voice. Suddenly, JK and his minions like Kapuya and others are absolutely concerned about what TUCTA has to say. Well, it's too little and too late!

  mtu anayekuona mtu wakati anataka kura yako tu sio mtu! Send them packing!
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  ndugu, matatizo ya kiafya hayana mwenyewe hasa kama na wewe ni binadamu. jaribu kadri uwezavyo kupingana na sera za JK lakini ugonjwa wake mwachie mwenyezi Mungu mwenyewe. Leo ni Kikwete na kesho waweza kuwa wewe au mimi kwa mapenzi yake Mungu. kwetu kuna msemo unasema, ugonjwa ni sehemu ya uumbaji wake mungu usithubutu kuutolea kejeri.
   
 9. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Anaijutia hiyo kauli...
   
 10. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kama baba anatunzwa na watoto wake, anatibiwa kwa pesa za watoto wake na kila kitu ni juu ya watoto wake. "Je ni kweli kuwa matatizo ya kiafya ya baba hayana mwenyewe? Nilifikiri matatizo ya kiafya ya baba yanawahusu watoto moja kwa moja?

  Respect
   
 11. D

  Dick JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maneno ni mengi kuliko vitendo.
   
 12. m

  mramba Member

  #12
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 23, 2009
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapohapo MGAYA shikilia uzi huohuo. Na naomba na wafanyakazi wote na familia zetu tumuunge Mgaya mkono. Huyu rais haelewi anachozungumza hata kidogo. Na kwa taarifa yenu akiingia ikulu kwa sababu ni muhula wake wa mwisho wafanyakazi sahauni kupanda kwa mishahara tena. Patafidiwa mpaka hilo ongezeko la sasa. CCM haitazami watu wake wanaishije ni mpaka waone ama watu wamekufa kwa mgomo wa madaktari au wakati wanataka kura zetu. Wakati mwingine wakila na kunywa kodi zetu aah! hatuonekani watanzani walala hoi.
  Kama yeye ni muungwana basi na awatake radhi hao wafanyakazi aliokataaa kura zao pamoja na kuwatishia.
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mgomo wenyewe uko wapi basi! TUCTA hakuna kitu.
   
 14. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mgaya mbona kakomaa sana! Si atangaze tu kuwa naye ni mwanasiasa! Kina Ngula wako wapi? TUCTA na vyama vilivyo chini yake wote ni corrupt tu, mara ngapoi tumesikia kuna ufisadi TUCTA, Chama cha Walimu nk, TUCTA acheni danganya toto, nyie wote , CHADEMA, CCM, TUCTA, RAAWU, CHODAWU, nk ni kitu kile kile tu, sana sana mtu ukizidi usumbufu unavutwa juu km Magreth Sitta. Kila mtu na abaki na utashi wake, heri hata JK alivyoelekeza kwa mfano wa mbayuwayu
   
 15. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #15
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Ndama huyu asitusunbue,kufanya kazi kwa RA eti na yeye anajiiita Mwanachama wa TUCTA au MFANYAKAZI, alafu eti anajiita Seniour member!!!
   
 16. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Kwanza amekuheshimu sana kukuita ndama.....hivi watoto wa Mamba wanaitwaje vile? Nona hilo ndo saizi yako...ama uitwe Kenge, itafaa zaidi....unapenda lipi kati ya Kenge au Mjusi? Maana welewa wako ni kama wa sisimizi.....
   
 17. K

  Kitukuu Member

  #17
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 26
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Usije ukawa bendera kufuata upepo... nafsi yako inakuambia nini? Au utampa kura Kikwete kwa vile tu chama chako hakikushiriki mgomo na pengine uliamriwa na wakuu wa chama chako?

  Aman!
   
 18. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Inanikumbusha ile taarabu "zege ukishalikoroga haliludi kuwa cement" naona JK kama angeweza yarudisha yale maneno naona ndo angekuwa na Peace of mind.
  Mgaya komaaaaa wafanyakazi TUKO nyuma yako,na iyo rushwa ya kuongeza fungu kinyemela hatuitambui.
  CCM lazima wajifunze nidhamu ya kumjari mteja na sio kuongea maneno ya kejeri vile kwa watu ambao monthly wanakatwa PAYEE ambazo zatumika kumfanya atoe very hopeless kauli.
  JK CUSTOMER CARE ZERO SASA UNAPITA JUKWAANI KUOMBA KURA ZA NINI?NDO MAANA WAANGU ANGUKA BSE DHAMIRA INAKUSUTA
   
 19. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Si ndiyo ninyi mlioingizwa kwenye makapuni na wazee wenu sasa kiburi kinawapanda. Yana mwisho hayo. Kuleni hivyo visenti kwa mara ya mwisho kabla pingu hajawatembelea. You know what I mean!!!!
   
 20. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2010
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  JK anajaribu kutoa TAKRIMA kwa wafanyakazi ili wasahau kauli alizo zitoa dhidi yao. Anaongeza mishahara bila hata ya kuwafahamisha....
   
Loading...