Tuchukue taadhari...kwa watumiaji wa daladala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuchukue taadhari...kwa watumiaji wa daladala

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Watu8, Jun 25, 2012.

 1. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,332
  Likes Received: 2,636
  Trophy Points: 280
  I have just received this email from a friend.. It has happened to a cashier from TIB (Tanzania Investment Bank)....Please be aware dunia imeharibika

  Dear friends
  Leo nimeona ni vyema nika-share nanyi kisa hiki cha kutekwa mfanyakazi mwenzetu ambaye ni cashier siku ya jumatano jioni wiki iliyopita.

  Ni kama movie lakini ni ukweli, cashier wetu aliomba ruhusa siku hiyo ya tukio aende kwenye mkutano wa wasabato uliokuwa uliendelea viwanja vya Biafra. Yeye pia ni msabato aliyeishika dini ya Sabato haswa, kwa hiyo aliondoka saa kumi kamili badala ya saa kumi na moja.

  Baada ya dakika 40 tulianza kupokea sms zinazosema mwenye namba xxx amepata ajali na kufa papo hapo na kwa taarifa zaidi twende muhimbili hospital. Baada ya kutazama hiyo namba xxx ilikuwa ni ya cashier wetu. Tulijaribu kuipiga iliita tu bila kupokelewa, na pia tulipiga namba iliyotutumia sms iliita bila majibu. Ilipofika saa kumi na moja tuliamua kuelekea muhimbili, ma baada ya kufika pale emergence tukaambiwa tuelekee chumba cha kuhifadhia maiti. Tulioneshwa mwili wa mtu aliyepata ajali lakini haukuwa wa cashier wetu, tukawatuma wenzetu waende hospitali zote lakini hapakuwa na taarifa zake

  Baada ya kuzunguka bila mafanikio tulitoa taarifa makao makuu ya usalama barabarani na baada ya dk kumi wakatwambia kuwa hakuna taarifa za ajali mbaya iliyotokea jioni hiyo. Hatua iliyofuata ilikuwa ni kutoa taarifa polisi juu ya tulio hilo na ndipo waliposema kwa kuwa ni mtu mzima tusubiri hadi siku inayofuata. Wakati huo huo ndugu zake pamoja na wafanyakazi wenzetu walikuwa pamoja wakiendelea na jitihada za kumtafuta hadi saa sita usiku. Kilichokuwa kinatia wasiwasi zaidi ile namba iliendelea kutumia sms namba takribani zote zilizokuwa kwenye phonebook yake na ndugu zake hawakuwahi kuona ndugu yao akichelewa kiasi hicho.

  Ilipotimu mida kama ya saa sita na nusu walisikia mtu akigonga mlango, alikuwa kaumizwa na amejaa matope, hakuwa na uwezo wa kuzungumza sana, ilibidi wampeleke kituo cha polisi na baada ya muda hospitali ya mwananyamala.

  Alipopata nguvu alianza kuwasimulia nduguze kilichotokea. Alipotoka ofisini alikwenda moja kwa moja kwenye kituo cha daladala cha karakana, pale kituoni walikuwa abiria wawili yaani yeye na mama mmoja. Baada ya dk chache ilikuja coaster iliyoandikwa mbele Kawe na ilikuwa na tinted nyeusi, yule mama hakupanda sababu alikuwa anaelekea posta ila yeye alipanda. Ndani ya gari kulikuwa na watu watatu pamoja na dereva, wawili wakiwa wamekaa nyuma na mmoja akiwa amekaa karibu na driver.

  Gari hiyo hiyo ilikuwa ni mpya, mmoja wa abiria alimumba simu cashier apige simu moja kwa jamaa yake maana alidai kuwa simu yake illiishiwa charge na walikuwa wametoka mtwara kupeleka maiti, alimuuliza cashier umri wake na kama ameoa na anafanya kazi wapi, cashier akamjibu hajaoa na hana kazi pia ana miaka 32. Walipofika Tazara hawakutaka kupakia abiria yoyote na walikuwa wote wamevaa miwani myeusi, na ndipo akaanza kuingiwa na mashaka akaomba ashuke, wao wakamwambia watapita biafra na hawana mpango wa kusanya kwa kuwa hata yeye walimpa lifti tu.

  Gari ilipokaribia taa za buguruni akainuka ili ashuke, jamaa wale wa nyuma wakamkalisha chini kwa nguvu, na sio kwenye viti yaani chini kabisa. Mmoja wao akafunga kitambaa cheusi kwenye macho na mikono ikafungwa kwa nyuma na mipira, baada ya muda akasikia kama wamempulizia perfume. Akihisi fahamu kumtoka polepole na neno lamwisho analokumbuka alisikia kuwa waelekee misitu ya Kibaha wakamalize kazi.

  Kilichomwamsha ni kofi zito alilopigwa na kusukumwa hadi nje ya gari. Alianza kulia na kuwasihi wasimdhuru, wakaanza kumrusha kichurachura huku wakimkanyaga. Walikuwa wameshamfungua kitambaa machoni na waliacha gari umbali kama wa dk kumi na lilikuwa ni pori zito na giza, wao walivaa vitu usoni na walikuwa wamevaa gloves. Wakamwekea simu yake mfukoni wakiwa wametoa simcard, walichomwambia wanachohitaji ni sehemu zake za siri na sio kitu kingine.

  Mmoja wao akaambiwa alete kisu kikali wanachokitumia, na walipompigia boss wao akawasisitiza nyeti zinazotakiwa lazma ziwe za mtu wa miaka 40 na kuendelea. Mwenzao mmoja akasema cashier alisema alikuwa na miaka 32, baada ya kumkagua wakakuta card yake inaonyesha kazaliwa mwaka 1979. Kulingana na yeye asemavyo ndicho kilichomwokoa ila waliendelea kumkung'uta kwa hasira.

  Wakamrudisha kwenye gari na baada ya mwendo wakampakia kwenye gari nyingine ndogo iliyokuwa na watu wawili ambao walimchukua na kumtelekeza maeneo ya sayansi. Hawakuchukua kitu hata kimoja wala kumwambia lolote,siku iliyofuata alipelekwa agakhan kwa uchunguzi zaidi na kwa sasa anaendelea vzr.

  Kwa ufupi ni hayo, ukweli mwenyezi Mungu atulinde na tumwombe pia abadilishe mioyo ya watu ambayo imekuwa migumu mno kwa ajili ya kupata vyeo na utajiri wa haraka

  Watu wanatafuta vyeo maofisini kwa njia hii.


  Hii taarifa nimepokea toka kwa rafiki imetumwa kwenye blog yetu, watz tuwe makini si watu wote ni wema, ni Mungu tu ndiye aliyemwokoa huyo mwenzetu.
   
 2. ERIC JOSEPH

  ERIC JOSEPH JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  poleni sana pia mpe pole sana kwa kupatwa na tukio baya mungu amwepushie mbali.pia amjalie afya njema
   
 3. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,749
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Dah hii kali!kwa jinsi hii foleni dar haiwezi kukoma,kila mtu atahitaji kuwa na kagari kake.
   
 4. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,332
  Likes Received: 2,636
  Trophy Points: 280
  nishawahi kusikia nadhani ni hapa jamvini...kuwa maeneo ya M'nyamala si salama kupanda daladala mida ya usiku mkali maana dereva na konda wote wanakua ni vibaka...ukiingia ndani ya daladala unakombwa kila kitu
   
 5. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Imeenda kula kwingine hiyo du mpe pole
   
 6. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Ee mungu baba uturehemu! Hili ni tukio la hatari mno,mungu pia amlinde na kumponya yule aliyepatwa na tukio hlo.
   
 7. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  Balaa kubwa hili, unaweza kuta tayari mtu kashatolewa uhai.
   
 8. doup

  doup JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  poleni jamani, tutoe tahadhali, kwa hali hii naogopa hata kutoa lift binadamu tumekuwa na roho mbaya sana, yote hii ni kuwa kiongozi & Serikali DHAIFU,
   
 9. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inasikitisha
   
 10. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,332
  Likes Received: 2,636
  Trophy Points: 280
  yup bila shaka kuna mtu mwingine aliyekidhi vigezo upande wa pili kashanyofolewa nyeti.
   
 11. salito

  salito JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  mhh msiba huu jaman binadamu tunaroho ngumu sana..
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha kwa kweli, hivi sasa hakuna mtu wa kumuamini kwa kweli.
   
 13. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Ee Mungu tusaidie, tunashukuru huyo kaka kupona. Mie nitakuwa nahakikisha daladala limejaa ndo napanda, lol.
   
 14. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Terrifying story!
   
 15. m

  majiyachupa Member

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  mie nitakua napanda daladala Za kugombea tu. Heri nisimame posta mbezi kuliko kukatwa dudu
   
 16. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Kabisaaaaa, ya kutaka viti ya nini? wakati usalama mdogo.
   
 17. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Poverty is a source of all crimes!!!! It is a source of unhappy life, it lowers human dignity!!! All you can see and hear today, their source is poverty!!! Finally in a country wellgoverned poverty is something to be ashamed of. In country badlygoverned, wealth is something to be ashamed of. Tafakari!!
   
 18. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  inasikitisha sana,yanaweza kumkuta yoyote yule!tuombe mungu hao wataka firigichi ya kiume wakomeeee!
   
 19. B

  Bob G JF Bronze Member

  #19
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ni Hatari sana
   
Loading...