Jaji Tz
Member
- Feb 16, 2015
- 33
- 19
MAANA YA ELIMU
Kwa maana yake ni ujuzi au Maarifa .
Utoaji wa elimu inamaanisha mchakato ambao maarifa, tabia, mila na maadili ya jamii moja hupitishwa kwa kizazi kijacho.
Kwa maana ndogo ni lazima elimu iendane na jamii na husika ili kuwawezesha wananchi kuweza kuitumia elimu ile ili iweze kuleta tija ,ni lazima elimu iendane na mila na utamaduni wa jamii husika ili kuweza kupitisha maarifa yale kutoka kizazi hadi kazazi kingine kizazi .
Elimu ni mchakato wa kipeleka maarifa kwa jamii kwa namna gani wanaweza kutatua changamoto zao zinazowakabili na kutumia fursa katika mazingira yanayowazunguka na kuleta tija kwa jamii husika, ni lazima elimu iendane na mazingira .
Ni muhimu elimu kuwapa watu uelewa mpana wa fursa na uwezo wao na kufuta dhana potofu za kuamini kuwa hawawezi au kuwa tegemezi kwa wengine kwa kipare tunasema Decolonization of Mind hapa ndipo changamoto kubwa ilipo kwani kila kitu kinaanzia kwenye akili .
Sasa ni wakati wa kuingalia elimu yetu na kitoa mapendekezo yatakayoleta tija katika mifumo yetu ili tuweze kujinasua na kuwa katika mazingira bora zaidi ya sasa ,kwa kutoa maarifa yatakayoleta tija kwa kutambua,kutumia fursa lakini pia kutatua matatizo yanayoikumba jamii yetu na kifanikisha haya ni lazima elimu yetu iwe ni elimu yenye sifa au inayoendana na sifa zifuatazo ;
(1) Elimu inayoendana na utambuzi na uinuaji wa vipaji ,mtakubaliana nami kwamba watu waliofanikiwa zaidi ni watu wenye vipaji na walioweza kutumia vipaji vyao sasa umefika wakati wazazi pamoja na taasisi za elimu kutambua na kukuza vipaji vya watoto au wanafunzi wao kwani hii itamwezesha mtoto/mtanzania kujiajiri ,kuajiri wengine na kuwa chanzo cha mapato kwa serikali .
(2) Elimu itakayochochea ugunduzi ,uvumbuzi pamoja na tafiti kwa maendeleo ya Teknolojia , kuna mstari wa Biblia unasema
" Asieamini wa nyumbani kwake huyo ni mbaya kuliko asieamini "
Sasa ni wakati wa kuamini taaluma zetu na kuinua teknolojia yetu bila ya kujali wenzetu wamefika wapi kwani hata mbuyu ulianza kama mchicha sasa ni wakati wa kuanza kwa mustakabari wa Taifa letu sasa na miaka ya mbeleni ,wanafunzi wafundishwe na kupewa nafasi ya kutafakari na kugundua tatizo na kulitafutia ufumbuzi pamoja na kutoa motisha kwa vijana/watanzania kugundua vitu kwani watanzania ni wengi na wana uwezo .
(3)Elimu itakayofungua fikra za watanzania na Uafrika wao kwa kufuta dhana potofu dhidi ya Afrika Mfano . Utegemezi wa Afrika .Elimu yetu isiwe ni njia ya wenzetu wale kuendelea kutukandamiza bali ikawe mwanga wa kufungua macho na kutambua tulipotoka ,tulipo na kule tunapotamani kwenda na kutupa fikra na maono chanya na yenye tija na kutukumbusha wajibu wetu kama waafrika , tulipata uhuru wa kisiasa lakini bado kuna changamoto ya uhuru wa kiuchumi na hatuwezi kisonga mbele kama hatutaanza na sekta ya elimu .
(4)Elimu itakayotoa wataalamu waliobobea katika fani zao kwa kuwapa muda mzuri na wa kutosha kusoma kwa undani na tija katika fani zao ,kuna msemo unasema
" It is better know nothing rather than half-knowing many things "
Ina maana kuwa ni bora kutokujua kitu kuliko kujua kwa uchache vitu vingi ,hivyo ni wakati wa elimu yetu kupunguza mizigo ya masomo na programu ili kuwapa fursa wanafunzi kubobea katika fani zao ambapo sio tu italeta tija kwa nchi bali pia kupata kipaumbele zinapotokea fursa za kikanda na kimataifa .
(5) Elimu itakayoendana na wakati na sehemu husika ili kuweza kutoa fursa kwa wananchi kupata suluhisho na kutambua fursa zinazowazunguka ili iweze kuwa na tija na kutoa suluhu ya matatizo ikiwemo tatizo kubwa la Ajira linalokumba mataifa mbalimbali . Kwa mfano somo la ujasiriamali au uvuvi kutolewa kwa wananchi katika maeneo yenye vyanzo vya maji ili kuweza kutumia elimu na maarifa waliopata kutumia fursa inayowazunguka kwani elimu ni maarifa yanayoiwezesha jamii kutumia fursa na kujiletea maendeleo kama itakuwa kinyume na hivi basi itakuwa ni mfumo wa kuchelewesha maendeleo kwa kutoa ujuzi usio na tija kwa jamii .
(6) Elimu ijumuishe masomo ya TEHAMA na kuunganisha taasisi zetu na TEHAMA ,lazima tukubali kuwa sasa tunaishi kwenye ulimwengu wa TEHAMA na sasa huduma nyingi zinatolewa kwa njia ya tehama na hii itawapa fursa wahitimu katika Ajira na shughuli zao za uwekezaji kwani wahitimu ni wengi lakini wanaofahamu tehama ni wachache , mtakubaliana nami kuwa hata tukichukua wanafunzi kumi wa vyuo wanaoweza kutumia Microsoft Excel utapata wachache au kukosa kabisa hii inawanyima fursa hasa kwenye nafasi shindani za kikanda na kimataifa .Na pia tutambue kuwa kwenye TEHAMA kuna fursa nyingi kuliko sehemu yoyote ile leo hata matajiri wakubwa duniani wametokana na TEHAMA Mfano, Bill Gates
(7) Elimu itakayolinda Afya na ustawi wa wananchi wa Tanzania
Kuna msemo ambao hata wizara ya Afya wanautumia
" Afya yako ,Mtaji wako " hivyo ni lazima tutambue kuwa ili tujenge taifa letu kitu cha kwanza kulinda ni Afya zetu hivyo lazima elimu pia ijikite katika pande hizi kwa kutoa elimu kwa wanafunzi na jamii namna bora za kulinda afya zao dhidi ya Magonjwa kwa kuwapa njia za kisayansi lakini kwa umuhimu sana zile za mababu zetu za asili kwani Mkataa vyakwao ni mtumwa kuwepo mfumo mzuri pia wa kutoa ujuzi huu kwa jamii kwani ndio njia hizi zilitumika na mababu zetu na walikuwa na afya njema lakini sisi tunaotumia njia za kisayansi tunakutana na changamoto nyingi mpaka vijana kulalamikiwa bungeni kuwa utendaji kazi wao hauridhishi pamoja na mambo mengine maswala ya lishe ili kupunguza matatizo ya shinikizo la damu na magonjwa mengine .
(8) Mwisho lakini sio kwa umuhimu Elimu yetu iwe elimu itakayochochea uzalendo kwa taifa letu kwa wanafunzi kufahamu Historia ya Taifa letu na Afrika yani tulipotoka na tulipo , kutambua kwa undani wake tunu za taifa letu ikiwemo lugha yetu adhimu ya kiswahili pamoja na Muungano wetu ,kufundisha maadili ikiwa ni pamoja na kupiga vita rushwa na ufisadi na kuweza kuzalisha wasomi wazalendo wenye upendo na taifa lao na wanaotambua majukumu yao .
Maoni na mapendekezo ili kuboresha sekta na Mfumo wetu wa Elimu ;
(1)Kuanzisha na kuendeleza Vyuo vya kati vya ujuzi vikiwemo vya ufundi (VETA) pamoja na vya ujasiriamali ili kutoa maarifa kwa watanzania kwani wajuzi hawa watafungua fursa kwa
wengi zaidi .
(2)Kuwekeza katika kukuza Teknolojia nchini na ikiwa ni pamoja na kutoa motisha na Taasisi zinazohusiana na kukuza Teknolojia kuondoa Urasimu .
(3)Masomo ya msingi kama Uraia ,Historia ,Lugha ,Geografia pamoja na masomo ya Baologia na mengine yanayoangukia katika kundi hili la msingi kufundishwa katika Ngazi ya Msingi na Tahsusi za ubobezi kuanza katika ngazi ya sekondari yani kidato cha kwanza ili kuweka ubobezi katika fani zao .
(4)Kuhamasisha na kufadhili tafiti pamoja na programu mbalimbali zenye lengo la kutoa suluhu ya matatizo na kugundua kitu kipya na hivyo kuwa fursa kwa jamii.
(5)Kuanzisha Program Mbalimbali katika taasisi zetu za elimu pamoja na jamii za kuinua na kukuza vipaji ikiwemo na kuanzisha taasisi ya kulea vipaji ,kwa mfano Academs kwa maswala ya Michezo .
(6)Ujenzi na uendelezwaji wa Maktaba katika Vyuo vyetu pamoja na shule na zile za jamii (Public Libraries) kwa ununuzi wa vitabu vyenye tija na vinavyoendana na wakati ,kuunganisha TEHAMA na kuajiri na kuendeleza wataalamu wa maktaba na hii iendane sanjari na ujenzi wa Maabara na Miundombinu bora na ya kisasa katika taasisi zetu za elimu .
(7)Na mwisho lakini si kwa umuhimu ,kufanya upembuzi wa mara kwa mara (Frequent Reviews) katika mfumo wetu wa elimu kwa kufanya tafiti ili kutambua changamoto na maboresho ili kuwa na elimu yenye tija na inayoendana na wakati .
Ni wakati wa kuichambua na kuitafakari elimu yetu ili iweze kuleta tija kwa jamii na taifa kwa ujumla wakati wa sasa .
Kufanya mabadiliko au kuona mabadiliko sio kutokutambua umuhimu wa elimu yetu bali ni lazima tuangalie na kuboresha elimu yetu hii ili kuendana na wakati na kuifanya iwe tija na sio chanzo cha malalamishi kwa wahitimu na wananchi kwa ujumla .
Ni lazima tutizame idadi ya wahitimu na uwezo wa serikali kuajiri na soko la ajira kwa ujumla ili kupunguza mzigo mzito wa Ajira uliobebwa na serikali kwani kwa namnà yoyote serikali haiwezi ajiri watu wote .
Kumekuwa na mjadala mkubwa zaidi dhidi ya Degree zilizopo mtaani kuwa hazina tija kwa jamii zaidi ya utegemezi ,wakati ni sasa wa kuchambua kati ya ngazi ya elimu na elimu ya ujuzi yenye tija kitu bora ni kipi ??
Kumekuwa pia na mjadala kwa baadhi ya wabunge kulizungumzia swala hili kwa pamoja ili kuweza kutengeneza Tanzania tunayoitamani wote na nina imani kuwa maelezo haya kwa ufupi yataenda kuchochea mawazo mengi mazuri na yenye tija kutoka kwa watanzania wenzangu .
Lazima tutambue kuwa elimu yetu ndio maendeleo yetu na maendeleo yetu ndio uhuru wetu wa kiuchumi ,na tutambue kuwa mabadiliko ni sehemu na maendeleo na maisha ya binadamu ni lazima tukubali kubadilika .
Nahitimisha makala hii fupi kwa salamu yetu pendwa ,
NAWASALIMU KWA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA [emoji1241][emoji1241]
Kazi Iendelee
Amon Nguma
0620615659
ELIMU YETU ,MAENDELEO YETU [emoji1241][emoji1241][emoji1241]