Tubadilike

ndupa

JF-Expert Member
Jan 25, 2008
4,403
141
si vyema wananchi wote watanzania hususwa ni vijana tukakabidhi imani yetu kwa wanasiasa eti watatukomboa. nadhani
mtakubaliana na mimi kuwa kinamama ni kundi lakwanza lililo amini kuwa ukombozi wao upo katika siasa na wakajiingiza
kikamilifu katika kipindi cha kwanza, cha pili, na chatatu tangia vyama vingi vilipofumuka. walikuwa washabiki wakubwa wa chama tawala kwa kuamini kuwa ni mtetezi wao. walidiriki hata kusema kuwa chama hicho ndicho kilichowalea.

Pamoja na hivyo waliendelea kuwa masikini huku wale waliowachagua kuzidi kumiliki mali. hilo wameligundua na wanajaribu kukaa penbeni na kutafuta njia nyingine yakujikwamua kiuchumi.

Sasa tuwatazame kina mama walivyopiga hatua kimeandeleo wanavyomiliki mali kushinda wanaume.

Tembelea mikoa ya ARUSHA, KILIMANJARO na hata TANGA uone kinamama walivyofadika na ujasiriamali.

Hali ya umasikini sasa imeamia kwa vijana ambao wamekuwa na sera ileile ya kuwa siasa ndo mkombozi wao .wamekuja upande mwingine wa shilingi eti wanachama pinzani, chama dume, chama cha wananchi, chama cha demokrasia na maendeleo.

Nadhani tujifunze toka kwa kina mama ambao wamepunguza morali ya siasa na kujiweka bize kwenye ujasiriamali na kupelekea idadi ya wapiga kura kuporomoka ghafla miaka ya sasa.

Hakuna chama pendwa wala mtetezi wa wananchi ndani ya bara hili. ukistaajabu ya kibaki utayaon ya kikwete. na ukitaka
kujua undani wa RAILA ODINGA. Jitahidi kujua undani wa lowasa kwanza. kiko chama kilicho ahidi elimu bure wilaya ya
moshi kama kitapata halmashauti yaani umeya. sasa tumekipa lakini hali ni ileile kama ilivyo halmashauri nyingine.

TUBADILIKE TUACHANE NA WATU HAWA TUCHAPE KAZI TUJIKWAMUE. TUSIANDAMANE KWA MASLAHI YAO. TUSIFE WALA KUPATA ULEMAVU KWA AJILI YAO. HAWANA NIA NZURI KWETU ZAIDI YA KUMILIKISHA MALI FAMILIA ZAO NA SIVINGINEVYO
 
tunapumua siasa,tunakula siasa,tunatembea siasa..mkuu siasa haiepukiki
sisi tutapambana na magamba mpaka kieleweke
 
wazo zuri ila lina mapungufu.........vijana tuchape kazi na kujiletea maendeleo yetu wenyewe ni sawa lakini tusisahau kufuata na kuamasisisha siasa safi kwani ndio nguzo ya maendeleo kijamii na kiuchumi
 
Back
Top Bottom