Tubadilike, watoto wanajifunza kwa matendo yetu.

Wisest man

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
993
332
Ubinafsi ni tabia ya kufanya mambo huku ukitanguliza maslahi yako mbele bila kujali mtu uliye karibu naye.

Ni kweli kwamba kujipenda kwanza ndio jambo la msingi lakini tafsiri hiyo haipaswi kuhusishwa na dhana nzima ya ubinafsi kwa sababu watu na mazingira yanabadilika kila wakati.

Watu wanakiri kwamba kwa sasa mahusiano miongoni mwa watu yamebadilika kwa miaka michache iliyopita kiasi cha kwamba kila mtu amekuwa akijifijiria yeye kwanza na kushindwa kumfikiria mtu aliyeko karibu yake.

Katika mada hii napenda kugusia kuhusu baadhi ya watu kutoonesha ushirikiano kwa watoto kuanzia wanaoanza kuona na kuelewa(miezi sita, mwaka na kendelea) huku wakisahau kwamba watoto wanajifunza kutoka kwao na kwamba, watoto ndio wazazi wa baadae(taifa la kesho).

Kwanza nimegundua watoto wadogo wana utambuzi mkubwa wa tabia kuhusu mtu wanayemuona kutokana na vile mtu huyo anavyowatendea/kuwachukulia wakati mnaookutana iwe kwenye daladala, hospitali, dukani na hata nyumbani.

Nimekuwa nikiwaona watoto wadogo wasioweza hata kutambaa wakionesha kufurahi kukuona labda mko jirani na kiti alichokaa mzazi wake kwenye daladala ila kwa makusudi au bahati mbaya unashindwa kumuonesha mtoto huyo kwamba na wewe umefurahi! hivyo anajiuliza kwanini hukushiriki furaha yake? Kama mtu huyo anakuwa karibu naye kila siku atafikia hatua ataanza kukukwepa kwa sababu anaona humpendi, ndio maana kuna watu wanakataliwa na watoto lakini hawajiulizi kwanini kwa wengine mambo ni tofauti?

Upo kwenye daladala karibu na mtoto usiyemfahamu anakuona unanunua ndizi au kinywaji unaanza kula na kunywa bila kushiriki naye japo kumnunulia huku akionesha kuhitaji ulicho nacho ila unaendelea kula na kunywa bila kujua ni kwa kiasi gani umemuumiza kisaikolojia mtoto huyo.

Upo na gari yako unaona watoto wanaotoka shule wakihangaika kutafuta usafiri wa kuwarudisha nyumbani baada ya kuvumilia njaa na shuruba nyingine za shule lakinj wewe ukiwa kondakta wa daladala au mtu uliye na usafiri binafsi unashindwa kuwasaidia unawajengea mtazamo gani wa kiulimwengu? Je watajuaje kutenda wema ikiwa hukuwafundisha jinsi ulivyo na unavyotendwa?

Unapokuwa karibu na mtoto mdogo hata wa miezi minne jitahidi kumfanya ajisikie furaha. Watoto wakati mwingine hupenda kufurahi na watu wasiowafahamu wanapokutana, akionesha furaha kwa kucheka na kurusha mikono na miguu nawe muoneshe kwamba uko pamoja naye, na kwa kufanya utakuwa unamhengea ufahamu wa kwamba anapendwa hivyo analaswa kuwapenda wengine.

Binafsi ni rafiki mkubwa wa watoto, hata kama wazazi wake nina ugomvi nao bado nawachukulia kwa jicho la upekee, nawapenda watoto nao wananipenda.

Tuwapende watoto na tusiwafanye wajisikie vibaya kwa namna yoyote ile, tambua kuwa unachomfanyia mtoto leo ndicho atakachowafanyia wengine kesho.

MTOTO WA JIRANI YAKO NI MTOTO WAKO.
 
Unachosema ni kweli kabisa Mkuu. Huu mtindo nimeufanya kama sehemu ya maisha yangu, huwa nawaonyesha sura ya tabasam na Changamko hata kama simfaham mtoto wa nan basi nao hufurah na kucheka pamoja nami. Nimejikuta kuelewana na makundi mbali mbali ya watoto, wengine hata majina siwafaham lakini wao wananijua..
Tuwapende watoto
 
Unachosema ni kweli kabisa Mkuu. Huu mtindo nimeufanya kama sehemu ya maisha yangu, huwa nawaonyesha sura ya tabasam na Changamko hata kama simfaham mtoto wa nan basi nao hufurah na kucheka pamoja nami. Nimejikuta kuelewana na makundi mbali mbali ya watoto, wengine hata majina siwafaham lakini wao wananijua..
Tuwapende watoto
Inafurahisha sana mkuu. Watoto ni sehemu yw furaha, ndio maana mtoto akikosekana ndani ya familia nyumba inapoa, akiwepo furaha inatawala.
 
Watu wengine ni makauzu hadi kwa watoto sijui huwa wanawaza nini, hata kama mtu hana interest na watoto so hivo asee
 
Back
Top Bottom