Alitokea baba mmoja ambaye mungu aliibariki nyumba yake,akawa na mali nyingi na utajiri wa kila namna
ajabu ni kwamba baba huyu hakuthamini mali hizi. zaidi familia yake iliishi kwa mateso kwani hakuwapatia mahitaji yao ya msingi.
vijana wake waliokuwa na uelewa walimhoji baba kwa kitapanya mali zile na kuwanyima mahitaji yao ya msingi. baba huyu aliwaadhibu vijana hawa kwa kushirikiana baadhi ya wanafamilia ambao aliwahonga. baadhi ya vijana hawa werevu walipoteza hata uhai.
pale ilipobidi baba huyu aliuza hata vitu vyenye thamani kubwa ili apate hela za kuwarubuni wale vijana wapumbavu ili wawatenge na kuapiga vita wale werevu.
ilifika kila baba huyu alipotapanya ile mali ya familia wale wapumbavu walimshangilia. alingia kwenye kumbi za starehe za kila namna. alifanya uhuni mwingi huku akishangiliwa. kila aliyempinga alikiona cha mtema kuni.
baba huyu alifika mahali akawa hafungi hata milango ya nyumba yake. majirani walikuja na kuingia hata chumbani mwake, walichakura hadi nguo zake za ndani. wale vijana werevu walipiga kelele mwiziiii,mwiziiii lakini wapi. wale vijana wapumbavu kwa kushirikiana nababa yao hawakujali. waliwatenga wale waliokuwa wakipiga kelele na kuwaita wapumbavu.
sasa hivi yule baba amechanganyikiwa kuona ndani hamna kitu. hata hela ya kulewea hana tena. amewageukia wale akiowaruhusu kuingia chumbani kwake na kuwaita wezi.baadhi ya wale vijana waoumbavu walikuwa wakimshangilia na kuruhusu majirani kujitwalia vitu wamemgeuka baba huyu.
TUPO HAPA KIJIWENI TUNAJADILIANA SIJUI BABA ATAPATWA NA NINI. HATA KAMKATE KA KUNYWEA CHAI HATUJAPATA.......