Darvon
Member
- Apr 14, 2018
- 93
- 74
Habarini za asubuhi.
Wakati tunakwenda makazini tujukumbushe yafuatayo.
Mambo yamebadilika kwa sasa na dunia imekuwa kijiji ambacho mwenye nguvu ndio anakula mema na tunawaandaa watoto wetu kuja kuishi na mwanakijiji mwenzie kutoka huko kwenye kona nyingine ya kijiji, hivyo basi tuwape maarifa kupitia elimu nzuri, kwa dunia hii wewe jiandae tu kutawaliwa milele endapo utashindwa kuwatengenezea mazingira mazuri wanao yatakayokuja kuwasababisha wawe na nguvu katika jamii wazungu wana msemo wao "Survival of the fittest"
Nakuambia niamini mimi kila kitu kizuri duniani ni gharama, mtoto hatakiwi afaulu tu mzee anatakiwa yaani ukikaa nae unaiona dunia nyingine nyumbani kwako. Nenda tu hapo kenya utagundua tofauti yetu na wakenya kwenye hiyo idara unaweza kuwa na makampuni au majumba mazuri lakini nakuhakikishia kuwa na mtoto aliyeandaliwa katika kiwango cha dunia ya kwanza ili asitafute kazi ila kazi zimtafute ni gharama sana.
Endapo pia gharama huna hilo sio tatizo muweke mtoto katika misingi mizuri itayomfaa katika maisha yake, mpe maarifa tofauti tofauti huku ukihakikisha kuwa haendi kuungana na makundi mabovu ya kumfundisha tabia za hovyo.
Thamani tunayowapa watoto wetu ndio watakayokuwa nayo maisha yao yote, maisha uliyonayo wewe ndio yanayowapa heshima wao pia mtaani, kizazi chetu kisije kuwa cha kudharaulika, nakuhakikishia kuwa ukishindwa kumuandaa mtoto wako aje kuwa "fit" zaidi ya wengine atadharaulika yeye, wewe, na wengine wote waliohusika katika future yake.
Sipendi ile tabia mzazi kumuambia mwanae mbona mimi nilitembea peku? Mbona nilivaa nguo zilizotoboka? Ni kama mtu vile anapambana kulipa visasi kwa mtoto, dunia ya leo ukimuandaa mtoto kwa aina hiyo ya maisha kumuacha kama vile hana wazazi, utakuta amechomwa moto, dunia ya leo sio ile ya 70, 80, na 90s.
Binafsi ninamuomba Mungu aniwekee kizazi changu, sina jina wala uwezo kivile wa kuwafikia watu kama kina @djkhaled na wenzake, ila muda si mrefu wajiandae kuona upendo wa masikini kwa mwanae unakuwaje.
Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha..!
Muwe na siku njema.