TUAMUE KUHUSU ZANZIBAR NA SIO KAULI. MAAMUZI YANA GHARAMA, TUKUBALI GAHARAMA.

Aug 1, 2012
35
27
KAULI HAZIKUMALIZA MGOGORO WA ZANZIBAR TANGU MWAKA 1995, MAAMUZI YALIMALIZA MGOGORO ZANZIBAR 2010, KAULI ZA LEO NI ZA KUTURUDISHA KWENYE CHUKI NA UHASAMA ZANZIBAR. Azimio la Baraza la Wawakilishi Baraza la Wawakilishi la Zanzibar mnamo tarehe 28 na 29 Januari 2010 lilijadili hoja ya mapendekezo ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Hoja hiyo iliwasilishwa kwenye Baraza la Wawakilishi na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Mgogoni Pemba Mheshimiwa Abubakar Khamis Bakary. Katika hoja hiyo, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliombwa kupongeza na kuridhia mazungumzo ya maridhiano yaliyofanyika tarehe 5 Novemba 2009 baina ya aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dr. Amani Abeid Karume ambaye alikuwa pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, na Mhe. Seif Shariff Hamad – Katibu Mkuu wa chama cha Civic United Front (CUF). Aidha, wajumbe waliombwa wakubali kuanzishwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi mkuu wa 2010. Baraza la Wawakilishi liliikubali hoja hiyo kwa masharti kwamba kufanyike kura ya maoni kwa ajili ya kutafuta ridhaa ya wananchi kuhusu jambo hilo na Serikali ilete mswada wa sheria kwenye Baraza ili utengenezwe utaratibu wa kisheria wa kuendesha kura ya maoni. Maamuzi hayo ya Baraza yalipitishwa kwa azimio lilokuwa na vifungu 12. Kwenye majadiliano ya Baraza la Wawakilishi kuhusu azimio hilo, ilielezwa na wajumbe mbali mbali kuwa maridhiano ya kisiasa baina ya CCM na CUF yamefikiwa ili kuondoa migogoro na mivutano ya kisiasa Zanzibar iliyodumu kwa muda mrefu tangu kurejeshwa kwa mfumo wa siasa za vyama vingi Tanzania na hususan Zanzibar kuanzia mwaka 1992, Uchaguzi wa kwanza katika mfumo wa vyama vingi tangu baada ya Mapinduzi ya 1964 ulifanyika mwaka 1995 ambapo mivutano ya kisiasa ilijitokeza wazi wazi baina ya vyama viwili vikuu vya siasa hapa Zanzibar yaani CCM na CUF. Uhasama na chuki za kisiasa zilishika kasi. Chama cha upinzani CUF kilikataa kuyatambua matokeo ya uchaguzi wa Rais na pia kilikataa kumtambua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye wakati huo alikuwa Mheshimiwa Dr. Salmin Amour Juma.

Aidha, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Upande wa Upinzani (CUF) walisusia vikao vya Baraza kwani walihudhuria vikao hivyo kwa kupangilia ili wasipoteze sifa tu za kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa mujibu wa Katiba. Vilevile wajumbe wa CUF hawakuwa wakizungumza wala kuchangia chochote ndani ya baraza la wawakilishi na wakati Rais alipokuwa akiingia ndani ya baraza la wawakilishi wao walitoka nje ya baraza. Kitendo ambacho kilikuwa kinafikisha ujumbe kwa serikali na kuzidi kujenga chuki miongozi mwa wazanzibari ambao waliamini CUF ilikuwa inashinda uchaguzi na CCM kupora ushindi wa wananchi.

Matokeo ya Uchaguzi wa mwaka 1995, 2000, na 2005 yalionesha wazi zipo hujuma dhidi ya CUF kwa kukaribiana sana kwa matokeo na kutokana na nguvu kubwa waliokuwa nayo CUF ndani ya Zanzibar hii ndio iliendelea kukitesa kisiwa hiki kwa kuwa walio wengi hawapati ushindi kila ifikapo uchaguzi.

Chuki na Uhasama viliendelea na kuweka msingi wa haja ya kuondoa hiyo chuki na uhasama miongozi mwa wazanzibari na kufikia hatma ya kuunza serikali ya umoja wa kitaifa mwaka 2010 iliyodumu miaka mitano huku Zanzibar ikiwa imetulia.

TUMESHUHUDIA KAULI YA JAJI WARIOBA, KAULI YA MSEKWA, KAULI YA MEMBE, KAULI YA JAJI MUTUNGI NA NYINGINE ZITAKUJA, NINI TAFSIRI YAKE?

Itakumbukwa Taifa letu limepitia mchakato wa katiba Mpya ambao ulikwama, na vilevile ikumbukwe kuanzishwa kwake kulitokana na nini? Wachache walipokubali kubezwa na kunyanyaswa bila kujali tafsiri za wengine ndipo kulikofanya serikali ya Kikwete kuamua kuruhusu mchakato wa katiba uendelee, Kambi Rasmi ya Upinzani chini ya Mh Mbowe, Freeman mwaka 2011 ilikubali kutolewa Bungeni kwa matusi, vijembe na kejeli nyingi lakini msingi ukawa umewekwa na mchakato ukatangazwa. Wakati msingi huu unawekwaulipingwa na Waziri wa Katiba na Sheria kwa wakati huo, Ulipingwa na Majaji wa nchi hii wakiwemo wale ambao badae walionesha kuwa na nia Njema na Taifa letu, Ulipingwa na viongozi wastaafu wa taifa hili na kila kona ya nchi hii kuonekana Mbowe na wenzake ni vituko na hawakijui nini wanachokifanya. Kauli za kuupinga uamuzi wa Upinzani kutaka katiba mpya hazikufanikiwa kuondosha ari ya wapinzani kudai haki kwa taifa la Tanzania kupata katiba mpya. Baada ya mchakato kuanza Jaji Warioba akiwa mwenyekiti wa Tume alionesha kuanza kuibeba CCM na baada ya kelele za wataka mabadilko alilazimika kufanya kwa haki pande zote mbili kwa maana ya serikali na wananchi chini ya wabunge wa Upinzani.

Kwa kurejea KAULI mbalimbali za Viongozi wastaafu na nguli wa sheria utaona siasa za kimkakati za CCM zikiwafanya wafanikiwe katika kuhalalalisha mambo yao. Si ajabu CCM kupishana katika hoja, misimamo au mitazamo. Pasipo kuwa waangalifu mnaweza kupima uhalisia wa mambo kwa kauli za wana CCM, ni wazi kama taifa tutapotea. CCM hutumia mwanya wa kutofautiana kwao kwa viini macho kupisha mjadala wa ajenda mahususi. Mfano, Hivi karibuni zilijitokeza kauli katika vyombo vya habari Membe akipinga kurudiwa uchaguzi Zanzibar, hii haikuwa kauli ya Membe binafsi, ni mkakati wa kuwahamisha katika mada na kushindwa kutekeleza mambo muhimu ya kuokoa Zanzibar isitwaliwe na walioshindwa CCM, na watanzania wakahama dhahiri kwenye swala la msingi la Zanzibar na kujadili Kauli za Membe, CCM wanazidi kwenda mbele kujiandaa na uchaguzi ili washinde kwa kiwango kikubwa kwa kupeleka wapiga kura laki moja zaidi kupata ushindi wa margin kubwa.

Itakumbukwa baada ya mkwamo wa katiba mpya bungeni, Jaji Warioba alitoa maoni yake ambayo yalipinga kile kinachoendelea katika Bunge la Katiba, that was a calculative strategy ya CCM ili kuzidi kuvuta muda huku wakikamilisha mambo yao, Kauli mbalimbali zilitoka na Bunge la Katiba lilimalizika kwa kura na hatimaye katiba pendekezwa kupatikana. Tulishuhudia kutofautiana kwa kiwango kikubwa ndani ya CCM lakini walimaliza mchakato kwa pamoja na walisherehekea kupatikana kwa katiba pendekezwa, Kauli za kupinga hazikusadia kunusuru mchakato hadi sasa, I stand to be corrected.

Tofauti ya CCM na vyama vingine nchini ni, CCM wapo consistent katika kutekeleza mikakati yao bila kujali consistent ya hoja na misimamo, Upinzani wako constistent katika hoja bila kujali wanafanikiwa au wanashindwa kutekeleza. (UNAFIKI NA UKWELI Respectively) CCM wapo tayari watukanane wao kwa wao ila mwisho wafanikiwe katika mikakati yao, Upinzani wapo tayari kushindwa ili mradi wanasimamia kweli.

Nilisoma status ya Humphrey Polepole wiki iliyopita katika ukurasa wa facebook, ni mwendelezo wa UNAFIKI kuhakiki mkakati wa CCM unafanikiwa, that’s a state strategy kutumia watu wenye kufikiri juu ya matumbo yao ili mradi wana uwezo wa kusikilizwa na walio wengi na hawawezi ku reason juu ya kile kilichoandikwa, KAULI ZA KUPUMBAZA na kuzidi kupoteza mwelekeo wa mjadala na kujadilimambo ambayo hayatusaidii kama taifa na kuruhusu CCM izidi kutawala.

Vyombo vya habari pia vikimnukuu Mzee Msekwa akishangazwa na Uchaguzi kurudiwa Zanzibar, hawa ni CCM wote, nyani wamoja ila misitu tofauti, ukishangazwa na kauli zao ni wazi huwajui, hata nyani wa mikumi wana milio tofauti ila tabia zao ni moja tuu na muonekano wao ni mmoja tuu wote mikundu yao ina rangi ya nyekundu, wao kwa ndani hawashangaani kwa sababu wanajua wanafanana na ule msamiati wa ‘nyani haoni Kundule’ si kwa CCM, wao wanaonana mikundu vizuri ila wanaonesha nje kama hawaonani(UNAFIKI).

Hoja yangu ni kwamba MGOGORO WA ZANZIBAR HAUTAMALIZWA KWA KAULI, UTAMALIZWA KWA MAAMUZI.

Leo tunaweza kuona na kusikia watu wakisema Jaji Warioba nayo nia njema, Mzee Msekwa nayo nia Njema, Jaji Mutungi (CJ Kenya) anayo nia Njema, Polepole anayo nia Njema, this are just planted thing, wakati CCM wakifanya kazi yao usiku na mchana kuhakiki Zanzibar inakuwa chini ya Shein lazima waoneshe nje kuwa na wao baadhi wanaguswa na kile ambacho pia nyie mnakisema mean while they move forward.

Leo nataka mfahamu uhalisia wa watu kama kina Jaji Warioba na wengine, hawa watu ni typical CCM wanaamini kushindwa kwa CCM ni hatari kwao hawako tayari CCM ishindwe, ukiwa na Jaji Mnafiki, ambae alipinga kinafiki uamuzi wa CCM kulifanya bunge la katiba ni kikao cha chama lakini bado alibaki kuamini CCM itaweza leta mabadiliko katika nchi hii, the same party with the same people halafu tunasema huyu ni mzalendo? Mimi nitabaki kuamini Jaji Warioba ni msomi ila kwenye swala la uzalendo hapana.

Ndugu watanzania wenzangu, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema wanasiasa wa hovyo hutumia hoja za ukabila, udini na ukanda pale inapoonekana hawakubaliki ili mradi tuu wapate madaraka, binafsi nimekuwa muhanga mkubwa wa ukabila, mwaka 2013 Waziri Lukuvi akiwa kanisani Dodoma alikataa kuwaachia Zanzibar waislamu, Wapemba, CCM inatafuta uongozi kwa misingi ya udini. Leo hawawezi sema hadharani lakini Maalimu Seif hawezi kuwa Rais kwa sababu za Udini, Ukanda na Itikadi. Hakuna demokrasia ni ubabe tupu, hawa ndio wanasisa wa hovyo aliowatabili mwalimu Nyerere enzi za uhai wake. Hivi karibuni katika sherehe za maadhimisho ya mapinduzi CCM walifikisha ujembe kwa CUF na UKAWA kuwa hatuwezi kutoa nchi kwa makaratasi, hatuwezi kuwapa nchi machotara, wakaishia kutoa KAULI, Zanzibar haitatolewa hapa ilipo kwa KAULI.

Ndugu watanzania wenzangu, swala la Zanzibar linatuhusu sote, mimi kuishi Njombe kusinifariji kwamba machafuko ya Zanzibar hayanihusu, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema tunahitaji kujikomboa kama Afrika, alifikiria hata mataifa mengine nje ya Tanzania, kwa maslahi ya nchi yetu zaidi kwani amani inapokuwepo kwa jirani ni dhahiri faida inakuwa kwetu sote kiuchumi. CCM hawalioni hili.

Ndugu watanzania wenzangu, NANI WA KUAMUA, CUF IMEJITOA KWENYE UCHAGUZI, CCM WAMESHANGILIA USHINDI, Tujiulize, wakati Zanzibar wanauwawa mwaka 1995, 2000, 2005 CUF ilishinda majimbo mengi na kutangazwa washindi. Pamoja na kushinda na kutangzwa baadhi ya maeneo bado wananchi waliuwawa, leo CCM inatangazwa kushinda kwa asilimia 100% nini matokeo yake? Tukipata majibu ya swali hili tutajua nini kinafata baada ya uchaguzi uliotangazwa wa marudio tar 20Mach 2015. KAULI HAZITALETA SULUHU.

Ndugu watanzania wenzangu, huenda wangeamua kumtangaza Shein kwa lazima Oct 25 2015 pengine Zanzibar ingekwa salama kwani hata 2010 walimtangaza pasipo ushindi Zanzibar ilibaki kuwa salama kwa kuwa wananchi hawakujengewa chuki ya mda mrefu kama ilivyo sasa ushindi wa wazanzibari kwa uwazi kupokwa na kuwapa machungu ya kipindi kirefu bila kuwa na Rais. Binafsi hata walipoamua kumangaza Magufuli kuwa mshindi kibabe naona imesaidia kwani ilikuwa ni haraka kabla watu hawajapata majeraha ya kuonja ushindi wao kwa Mzee Lowassa na haraka wakamtangaza wa kwao, kwa busara haikuwa rahisi ila ilibidi Maisha ya watanzania yawe na thamani zaidi kuliko kuingia ikulu kwa mzee Lowassa na ndio mana hadi leo tuna amani Tanzania.

YAPI NI MAAMUZI SAHIHI KWA SISI WATANZANIA?

Ndugu zangu watanzania wenzangu, ni vigumu sana kuamua katika swala hili kwani uamuzi wake hauwezi kukosa gharama, lazima una gharama, hakuna sheria ambayo inaweza kutetea uamuzi wa kututoa hapa tulipo, Utasikia tuu ‘uamuzi wa tume hauhojiwi na chombo chochote’, ukitaka kwenda mahakamani huwezi sikilizwa, ukitaka kwenda kushauri majadiliano utaambiwa hayata siadia kwani hayapo kisheria. Baba wa haki wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela hakusita kutafuta haki kwa gharama ya yeye kuishi jela kwa miaka takribani 27. Baba yetu wa Taifa hakuamini kukaa na wakoloni kwa kuwa mnyenyekevu kwao, aliamini ili waondoke lazima yawepo mapambano, hakuamini kumuondoa Iddi Amini kwa mazungumzo, aliamini kumuondoa kwa kupigana nae na watanzania kushiriki kumpiga kwa pamoja. We have now the enemy, our enemy is our government (Dola) ingekuwa adui yetu ni Shein tungeshirikiana na Magufuli kumuondoa, lakini adui yetu ni Mfumo wa CCM na Dola kwa ujumla. Adui yetu ambae tunahitaji kupambana nae kikosi chake kinaongozwa na Magufuli,na wanajua kupigana vita vizuri,wanajua mikakati ya vita, wamejipanga kupigana vita, wanapanga vikosi vya kupima nguvu zetu zikoje, wanapanga vikosi vya uchokozi, mashambulizi ya uchokozi yamefanywa tayari mara mbili yakiongozwa na Jecha, hatujajibu hata moja kwa kuwa tunaipenda nchi yetu isiingie kwenye vita, hatujafikiri kupigana kwa kuwa tunaipenda nchi yetu na uhai wa watu wetu,tunafikiri mapenzi na nchi yetu yanaonekana kwa kuwa wapole, kuwa wakimya, kuwaachia CCM waendelee kututawala kibabe huku wakituibia rasilimali zetu.

HATUWEZI KUBAKI KUTOA KAULI ZA KULAANI TU VITENDO VYA CCM ZANZIBAR NA TUME YAKE (JECHA) HUKU WAKIENDELEA BILA HAYA KUFANIKISHA MAMBO YAO. TUKAOKOE MAISHA YA NDUGU ZETU ZANZIBAR, TUKAPIGANE KUSAKA HAKI YAO, TUSIANGALIE GHARAMA, TUANGALIE WAPI ILIPO IMANI YETU NA TUILINDE. WAASISI WA AFRIKA WANGEOGOPA GHARAMA BASI LEO TUSINGE KUWA HAPA, HAWA WACHACHE WASIURUDISHE NYUMA. LEO BURUNDI TUNAIONA ILIVYO, TUSIPOCHUKUA HATUA MAPEMA NASI TUTAFIKA HUKO. VIJANA TUNA NGUVU, TUTUMIE UJANA WETU KUTETEA TAIFA LETU TUTAPATA THAWABU MBELE ZA MUNGU.


MASONGA, EMMANUEL

TUITAFUTE HAKI YA ZANZIBAR

+255753170161
 
niko zenji mpaka sasa sisi tusio wakazi wa uku tu mashakani maana tunaonekana tu vibaraka wa ccm
 
Zanzibar hamtapigana wananchi kwa wananchi bali wananchi na vyombo vya dola, mwisho wa siku vyombo vy dola vitagoma kusikiliza wanasiasa na kuamua ya wananchi mf. Misri, Libya n.k

Maana kila polisi atapoteza ndugu yake na kila mwanajeshi pia, wote mtabaki kiwa na maumivu haki itachukua muda ila itapatikana tuu, damu imwagike damu isimwagike kuna watu watajibu
 
Back
Top Bottom