Tuamke Watanzania.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuamke Watanzania....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtoboasiri, Sep 21, 2011.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  ...nchi inaelekea kubaya.

  1. Kama unafaidika na utawala mbovu (hakuna anaebisha kuwa sasa hivi hakuna sekta hata moja ya umma inayofanya vizuri) wa serikali iliyopo madarakani basi ujue kuwa hicho "unachokifaidi" sasa hivi hakiwezi kuwa "sustainable". Mabadiliko ni LAZIMA YAJE hata kama unajidanganya kuwa itakuwa "Business As Usual". Pamoja na kukejeli maandamano kunakofanywa na wanamagamba, fahamuni kuwa watu wenye matumaini huwa na subira na unaweza ukawaelezea "ubaya wa fujo na maandamano" angalau wakakusikiliza hata kama hawakuamini. JK na genge lake wanachofanya sasa ni kuzalisha jeshi la watu wasiokuwa na ajira na mbumbumbu wa shule za kata wanaomaliza kidato cha nne huku hawajui kusoma na kuandika na hivyo kuja kukosa ajira (iwe za kujiajiri au kuajiriwa). Watu hawa hawatakuwa na matumaini na kuwatishia jela/risasi hakutasaidia siku hiyo (si bora awe jela atakakokuwa na uhakika wa chakula hata kama ni kibaya?)

  2. Waislamu wa kweli wakemeeni kwa nguvu zenu zote watu wenye ajenda zao za siri eti kuna "mfumo Kristo". Kumbukeni kuwa utawala huu mbovu unawadhulumu Watanzania walio wengi bila kujali dini au imani zao. Ni utawala mbovu ndio umetufikisha hapa na unazidi kutupeleka pabaya. Kumbukeni kuwa bei ghali za petroli, dizeli, sukari na bidhaa mbalimbali nyingine zinatuathiri sote. Kuna Waislamu maskini, kama walivyo wa dini nyingine na wasio na dini. ADUI YETU WA KWANZA KWA UJUMLA WETU NI CCM.

  AMKA MTANZANIA, KATAA KUTUMIWA KAMA KONDOM!
   
Loading...