VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Sisi wananchi tunataka kuwa katika upande mmoja.Upande wa kuamini au wa kutoamini. Lakini,tunaitegemea Serikali ituaminishe au itufanye tusiamini. Serikali ya chama chetu cha Mapinduzi inazunguka.Inajikanyaga.Inajiuma.Inazunguka mbuyu tu.Haina kauli moja.Haina usawa wa hoja na majibu. Inapishana kutoka huyu hadi yule. Kizungumkuti. Mchafukoge.
Ni kuhusu UDA. Wapo wanaosema mauzo yamefanyika. Mnunuzi ni Saimon Group inayomilikiwa na Robert Kisena. Wapo wanaosema kuwa mauzo hayakufanyika na Kisena na Kampuni yake hawana hata hisa moja. Wapo wanaosema kuwa suala hili lipo TAKUKURU kwakuwa kuna harufu ya rushwa. Wapo wanaosema Serikali itakuja na jibu moja.Wapo waliokana uwepo wa UDA katika Wizara zao. Tuamini au tusiamini?
Tuamini au tusiamini kuwa Serikali haijui kinachoendelea na kilichotokea UDA? Suala hili la UDA linaiaibisha Serikali na chama cha Mapinduzi.Kinaanika udahifu wa kiuongozi katika Taasisi na Idara za kiserikali zinazoshughulika na UDA katika maisha ya kila siku.
Wananchi wa Tanzania wanataka kujua.Kujua kuhusu UDA.Kujua kuhusu kilichotokea na kinachoendelea UDA. Kumjua mmiliki,mnunuzi,mwendeshaji na kadhalika. UDA haina ukubwa wowote wa kuogofya. Haina ukubwa wowote wa kuwafanya viongozi wetu wapishane katika kauli. Ishughulikiwe haraka.
Tunataka kuamini kuwa Serikali ni moja na inaweza.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Uandishi gani wa kitoto huo? una umri gani wewe? mwalimu gani alikufundisha uandishi wa kuweka nukta kila baada ya neno? watu kama wewe ndio wanafanya walimu wasipandishiwe mishahara.
Kaka hebu tujuze kilichotokea dodoma kwenye kikao cha chama.
MCHUNGUZI HURU halafu hujui hata uandishi!? Kijana,hufai kuwa CCM. Tunahitaji vijana tofauti na wewe.Uandishi gani wa kitoto huo? una umri gani wewe? mwalimu gani alikufundisha uandishi wa kuweka nukta kila baada ya neno? watu kama wewe ndio wanafanya walimu wasipandishiwe mishahara.
Subiri ripoti ya TAKUKURU
Kazi za CAG zinajulikana zinaonekana matunda yake...haya tuambie hiyo TAKUKURU imewahi kufanikiwa kupeleleza kesi ipi na kufanikiwa kuchukua hatua kwa maslahi mapana ya Taifa?...Wajinga ndio waliwao...
Kama kosa ni la kimantiki sawa tueleze ila kama ni tatizo la misspelling wewe ndiye una mawazo ya kitoto.Uandishi gani wa kitoto huo? una umri gani wewe? mwalimu gani alikufundisha uandishi wa kuweka nukta kila baada ya neno? watu kama wewe ndio wanafanya walimu wasipandishiwe mishahara.