Mwendabure
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 2,138
- 1,043
Salam WanaJamvi!
Kwa wale wakazi wa Jiji la Dar ni wazi kwa kila siku zinavyoenda ndivyo agizo la Mkuu wa Mkoa la kufanya usafi kila siku za jumamosi linavyozidi kupoteza mvuto. Ni wazi mwitikio wa wakazi wa jiji umekuwa mdogo mno ukilinganisha na hapo mwanzo agizo lilipotolewa. Na mtakubaliana na mimi kuwa ni aghalabu sana kila Jumamosi kuona watu kwa makundi wakifanya usafi kando ya barabara, Mitaro, Sokoni, viwanjani nk.
Kwasasa huku Uswazi maeneo mengi Jumamosi ni siku ya kufanya mazoezi (Jogging) kwa afya zetu. Marundo ya viloba vya takataka zinazoonekana kando ya barabara ni taka zinatoka Magengeni, majumbani (mabaki ya chakula nk) sio usafi wa jumla tena. Siku hii imegeuka siku ya kusogeza viloba vya taka kando ya barabara na Mazoezi.
Asante Mh. Mkuu wa Mkoa kwa kutuletea siku hii japo na sisi wauza Nyanya na Chapati tunaamka saa Nne kila Jumamosi kama nyie huko juu.
Wasalam..