Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,415
- 22,026
Nimefikiri sana juu ya hili, nikaona kwamba ni kama kulikuwa na kampeni fulani ya serikali kutaka kuonyesha inaweza kukamata mtu yeyote na kumweka ndani bila hata kujali nafasi yake katika jamii au sheria za nchi. Nahisi lengo lilikuwa kutia hofu wananchi, na suala la madawa ya kulevya lilitumika kama daraja tu, a means to an end.
Naona watu kama Mbowe, Gwijama na Manji na wasanii maarufu ilikuwa wawe kielelezo, ili mlalahoi kama wewe na mimi tuone kwamba kama hawa watu wanaweza kuwekwa ndani kirahisi namna hiyo, basi sie wananchi wa kawaida je?
Na tukumbuke kwamba tukio hili limeenda sambamba na Raisi Magufuli kuwakumbusha wakuu wa JWTZ na Polisi kwamba lazima watu wayaogope majeshi yao. Katumia neno kuheshimu - kwani watanzania hawawaheshimu Polisi na JWTZ? Heshima gani raisi anataka wananchi wawe nayo - woga?
Mie nadhani huu ni mkakati wa kutia hofu ndani ya wananchi ili tuwe taifa la kutodiriki kukosoa.