Tuambiane ukweli: Ni kweli Kuna Petrol station zenye mafuta masafi na zenye mafuta machafu.

Residue ndio inafanya mafuta yawe machafu.
Ni mabaki mabaki ya compunds baada ya mafuta kutuama sehemu moja muda mrefu.
 
Ni usafi wa zile tank, Kuna baadhi ya sheli wanatank moja tu kiasi kwamba mda wa kufanya usafi hawana, pia ni ngumu kwao kupoteza mda na hasara ya kufanya usafi tenk hilo maaana liko busy!

Kwahiyo mrundikano wa uchafu huwa mwingi kiasi kwamba hata mafuta yakiwekwa yanakuwa machafu.

NOTE; Epuka sana kujaza mafuta kwenye sheli hizo hususani pale tenker la mafuta linapokuwa punde limemimina mafuta!

USHAURI; kwakuwa ni ngumu kuzijua sheli zenye tenk moja maana yamefukiwa; Hivyo nakushauri mida mizuri ya kuweka mafuta ni alfajiri sana, au usiku mnene pale ambapo mafuta yanakuwa yametulia (decantation theory)
 
Ninavyojua mimi kuna baadhi ya gas station huweka maji kwenye mafuta, na kuna gas station nyengine unalipia laki 1 lakini wanaweka mafuta ya 70,000. Hapa hucheza na pump ya mafuta sijui hufanya vipi.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Mimi ninavyofahamu ni kwamba mafuta yote huagizwa pamoja, Sasa vipi nasikia Kuna sheli zinatoa mafuta masafi na yingine zinatoa mafuta machafu? kuna ukweli kuhusu jambo hili au ni maneno tu?
Zipo za wahuni japo ni chache, una kipindi mpaka msafara fulani uliwahi kuwekewa mafuta yakubumba, well zinaweza zikawa ni hadithi za elfu lela ulela ila kwenye wema na wajinga wapo pia
 
Petrol stations nyingi zinazomilikiwa na wazawa hawazingatii matakwa ya kusafisha matank kila baada ya kipindi fulani.Zoezi hili ni gharama na wanalikwepa tofauti na vituo vya mafuta vinavyomilikiwa na kampuni za kimataifa daima hufuata viwango bila kujali gharama zake.
 
Back
Top Bottom