Tuacheni udhalilishaji, imetosha sasa

Unamabadiliko makubwa sana hongera-kashfa zako tutahifadhi
 
Naona watu wa UKAWA, wanamshukia Shonza na CCM hali ya kuwa wao huwa wanafanya hayo, nao wanajifanya wamesahau kuwa walimuita EDO mwizi, fisadi, jizi, dhaifu, na mengine mengi. Leo wanaona ubaya ukweli kusemwa
 

Mimi sijui niizungumziaje hali halisi inayoendelea mitandaoni but kuhusu mama regina bana mh' unajua kila mtu either mtu mzima au kijana tunatabia zetu binafsi regarding maisha yetu ta kila siku kwa ujumla, watu tunao kaa nao, mambo tunayofanya nao, yanapelekea au yanachangia sana on how they react towards you, kma ni mtu wa utani basi utakuwa mtu wa matani kwa watu wako, mtu wa matusi basi hvyhvy, so nikizungumzia mama regina yes yule ni mama yetu, we have to respect her, NI MAMA na NANI KAMA MAMA''.. sasa yale mazingira aliyokuwa na watu aliyokuwa nao, maneno aliyokuwa akiyaongea,sishangai kwa kilicho mtokeo coz mazingira aliyokuwa yalipelekea yeye kutendewa kitendo kile'' na kitendo kile kilichomtokea ni cha aibu sana lakini kimeacha maswali mengi sna, je yule mtu ni nani? Mtu wake wa kariibu au ili mtuma tu kumnaniiino mama vle??.. Jibu ni sijuii.....

Pili tukiacha ya mama regina haya mengine ya mitandaoni mi naona ni hali ya siasa nchini,,naziona nisiasa tu nchini...Propaganda, kila mtu anataka mwenzake aonekane mbovu ili kwake iwe advantage, so ni siasa tu.

Siasa ni Siasa..your in it, play within it. OVAAA!!!..
 




Dhidi ya fisadi Lowasa na Genge hakuna mipaka, kila kitu kinaruhusiwa, maadili yote yanayojulikana yanaacha kutumika na hili hata Mungu analijua na amelikubali, hili nilifundishwa na Mh.Lema Mbunge wa (zamani) Arusha Mjini kwamba ni ,,Heshima kwa Mungu kumtukana na kumzomea fisadi kama Lowasa na Genge lake"


 
Last edited by a moderator:
Saa nyingine akili za chadema zinakurudia, safi sana dadaangu hata mimi sipendi tabia ya kudhalilisha wazazi, viongozi wetu etc. Maana utashangaa mtu anadiriki kumtukana hadi mkuu wa nchi!
 
Tukana tu na tukanwa tu mpaka kieleweke.Aliyeasisi matusi katika harakati hizi za uchaguzi atapata ijira wake siku isiyo na jina.MUNGU MKUBWA
 
Tusipoelemea upande wowote tutakuwa wawazi kuwa matusi yanatolewa na pande zote za vyama vyote vya siasa. Tukumbushane tu jinsi watu walivyomtukana Rais Kikwete matusi ya nguoni na hadharani wakati yupo Marekani anafanyiwa upasuaji wa tezi dume.

Jambo la msingi siasa za udhalilishaji hazifai, tuziache mara moja.
 

Matusi hayasemwi hadharani katika jamii yoyote, ila shida inakuja pale ambapo CCM wanatoa kauli basi zinakuwa matusi, ila watu wa UKAWA wakinena kauli zao si matusi. Cha msingi sisi wananchi amabao ndio tunatumiwa kama daraja tuwe makini na wanasiasa wote, sio wa CCM tu au wa UKAWA. Maana wanasiasa wote wa upinzani na chama tawalka hawaishi maisha ya ovyo, tutakaoumia ni sisi hivyo tuuache ushabiki i==
 
Kwasababu mwanamke mwenzako amefanyiwa hivyo ndo umekuja kukemea hapa?
Wakati Lowasa anadhalilishwa ulikuwa wapi?
CCM mmeanzisha hizi siasa. Anza kuwakemea Nape na wenzake.
Tumuunge mkono kwa hili alilolikemea. Kama hayo mengine si jukumu la J shonza pekee hata wewe haya unayoyasema umekemea lini humu jf? Wewe EL alivyodhalilishwa ulianzisha thread ya kukemea?
 
nafikiri aliopo sasa anatamani muda urudi nyuma asifanye alichofanya
 
eddo ni eddo mama Regina ni Regina kwa ufupi mama aheshimiwe!
 
Lile tukio lilikua limeandaliwa kwa makusudi ya kutengeneza picha za kuuza! Huyo kijana alipewa pesa toka CCM ni inasemekana hata kadi ya CHADEMA hana, Na niwaambie kwamba hata huyu Juliana Shonza naye inawezekana kabisa ameshiriki kuandaa hiyo video. Ukitaka kulifahamu hilo fuatilia utaona kwamba mtu wa kwanza kuituma hiyo picha kwenye mtandao ni kijana wa UVCCM. Juliana Shonza aache unafki huyu dada ana roho mbaya sana.
 
Lakini aliyemdhalilisha sio mwanachama wa ccm ni nyinyi wenyewe chadema, na wa kuanza kuzisambaza ni nyinyi wenyewe chadema;mama lowassa haambatani na ccm, kwanini lawana zije ccm? Ukweli ni kwamba kuna wanachadema ambao hawajafurahishwa na ujaji wa lowassa cdm
 
Nionavyo mimi ingekuwa vyema kulizungumzia hili kwenye vikao vyenu vya dharula badala ya kulileta huku kwenye umati wa watu na kutajana majina na kufanya watu wawe na shauku ya kujua ni hasa kilimtokea mama huyo.
 

Kitu ambacho nimegundua ndugu yangu sasa hivi hizi siasa zimegeuka ni sehemu ya kutokea kimaisha, hasa vijana wanapoona tukio lolote hasa la udhalilishaji wanalitumia kama sehemu ya mtaji. Sina hakika kama ni chuki dhidi ya Lowassa ndio mtu afanye hivyo bali ni tamaa ya fedha ndio imewafikisha vijana wengi kwenye eneo hili la kukiuka maadili. Na kwa bahati mbaya sana hao wenye kupenda siasa za kipuuzi ndio wenye pesa za kufadhili upuuzi huu wakidhani utawaongezea kura. Huyu mleta mada huenda amebadilika ama ni kujifanya mwema sina hakika na moja kati ya hayo lakini alikuwa ni kinara na hadi leo ni baadhi ya watu wenye kupenda kukashifu watu na kutoa maneno ya kejeli. Mfano halisi sio mara moja au mbili amekuwa akimuuta Slaa babu kwa maana ya dhihaka, na Mbowe zero kwa minajili ya kumshushia hadhi yake. Sasa leo anaposema siasa chafu sijui anamaanisha kabadilika ama anajutia yale aliyokuwa kinara wa kuyaeneza ama vipi.

CC: Juliana Shonza
 
wewe endelea kumaanisha utakavyo wewe kauli za siasa, kama una mzazi wa kike hauwezi kushabikia udhalilishaji huu.... tena inaonekana kabisa ni sexual harassment..... sasa kama una mama ungeelewa....
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…