Tuache visingizio katika soka


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,977
Likes
5,351
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,977 5,351 280
KATUNI%28131%29.jpg

Maoni ya katuni.Wiki iliyopita, klabu tatu zilizokuwa zikiiwakilisha Tanzania katika michuano mbalimbali ya Afrika zilitolewa kwa vipigo vya aibu. Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara walitolewa na FC St.Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa jumla ya magoli 4-2, wakifungwa 3-2 nyumbani na kisha kupokea kipigo cha goli 1-0 ugenini, kwenye Uwanja wa Stade Municipal de Lubumbashi, katika mji wa Lubumbashi nchini Kongo.
Mafunzo, wakishiriki michuano hiyohiyo ya Yanga baada ya kutwaa ubingwa wa Zanzibar msimu uliopita, walifungwa jumla ya magoli 6-1 na wapinzani wao, klabu ya The Gunners ya Zimbabwe. Awali, walikubali kipigo cha nyumbani cha magoli 2-1, kisha wakafungwa 4-0 ugenini Zimbabwe.
Miembeni pia haikufua dafu mbele ya wapinzani wao Petrojet ya Misri baada ya kuambulia sare ya 2-2 nyumbani kabla ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kufungwa magoli 2-0 ugenini.
Matokeo haya mabaya kwa klabu zetu, yanamaanisha kuwa sasa, tegemeo letu liko kwa Simba pekee, ambayo itaanzia raundi ya pili ya Michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya FC Lengthens ya Zimbabwe.
Aidha, tunaona kwamba matokeo hayo yanayouma ni sehemu ya mchezo. Lakini, tunachotaka kukumbushia ni visingizio visivyo na kichwa wala miguu vinavyotolewa na viongozi, wachezaji na hata walimu wa timu zetu mara baada ya vipigo.
Sisi, pengine na Watanzania walio wengi, hatufurahii maelezo yasiyokuwa ya kiufundi juu ya kuboronga kwa timu zetu.
Mathalan, tunakumbuka kuwa kabla ya kucheza na FC Lupopo nyumbani, Yanga haikuwa na maandalizi ya maana. Haikucheza mechi yoyote ya kirafiki ya kimataifa na taarifa zilidai kuwa hata wachezaji wake, baadhi walikuwa wakilalamikia mishahara yao siku chache kabla ya mechi hiyo. Mwishowe wakafungwa 3-2.
Hiyo haitoshi, siku chache kabla ya kurudiana na Lupopo, Yanga wakacheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya ZESCO ya Zambia kwa kutumia kikosi kisichozoeleka na kutoka sare ya 1-1.
Walipoenda ugenini Lubumbashi, haikushangaza kusikia kuwa wachezaji waliokuwa jukwaani kutazama wenzao wakijifua dhidi ya ZESCO wamefungwa tena 1-0 na wenyeji Lupopo, hivyo kutolewa mashindanoni.
Baada ya hapo, vichekesho vilifuatia baada ya kuzuka madai kuwa eti, Yanga walifungwa kwavile uwanja wa wenyeji wao (Lupopo) ulijaa tope.
Sisi tunaona kuwa kisingizo hiki hakikuwa na mashiko hata chembe, kwa kuzingatia kuwa wachezaji wa Lupopo hawakuwa samaki aina ya kambale ambao ni wazoefu wa kuishi kwenye matope. Kama tope ni kikwazo kwa Yanga, wenyeji bila shaka walikwazika pia.
Zaidi, tunaona ksiingizo cha Yanga ni kichekesho kwa sababu, kama walizoea kucheza kwenye viwanja vizuri, walipaswa kuwafunga magoli mengi wapinzani wao pindi walipokutana nao katika mechi ya kwanza -- kwenye uwanja wa kisasa wa Taifa ambao ubora wake uliwahi kusifiwa na nyota Didier Drogba wa klabu ya Chelsea ya England.
Kama ilivyokuwa Yanga, Mafunzo nao wametoa mpya kwa kudai walifungwa 4-0 ugenini na wapinzani wao The Gunners kwa sababu Zimbabwe kuna baridi kali.
Malezo haya. Ni muendelezo wa visingizio visivyo na mashiko, kwani mwerevu yeyote anaweza kujiuliza kuwa, kama hoja ni hali ya hewa, kwanini wao (Mafunzo) hawakushinda kwa idadi kama hiyo ya magoli walipocheza nyumbani na wapinzani wao?
Sisi tunaona kwamba visingizio kama hivi havina nafasi katika soka la sasa, ambalo hutawaliwa na mbinu kali za kisayansi.
Yanga, Mafunzo na klabu nyingine za soka zijikite kwenye maandalizi ya uhakika kama zinavyofanya klabu za FC St. Eloi Lupopo, Petrojet, The Gunners na klabu nyingine za wenzetu. Tuache visingizio.
CHANZO: NIPASHE
 
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Messages
10,225
Likes
884
Points
280
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined May 3, 2009
10,225 884 280
sisi bana km kungeanzishwa ligi ya kukaa vijiweni na kupiga domo kusifia wachezaji wetu wasio na viwango, nadhani vijiwe vya yanga na simba vingekutana fainali kila mwaka. sitasahau kile kichwa cha habari eti yanga sasa yapata winga teleza, kwenye mazoezi ukienda kuangalia huoni hata krosi moja ya huyo winga kwama na si teleza tena ah magazeti nayo!
 

Forum statistics

Threads 1,238,930
Members 476,277
Posts 29,337,199