Tuache uwongo Genocide ya Rwanda haikusababishwa na Media bali ni Utawala wa Kibabe na wa Kikabila.

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Ukisoma vizuri sana Kitabu Kilichoandikwa na Mwandishi Gerald Prunier chenye Title ya ' The Rwanda Crisis, History of a Genocide 1959 - 1994 ' utagundua kuwa ni asilimia ndogo mno ambapo kimahesabu inaweza kuwa ni 2% mauaji yale yalisababishwa na Vyombo vya Habari ( Media ) ila kwa 98% yale mauaji yalisababishwa sana na Uongozi wa Kibabe, Uonevu, Kiburi, Jeuri, Dharau na kubwa mno Ukabila wa kutukuka kutoka kwa Kiongozi ( Rais ) aliyekuwepo ambaye alipenda mno kuweka Watu wa Kabila lake tu la Kihutu katika nafasi za juu za Uongozi.

Nitoe tu RAI yangu kwangu nyie Viongozi mnaopenda kukurupuka kutoa references za matukio ambayo kimsingi hata hamna uhakika nayo kwani kwa kufanya hivi kunaweza kutufanya tuzidi kuwadharau na kuwapuuza japo kiukweli mna Elimu kubwa sana.

Kiongozi mzuri ni yule ambaye huwa ni makini na mara nyingi sana hupenda kujisomea maandiko au vitabu mbalimbali ili kujiongezea maarifa fulani lakini pia hata kumuwezesha kuweza kujenga Hoja nzuri na zenye mantiki mbele ya Watu ambao wanamuamini na siyo kutoa tu kauli za kukurupuka ambazo kimsingi yawezekana hata huna uhakika nazo.

Narudia kwa kusisitiza kuwa Genocide ya Rwanda kwa 98% ilisababishwa na Uongozi wa Kibabe, Uonevu, Kiburi, Jeuri, Dharau na kubwa kuliko Ukabila wa kutukuka ambapo Kiongozi aliyekuwepo alipenda mno kuwaweka Watu wa Kabila lake la Kihutu katika nafasi Nyeti za Uongozi kama Ukuu wa Usalama, Jaji Mkuu, Mkuu wa Kitengo chake cha Usalama ( Rwanda wanakiita PPU sijui hapa Tanzania wanakiitaje ), Mkuu wa Majeshi, Bosi wa RRA ( hapa tunaita TRA ) na nyinginezo ila mauaji hayo yalichochewa kwa kiasi cha 2% tu na Vyombo vya Habari ( Media ).

Bahati nzuri ni kwamba hiki Kitabu kinapatikana karibu katika Libraries nyingi duniani na hata katika Mitandao ( ambayo hata hivyo tumeambiwa ni ya hovyo hovyo ) hivyo sometimes tunaweza tukapunguza safari zetu zisizo na maana za Kushtukiza katika Taasisi fulani fulani ili kupata Kiki na tukautumia huo muda kujisomea kidogo kupata uelewa ili siku zingine tukikutana mikutanoni mkiwa mnazungumza tuweze kuamini kuwa hata Shahada zenu za Uzamivu ( PhD ) mlistahili kuwa nazo.

Najua message sent and delivered!!!!!!!

Nawasilisha.
 
Ndg zangu,UONGO ukisemwa na kuachwa bila kukanushwa hugeuka kuwa kweli.

Hivi karibuni,wapo baadhi ya viongozi wanaohubili na kuaminisha watu eti mauaji ya KIMBALI huko Rwanda,yalisababishwa na waandishi wa habari jambo ambalo si kweli!Mauji hayo yalisababishwa na wafanya-SIASA WALIOLEWA NA MADARAKA,WALIOPENDELEA ama NDUGU au WATU WA JAMII YA KWAO.Walihisi wao ni MIUNGU watu!

Ulevi wa MADARAKA ni jambo baya sana!Hao watawala hawakutaka tena kushauliwa ktk lolote!Aliyekuwa upande kinzani walihakikisha wanampoteza.Walibebana wao kwa wao(WAHUTU).Mnyarwandwa wa jamii ya Kihutu,alikuwa haguswi,iwe kwa kufanya makosa yaliyo ya wazi au vinginevyo;alikingiwa kifua na utawala uliopata kuwa DHALIMU na ULIOKUWA HAUSHAULIKI!Hii ni sawa na,kwa mfano;kabila la WASUKUMA huko Tz watawale na hata wakifanya makosa ya wazi,wasiguswe(mfano).

Ndivyo ilivyokuwa.Watu walivumilia na mwisho wa siku,mauaji yalianza.

Kwa hiyo,si kweli mauji yale yaliletelezwa na salamu za waandishi.Bali yaliletelezwa na watawala MADHALIMU na yaliyopata kuwa HAYASHAULIKI KTK LOLOTE!

Jumapili njema.
 
Ukisoma vizuri sana Kitabu Kilichoandikwa na Mwandishi Gerald Prunier chenye Title ya ' The Rwanda Crisis, History of a Genocide 1959 - 1994 ' utagundua kuwa ni asilimia ndogo mno ambapo kimahesabu inaweza kuwa ni 2% mauaji yale yalisababishwa na Vyombo vya Habari ( Media ) ila kwa 98% yale mauaji yalisababishwa sana na Uongozi wa Kibabe, Uonevu, Kiburi, Jeuri, Dharau na kubwa mno Ukabila wa kutukuka kutoka kwa Kiongozi ( Rais ) aliyekuwepo ambaye alipenda mno kuweka Watu wa Kabila lake tu la Kihutu katika nafasi za juu za Uongozi.

Nitoe tu RAI yangu kwangu nyie Viongozi mnaopenda kukurupuka kutoa references za matukio ambayo kimsingi hata hamna uhakika nayo kwani kwa kufanya hivi kunaweza kutufanya tuzidi kuwadharau na kuwapuuza japo kiukweli mna Elimu kubwa sana.

Kiongozi mzuri ni yule ambaye huwa ni makini na mara nyingi sana hupenda kujisomea maandiko au vitabu mbalimbali ili kujiongezea maarifa fulani lakini pia hata kumuwezesha kuweza kujenga Hoja nzuri na zenye mantiki mbele ya Watu ambao wanamuamini na siyo kutoa tu kauli za kukurupuka ambazo kimsingi yawezekana hata huna uhakika nazo.

Narudia kwa kusisitiza kuwa Genocide ya Rwanda kwa 98% ilisababishwa na Uongozi wa Kibabe, Uonevu, Kiburi, Jeuri, Dharau na kubwa kuliko Ukabila wa kutukuka ambapo Kiongozi aliyekuwepo alipenda mno kuwaweka Watu wa Kabila lake la Kihutu katika nafasi Nyeti za Uongozi kama Ukuu wa Usalama, Jaji Mkuu, Mkuu wa Kitengo chake cha Usalama ( Rwanda wanakiita PPU sijui hapa Tanzania wanakiitaje ), Mkuu wa Majeshi, Bosi wa RRA ( hapa tunaita TRA ) na nyinginezo ila mauaji hayo yalichochewa kwa kiasi cha 2% tu na Vyombo vya Habari ( Media ).

Bahati nzuri ni kwamba hiki Kitabu kinapatikana karibu katika Libraries nyingi duniani na hata katika Mitandao ( ambayo hata hivyo tumeambiwa ni ya hovyo hovyo ) hivyo sometimes tunaweza tukapunguza safari zetu zisizo na maana za Kushtukiza katika Taasisi fulani fulani ili kupata Kiki na tukautumia huo muda kujisomea kidogo kupata uelewa ili siku zingine tukikutana mikutanoni mkiwa mnazungumza tuweze kuamini kuwa hata Shahada zenu za Uzamivu ( PhD ) mlistahili kuwa nazo.

Najua message sent and delivered!!!!!!!

Nawasilisha.

Hivi mtu wa ccm na wachadema wakiandika kitabu kuhusiana na Maendeleo yanayotokea Tanzania kitakuwa sawa?
 
Media "ilitumika kuchochea" mauaji sio "kuanzisha" mauaji. Mauaji yanafanyika kwa silaha sio kwa kuhabarisha. Kuna tofauti kubwa kati ya "kuanzisha" na "kuchochea/kuhamasisha" mauaji.
 
... Hujasaidia kitu, weka hicho unachokijua.

Safi sana Mkuu nataka aseme hicho anachokijua halafu nimwelekeze kama ana hicho Kitabu hapo alipo sasa hivi afungue page ipi ili nimuumbue vizuri kusudi siku nyingine asiwe anakurupuka pindi Wanamume tunapoweka uzi humu JF? Ukiona hadi natiririka na uzi humu jua nimejikoki vizuri hasa Kidata. Kwanza sidhani hata kama Kitabu chenye ameshakisoma pages zake 5 tu achilia mbali pages zake jumla 355.
 
Media "ilitumika kuchochea" mauaji sio "kuanzisha" mauaji. Mauaji yanafanyika kwa silaha sio kwa kuhabarisha. Kuna tofauti kubwa kati ya "kuanzisha" na "kuchochea/kuhamasisha" mauaji.

Kwahiyo hapa unanipasha Mimi GENTAMYCINE au yule aliyetuaminisha majuzi pande zile za Magogoni tena huku akijigamba?
 
Mkuu Ulikuwa Wapi? Ni kitambo Sasa Umepotea Comrei.

Nakupongeza kwa kuja na kabandiko kako ka kutoa Angalizo kwa Viongozi wetu.

Lakini napenda ni kukumbushe kwamba sisi tulio ona Mbali tuliwambia tulipokuwa tanaelekea kwenye Uchaguzi 2015

kwamba Tanzania inamwitaji Kiongozi Mwenye Vision.

Sasa nadhani mmeanza kupata Akili, tatizo la maendeleo ya Tanzania halikuwa Ufisadi Bali ni Mipango Mizuri ya Uongozi na Utendaji.

Japo wengi tuliaminishwa kwamba tatizo la tanzania kutokuendelea ni Ufisadi lakini sasa tunagundua kwamba tatizo ni Mipango na Utekelezaji wa Serikali usiokuwa na Dira au Mipango Madhubuti.

Niaibu kuona kanchi kadogo kama Rwanda kalichotoka kwenye Vita juzitu 94 kameshatuacha kwa mbali sana kwa maendeleo!!!!!

Halafu sisi tunabaki kutimuana timuana visasi gilba na maneno mengi badala ya kuweka mipango mizuri ya maendeleo tunabaki kutumbuana!

Mtashtukia 2020 imefika tunakwenda kwenye Majukwaa na kuanza kutoa sababu lukuki kwa wananchi na kupiga pushap jukwaani ili kutafuta huruma za wananchi?

Sikweli kwamba Rais Aliyepo madarakani sasa hivi hajafanya mazuri.

Amefanya tena Mengitu. Ila wananchi tunataka tuone Maendeleo kwa wananchi na siyo kama mwalimu nyerere alivyotuambia kwamba maendeleo siyo Vitu bali maendeleo yanatakiwa yaonekene kwa watu.

Ikiwa mtanzania kwa sasa hata mlo 1 haupati tena! Ukija kumwambia umejenga Mabarabara, umepunguza wafanyakazi hewa na kutumbua Majipu, hunakushanya matrilioni ya kodi, huku yeye haoni unafuu wa maisha hawezi kukuelewa kabisa.

Tujifunze katika utawala wa mzee mkapa yeye aliwezaje kupandisha uchumi wa nchi na kudhibiti mifumuko ya Bei?

Sote tunakumbuka kulikua na urahisi wa bidhaa muhimu kama vyakula, usafiri, ujenzi na Nk.

Sasa wananchi wanajiuliza Awamu hii vp? Kama imeweza Kudhibiti mianya yote na kukusanya matrilioni kwa mwezi mbona hawaoni unafuu wa maisha?

Nahapa wananchi wakihoji viongozi wasiwaone wananchi siyo wazalendo kwa kuhoji kulikoni?

Uzalendo ni pamoja na kuhoji hasa pale tunapoona mambo hayaendi sawa.

Nimalizie kwa kusema, kuchagua ni uchaguzi wa kila mwananchi ila maumivu ya kuchagua vibaya Au Vizuri yanatugusa Wote.
 
Hiyo ni story ya kutungwa na uhalisia si huo.
Hii sio hadithi" story" bali ni ripoti ilioandikwa na wabobezi wa TASNIA HIYO YA HABARI! na kuwasilishwa kwenye Tume ya Haki za binadamu katika kitengo kinachohusika na ufumbuzi wa migogoro.
 
Hii sio hadithi" story" bali ni ripoti ilioandikwa na wabobezi wa TASNIA HIYO YA HABARI! na kuwasilishwa kwenye Tume ya Haki za binadamu katika kitengo kinachohusika na ufumbuzi wa migogoro.
Hao unaowaita WABOBEZI,wapo ulaya huko.Mm nipo Rwamagana,Rwanda.Jawabu unalo....
 
Vyombo vya habari ndivyo vilivyopiga mwangwi mkuu wa chuki za ukabila na kusababisha kufumuka hiyo unayoiita genocide.
Itafute na uiangalie documentary ama tuseme clip huko you tube inaitwa Hotel Rwanda.
Hapo utaona jinsi vyombo vya habari, hasa radio zilivyotumika kuhamasisha mauaji hayo.
 
Hivi mtu wa ccm na wachadema wakiandika kitabu kuhusiana na Maendeleo yanayotokea Tanzania kitakuwa sawa?

Kwani huyo Mwandishi Gerald Prunier ni Mnyarwanda? Kwanza samahani Mkuu usitake tuchoshane mapema yote hii naomba nikuulize hivi hicho Kitabu achilia mbali tu Kukisoma je unakijua au umeshawahi tu kukibahatisha kukiona kwa hiyo Mijicho yako mikubwa kama taa za Meli?
 
Back
Top Bottom