Tuache ushamba tuwe wavumilivu, siasa za kushambuliana majukwaani zilikuwepo tangu 1995

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
Mimi nawashangaa sana hawa wanafiki wanaojipendekeza eti ooh Tundu Lissu aache kuongea maneno makali dhidi ya Mukulu.
Hizi ni siasa, ukiambiwa kitu kwa hoja jibu kwa hoja na siyo kuanza kupiga mayowe hovyo hovyo kama mtoto mdogo.

Wahenga tuliookuwepo tangu 1995 wakati uchaguzi kupitia mfumo wa vyama vingi unaanza tuliona Mrema alilvyomshambulia sana Mkapa majukwaani, tuliona Mrema alivyoisulubu CCM majukwani lakini hatukuona Mwinyi akituma polisi wamshughulikie pamoja na ugeni wake wa siasa za vyama vingi. Zilikuwepo kurupushani za hapa na pale lakini hazikuzidi kama sasa. Huu wa sasa ni ushamba wa kisiasa hasa kwa CCM. Dr MAGUFULI ni mgombea kwa sasa kama walivyo wagombea wengine, kuzuia au kuchukia asisemwe majukwaani kwa sababu ya watu kutoelewa siasa.

Mwaka 2010-2015, Dr Slaa alimshambulia sana JK akampa majina ya kila aina, lakini kwakua CCM ya wakati huo ilikua inaelewa nini maana ya siasa za ushindani, walijibu hoja kwa hoja hatukuona polisi wakitumika hivyo kama ilivyo sasa. 2015 Tuliona LOWASSA akitumwa na jukwaani matusi ya nguoni lakini wafuasi wake nao walijibu kwa hoja hatukuwahi kuona watu wakinuna kama ilivyo hivi sasa. Huu sasa ni ushamba wa siasa tumejazana chuki na visasi.
 
Back
Top Bottom