Tuache siasa katika elimu ni hatari.

Mkulia

JF-Expert Member
Apr 26, 2012
375
95
Imekuwa ni jambo la kawaida kwa nchi hii kuingiza siasa hata katika maeneo ambayo siasa haitakiwi kabisa. Hivi sasa ni kawida kukuta taaluma ya utabibu,kilimo na hata elimu ikiendeshwa kisiasa zaidi. Miaka ya hivi karibuni taaluma ya ualimu pia umevamiwa na wanasiasa na kuendeshwa kisiasa zaidi. Kwa mfano katika shule za msingi kuna mafunzo ambayo huendeshwa na chuo kikuu huria ambapo mwalimu wa daraja la lllA anaweza kujiendeleza na kupata Stashahada,Shahada na shahada ya uzamili kwa kutumia cheti chake cha ualimu daraja la llla pasipo hata na kuwa na cheti cha kidato cha VI. Pia mwalimu huyo akifaulu mafunzo yake mathalani ya Shahada wanam-regard sawa sawa na yule aliyehitimu kidato cha lV,cha VI na kwenda chuo kikuu akasoma BAED/BED kwa miaka mitatu au zaidi. Hakika huku ni kudhalilisha taaluma ya ualimu na elimu yenyewe. TUJADILI.
 
Kwa serikali hii ya wezi na wanyang'anyi,usitegemee hata siku moja kuona mabadiliko katika elimu,maana wanazingatia ulajitu.tanzania ya jana ilibarikiwa kuliko ya leo.
 
Back
Top Bottom