Tuache porojo tuje kwenye matendo

Tuache porojo tuje kwenye matendo

Kiwalani finest

Senior Member
Joined
Jul 6, 2024
Posts
116
Reaction score
85
Tuache porojo tuje kwenye matendo hatua zinazochukuliwa kwa mafukara na watumishi wa umma
hatua hizo zichukuliwe ndani ya ccm ili kuondoa mionekano ya kiubaguzi na kiupendeleo

Nakumbuka Tarehe 25/04/2025 akilihutubia Taifa kuelekea kwenye maadhimisho ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema:


“Niseme kuwa hakuna (mtu awaye yeyote yule) aliye juu ya Sheria.
Na wote tunatakiwa kuendesha shughuli zetu za kisiasa tukizingatia kuwa Amani (haki za watu) na usalama wa nchi ndiyo kipaumbele cha kwanza.”
(Mwisho wa kunukuu)

Shida zetu zinatatuliwa na Viongozi wacha Mungu walioapa:
Kuhifadhi, Kulinda na Kutetea Katiba na Sheria za nchi.
Ndani ya Katiba na Sheria za kimfumo, Viongozi wanatakiwa kuwa:


  • Wanyenyekevu
  • Kutokuwa wabaguzi
  • Kutokuwa wapendeleaji
  • Kutokuwa na viburi vya kusema: “Hata nikivunja taratibu, Watanzania watanifanya nini?!”

Kuyashiriki haya huku ndiko kunaitwa kupuuza Maandiko Matakatifu na kupuuza maandiko ya kimfumo.


Padre Charles Kitima
Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Nakumbuka Tarehe 26/04/2025 alisema:


“(Miaka ya nyuma) hatukuwahi kuwa na upuuzi wa namna hii unaofanywa sasa hivi.
Huu ni upuuzi kwa sababu watu wachache wanataka kuonyesha kwamba kwa sababu tumetoka kwenye mfumo ambao wananchi wanapenda sana kuheshimu viongozi wao,
na wanajua wananchi hawawezi kuwafanya lolote.
Na Watanzania si watu wa vurugu.
Ndiyo maana wale wenye kuamua wanafanya (chochote) wanachotaka wakijua hawatawajibika.”
(Mwisho wa kunukuu)

Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi
Katibu Mkuu CCM Taifa – Akiwa Rorya
Nakumbuka Tarehe 25/04/2025 alisema:


“Suala la kukumbushana kuhusu kuchunga kauli zetu na matendo yetu (ili) yaendelee kujenga umoja wa nchi yetu, lazima tuendelee kukumbushana (Watanzania) wote.”
(Mwisho wa kunukuu)

Kiongozi wa CCM lazima awe mfano bora, kwanza kwa kuzingatia kuwa CCM ndiyo iliyounda Serikali na ndiyo inayoisimamia Serikali.
Uadilifu na uaminifu lazima uanzie CCM kwanza kabla ya kunyoosha kidole kwa Serikali.
CCM lazima ijue vidole vitatu vya kiganja kilichonyoosha kidole vinamuelekea CCM.


Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi
Katibu Mkuu wa CCM Taifa – Akiwa Rorya
Nakumbuka Tarehe 25/04/2025 alisema:


“Sisi chama chetu lazima kiwe chama cha (kutolewa) mfano.”
(Mwisho wa kunukuu)

Mheshimiwa Wakili Jasiri na Msomi Peter Madeleka
Ex-Police Officer
Nakumbuka Tarehe 24/04/2025 alisema:


“Moja kati ya masharti ya chama cha siasa ni kuhakikisha kinafuata sheria za nchi ili kisifutwe.
Kikienda kinyume na hapo kikaanza kwenda kwa kuitikia matukio yanayotokea, maana yake ni kwamba kinakiuka zile kanuni za kukisajili chama,
kitafutwa, na kikishafutwa hutapata nafasi tena ya kukiita kwamba hiki ni chama.”
(Mwisho wa kunukuu)

Shekhe Kabeke
Shekhe anayemuwakilisha Mufti wa Tanzania kwa Mkoa wa Mwanza
Nakumbuka Tarehe 22/04/2025 alisema:


“Sisi viongozi wa dini hatutakiwi kuwa na upande (tunaouelemea zaidi ya kuisema haki).
Sisi tunatakiwa kusimama katikati na tuseme yaliyo ya kweli.
Sisi tunapaswa kusimama katikati, kushauri na kuwaombea.”
(Mwisho wa kunukuu)

Kiongozi anayepuuza kiapo alichoapa kwa Mwenyezi Mungu na kisha kuishi akikiuka maandiko ya kimfumo, lazima tupaze sauti atoke,
kwani kiongozi anayepuuza Maandiko Matakatifu huwa ni mnafiki.
Na mtu mnafiki ana dalili tatu.
Lakini pia mnafiki huwa ana ukafiri wa viwango vya PhD.


Lazima tuseme sana.
Tusikae kimya.
Tukinyamaza haitusaidii lolote.
Lazima tuseme.


Nakumbuka Tarehe 26/04/2025
Padre Dkt. Charles Kitima

Katibu Mtendaji Baraza la Maaskofu Katoliki wa Tanzania
Akifanya mahojiano na DW idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani alisema:


“Tusipoonyana mapema tutafika mahali hakuna atakayefurahia, na wote tutateseka.”
(Mwisho wa kunukuu)

Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Nakumbuka Tarehe 25/04/2025 alisema:


“Muungano wetu unaendelea kuzingatia misingi ya Utawala Bora katika nyanja mbalimbali,
ikiwemo Utawala wa Sheria, Haki za Binadamu, Uwazi, Uwajibikaji na Maridhiano.”
(Mwisho wa kunukuu)

Nikashtuka huko ndotoni nilipokuwa naota,
na nikabaini nilisinzia nikiwa sijakula – njaa ilikuwa inaniletea ndoto za ajabu.
Nikaamka.




Kidumu Chama cha Mapinduzi
Mathias Mugerwa Kahinga
 
Back
Top Bottom