Tuache mazoea, dunia ya sasa imebadilika mno

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,108
[h=2]
Edmfungwa.jpg

Maoni ya Katuni


Akiwa mgeni rasmi katika hafla ya kutunuku tuzo kwa waandishi bora katika fani mbalimbali (EJAT) mwaka juzi, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi,

ambaye anatajwa kama baba wa demokrasia nchini kwa kuasisi na kusimamia mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini hasa kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi na kuruhusu kutamalaki kwa vyombo huru vya

habari, aligusia jinsi fursa nzuri zinazotolewa katika jamii zinavyotumiwa pia na baadhi ya watu kupenyeza mambo yasiyofaa kwa maslahi yao binafsi.

Mzee Mwinyi alisema wakati serikali yake ilifungua milango ya kiuchumi kwa kuruhusu soko huria katika kuendesha uchumi kila kitu kikiwa ni ruksa kufanywa tofauti na mfumo hodhi wa kidola ambao kila kitu

kilikuwa mikononi mwa dola, wapo watu waliotumia mwanya huo kutenda mambo yasiyofaa.

Alisema “wakati milango ya kiuchumi ilipofunguliwa kuna majongoo na tandu walipitia dirishani kuchafua hali hiyo” kwa maana hiyo ni wajibu wa vyombo vya habari na jamii kushirikiana kufagia uchafu huo ili nia njema ya kufungua milango hiyo itimie kwa jamii.

Kila tunapotazama nyuma na kuitafakari kauli ya Mzee Mwinyi leo hii, tunapata picha halisi ya mambo yanayotokea miongoni mwa jamii kila uchao. Wapo watu wengi ambao ama kwa makusudi au kwa kutokujua tu au kupuuza tu sheria, taratibu na kanuni, wametumia fursa ya kulegezwa kwa masharti ya kiuchumi katika sekta mbalimbali na kuendesha mambo kama watakavyo wao.

Kuna mengi yameshuhudiwa, haya ni kuanzia kuagiza bidhaa feki, zenye viwango duni, kuanzisha taasisi za kutoa huduma za jamii kama afya na elimu kadhalika bila kuzingatia kanuni. Kumekuwa na utitiri wa shule ambazo hazina usajili, vituo au hospitali ambazo hakika hazina hata chembe ya sifa ya kutoa huduma husika kwa jamii. Taasisi hizi

siyo tu kwamba zimegharimu rasilimali nyingi wananchi, bali pia zimesababisha madhara makubwa.
Mathalan, jana gazeti hili katika ukurasa wake wa pili liliandika habari iliyobeba kichwa cha habari kisemacho “Nacte yasema Agape haina sifa za kutoa stashahada” ikinukuu Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi juu ya hadhi ya chuo tajwa

kuwa hakina ithibati ya kutoa mafunzo ya ngazi ya stashahada.
Wenye chuo nao wamesema kuwa wana makubaliano na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) katika kutoa mafunzo hayo, hivyo kuwa na haki ya kuendesha mafunzo kwa wanafunzi wa ngazi hiyo. Hili nalo linapingwa na Nacte kwa sababu taratibu za kuandikisha chuo kutoa mafuzo hayo ni lazima yapitie kwao na siyo makubaliano ya kisheria na chuo kingine.

Tunajua bado kuna mvutano baina ya Agape na Nacte katika suala hili, siyo wajibu wetu kusema ni nani yuko sahihi au kinyume chake, lakini itoshe tu kusema kuwa katika mvutano wote huu mwisho wa yote wapo watakaoumia.
Tumesema hapo juu kwamba fursa zinazoanzishwa nchini ni vema zikatumiwa vizuri, kwamba anayetaka kuanzisha

taasisi kwa ajili ya kutoa huduma yoyote ile ni vema akatimiza masharti yote yanaotakiwa ili asije kuwa kikwazo kwa wananchi wanaotumia huduma yake wakiamini kwamba kila kitu kiko sawa.
Kadhalika, tunaamini Nacte pia wanapashwa kuwa makini katika utekelezaji wa kazi zake, wawe na uwezo wa kutembelea maendeo mengi nchini kokote kulikoanzishwa taasisi kama hizi, ili kuhakikisha kwamba hakuna watu ama

kwa kujua au kwa kutokujua wanatumia fursa hizo kuwakamua wananchi bila wenyewe kupata hicho walichokusudia katika huduma hizo.

La msingi zaidi, ni jambo la kustaajabisha sana kwamba wapo wazazi au wananchi kwa ujumla wao wanakuwa na ujasiri wa kuwaandikisha watoto wao katika taasisi ambazo hawana uhakika kama zina sifa za kutoa mafunzo yanayosakwa humo. Hili ni jambo la kushangaza, kuumiza na kwa kweli kuamsha maswali mengi juu ya uelewa wa watu wetu kama taifa.

Hakuna kitu kigumu kutafuta kama fedha, watu hutoka jasho ili wapate fedha kidogo sana, hujifunga mkanda na kujibana sana katika kuzitumia fedha hizo, wengi hujifunga kweli kweli ili kumudu ada za shule na vyuo kwa watoto wao; katika mazingira ya namna hii inakuwa ni vigumu kuelewa inakuwaje pamoja na shida zote hizi mzazi huamua tu

kulipa fedha kwenye taasisi ambayo hana uhakika ina sifa na hadhi gani katika kutoa mafunzo husika?
Tunafikiri kwamba pamoja na Nacte kuwa na wajibu wa kusajili taasisi hizi, pia ni wajibu wa mzazi mmoja mmoja

kujibidiisha kwa njia mbalimbali kuzitambua na kuzielewa taasisi wanazotarajia kupeleka watoto wao; ni vema kufanya hivyo kwa sababu mwisho wa yote watakaoumia ni wao na watoto wao.
Tuache kufanya mambo kwa mazoea dunia ya sasa imebadilika sana, kila mahali majongoo yanajipenyeza; tuwe makini.



CHANZO: NIPASHE


[/h]
 
I concur with the article. Kama jamii inabidi tujitahidi kuwa na maadili na kuacha uhuni na short cuts. Tunaumiza jamii yetu wenyewe.
 
Back
Top Bottom