Tuache kulalama, tutoe majibu

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,875
Kumekuwepo na kurushiana maneno baina ya watu humu JF kuhusu suala la mchanga. Watu wamechukulia suala hili kivyama zaidi kuliko kitaifa. Leo namba tupate maoni ya wana JF humu kuhusu maswali haya machache yanayoweza kutupa dira ya kushughulikia tatizo lenyewe. Kumbuka kama lengo la mh. Rais litafanikiwa litakuwa na tija kwetu sote na kama litafeli pia ni hasara kwetu sote kwahiyo tuache itikadi tujibu kama wazalendo.

1. JE ACCACIA WANATUIBIA KWENYE MIKATABA AU NJE YA MIKATABA?.....
(a) Ndiyo
(b) Hapana
(c) Sijui

2. UNADHANI NI NJIA GANI INGEFAA KUPATA SULUHISHO LA SISI KUIBIWA?
(a) Kuzuia michanga kwenda kuchenjuliwa nje na kujenga mitambo hapa nchini
(b) Kuacha michanga iendelee kusafirishwa na kushughulikia mikataba kwanza
(c) Kupiga marufuku kusafirisha mchanga huku tukishughulikia kujua uhakika wa kinachosafirishwa
(d) Sijui

3. UNGEKUWA WEWE NI MH RAIS UNGEANZA NA LIPI KATIKA HUU MGOGORO?
(a) Kusitisha usafirishaji ili kupata ukweli kwanza
(b) kuacha mchanga uendelee kusafirishwa huku ukitafuta ukweli
(c) Kupitia mikataba kwanza huku michanga ikiendelea kusafirishwa
(d) Sijui

4. JE TUNAIBIWA KWENYE NINI HASWA?
(a) Michanga
(b) Madini yote
(c) Yote kwa pamoja
(d) Sijui

TOA USHAURI WAKO KWA RAIS WETU KWA NAMNA GANI UNAONA SWALA HILI LISHUGHULIKIWE
 
Wewe mwenyewe umekuja kulalama hapa wala hujatoa ushauri
 
Back
Top Bottom