Tuache kufukua makaburi!

The Priest

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
1,029
256
Waziri wa Muungano, Mhe. Samia Hassan Suluhu, leo jioni wakati akifanya majumuisho ya matumizi ofisi ya makamu wa Rais, mazingira na Muungano, amesema kuwa tuache kufukua mambo ya Muungano na jinsi ilivyokuwa, kwani hata mtoto hakosi kasoro.

Hivyo tuulee muungano wetu mzuri na mchanga, kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho..

source.TBC1 Bunge jioni.
 
Hata mimi nimemuona,kwa tabia hii ya viongozi wetu muungano ni bomu linalosubiri muda ufike lilipuke ngoja tuone wazenji watasemaje
 
Tunaona magamba na waliotumwana magamba kwenye luninga wakiwa bungeni, jinsi wanavyotetea maslahi ya chama na siyo maslahi ya Taifa. Tunawasubiri kwenye kona ambapo watakuja juta, wataona hasira za umma zinawaangukia bila huruma.
 
Yaani nimemshangaa sana yule mama,watz hatuujui Muungano nao wanaona kama kutaka kujua,ni kufukua makaburi..
 
Back
Top Bottom