Tuachane na kuvaa nguo za Chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuachane na kuvaa nguo za Chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by pmganga, Jul 24, 2010.

 1. p

  pmganga New Member

  #1
  Jul 24, 2010
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kibinafsi napata kichefuchefu ninapoona ushabiki wa vyama unaendana na kuvaaa nguo zenye rangi ya bendera za vyama.. Jamani hivi kasumba zimepitwa na wakati. hata hao wachina wa enzi za Mao Tsetung wanavaa suti wakati wa mikutano yao na hata kampeni za uchaguzi. Naomba mtu yeyote atupe majina ya nchi ambazo zinaushabiki huu katika ngazi ya kitaifa. Tuache hizi.. ni uozo katika kizazi hiki kujivisha magwanda ya rangi za chama. CCM ndo kabisa wanapotosha jamiii. Mimi nimetembea sana nchi za wenzetu nasijaona haya. Kwa kweli mtindo huu hauna maana yoyote kwa maslahi ya nchi. Vaaa unavyo vaaa ila kirasmi pembeni peperusha bendera ya chama chako.
   
 2. telele

  telele Member

  #2
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe unataka kila kitu tuige nchi zingine? hatuwezi kuwa na mambo yetu tuu ambayo siyo lazima na nchi zingine ziwe nayo? acha kasumba za kuigaiga na kujiringanisha na nchi za wenzetu. wacha watu wajinafasi. kwani inakupunguzia nini au kukuongezea nini? acha roho na mioyo ya watanzania ifanye ile kitu roho inapenda, awe wa CHADEMA au wa CCM au wa TLP wache wavae. au nyie CCJ (eti now imekuwa CCK) hamna sare nini? POLENI
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni mwelekeo wa utawala wa kidikteta -- kama vile wanachama wa chama cha Nazi wakati wa Hitler -- hususan wale makada wake waliokuwa wakiitwa "Brown Shirts." Someni Historia. CCM inaipeleka nchi hii pabaya sana.
   
Loading...