TTCL na ZANTEL 3G UTUMBO MTUPU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TTCL na ZANTEL 3G UTUMBO MTUPU

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by mpingauonevu, Jun 22, 2012.

 1. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 617
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Wana JF
  Baada ya kuona matangazo ya Banjuka na Nduki ya TTCL Broadband Niliamua kujiingiza kama mwanachama mpya. Niliyoyakuta ni Wizi Mtupu! Ndani ya wiki nilitumia 10,000! kila nikiwapigia hamna msaada wala nini yaani customercare ya hovyo kabisa! Ninaposema wezi namaanisha maana kama unatangaza tofauti na unachotoa huo si ni ujambazi? NAOMBA TUME YA USHINDANI IWAFUATILIE HAWA MAJIZI!

  Nikahamia ZANTEL uuwii kumbe wote watoto wa baba mmoja. Can u imagine unaingia kwenye website ya Zantel halafu hakuna imformations za 3G Moderm? Fikiria kununua bundle mpaka utumie simu ya mkononi!
  KASHEHE YA MWISHO TAFUTA VOUCHER ZAO KAMA UTAPATA! kweli ukiona kampuni hazina wateja ni za kuokota!
  R.I.P TTCL na ZANTEL!
   
 2. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Hapa nimekusoma kwa 3G ya Zantel.
   
 3. MAKOSHNELI

  MAKOSHNELI JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 474
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 80
  ZANTEL Wanaongoza kutengeneza matangazo mazuri tu
   
 4. k

  kamili JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Mh elfu 10 tu! bado utaona mengi. Nani kakudanganya unachotangaziwa ndicho? Makampuni mumiani yanazidi kuongezeka kila siku. Tunajikaza hivyo hivyo otherwise tutakosa habari.
   
 5. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hamia Airtel
   
 6. J

  Jahom JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 349
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Yah, I suffered the same. TTCL wanafanya kazi kama vile wako peke yao sokoni enzi hizo. Customer care mbovu kuliko maelezo gharam kubwa kuliko na hata ukienda ofisini kwao unakuta wanapiga story zao tu na utaondoka bila msaada wa uhakika.
  Nilikuwa mzalendo lakini sasa BASI. Sijui tufanye nini watu hawa wabadilike!!!!!!!
  AIBU TUPU!!!!
   
 7. J

  Jahom JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 349
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kama ninaweza kumshawishi kila mmoja hapa jamvini, ni kuwasusia TTCL mpaka wakose mishahara labda akili zitakuja wafanye kazi kulingana na soko. Watz tutaacha lini uvivu na wizi? Mtu hajali kuhusu huduma mbovu anayotoa kwa kuwa ana hakika atalipwa mshahara wake, halafu huwezi kumfanya kitu kwa kuwa hakuna hata mkubwa wake utakayemwambia akawawajibisha wa chini yake kwa kuwa naye yuko hivyo. AIBU TUPU.
   
 8. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  TTCL ukilipa per flow ni gharama sana, Tshs 75/MB, nafikiri wao ndiyo wana huduma nzuri sana kama unatumia simu ya nyumbani na ukichagua bundle ndiyo unalipa kidogo. Ila ukimaliza bundle, unaingia per flow ambayo ni gharama za juu. Kuhusu voucher, mbona zipo sehemu nyingi, ukienda mahali popote kwenye max Malipo unaweza kununua TTCL broadband, sema wauzaji wengi hawajui, na usipomweleza vizuri atakuuzia ya voice.
   
 9. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu, nini kilichokupata mpaka unataka tususie huduma zao? Toa mfano halisi basi.
  Mimi natumia TTCL broadband, na mpaka ukiacha matatizo ya mara moja moja i enjoy their service. Customer services issue bado TTCL nawaweka juu kulinganisha na makampuni ya simu za mikononi, hasa inapokuja kwa huduma kwa njia ya simu. Wakati inakuchukua chini ya dk 1 kuunganishwa na customer care rep wa TTCL, hali siyo hivyo kwa kupiga simu kwenye kampuni ya simu za mikononi huduma kwa wateja.
   
 10. J

  Jahom JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 349
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nilinunua bundle ya MB 500 wakati huo kwa ajili ya kutumia kwa mwezi, iliisha baada ya siku mbili. Nikapiga simu kupata ufafanuzi kila aliyepokea hakunipa maelezo kwa kunieleza ngoja afuatilie halafu wanaondoka hewani. Nalinganisha na Sasatel japo coverage yao ni Dar pekee, 30,000 inatumika mwezi mzima unlimited. Issue hapo ni cost kubwa na huduma kwa wateja isiyo ya uhakika. Kama uko kny broadband nadhani mambo yanaweza kuwa tofauti.
   
Loading...