TTCL mnakula sana MBs

TTCL mnakula sana MBs

Gini

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2018
Posts
398
Reaction score
385
Nimekuwa mtumiaji wa TTCL kwa muda sasa, mbali na kuwa na changamoto za mtandao ambao kimsingi mi kero lakini imeibuka changamoto nyingine ya kula MBs.

Unajiunga na kifurushi na kupewa MBs 500 lakini namna zinaenda unabaki unashangaa. Na hapo unakuwa umetumia twitter kusoma tu posts, umeingia WhatsApp kusoma meseji na JamiiForums kusoma soma.

Kote huko huja download video wala kuangalia status, ukitumia masaa mawili mfululizo kuwa katika hizo social networks u ajikuta MBs 150 zimekatika. Ni mimi tu au na ninyi waungwana mnakumbana na tatizo hili?
 
Mimi niliacha kutumia mtandao wao baada ya mwezi mmoja tangu niliposajili laini yao

Vipi je kuna vifurushi vya Bei nafuu kwa sasa au ni magumashi tu?
 
Kwa mnaotumia kompyuta ya Windows, hakikisha connection yako umeiweka kuwa "metered".

Ukiwa unatumia Android hakikisha umeweka app ya Glasswire inayohesabu matumizi yako, ili kupata ulinganifu.
Asante sana ndugu, yaani ndani ya mwezi huu mpaka leo nimetumia GB 10.2 dah ni matumizi makubwa sana. TTCL wanakula sana MBs, so nafanyaje ku balance hii kitu
Screenshot_20201223-225321.jpg
 
Hiyo bandwidth hawajala TTCL. Ni app zako. Inawezekana unatumia tethering. Au simu yako ya inadukuliwa.
 
Naepukakana vipi na hili tatizo?
Hakikisha simu yako haina bloatware: iroot halafu ondoa app zote zisizo na maana.

Weka firewall.

Uninstall VPN app.

Degoogle. tycrek/degoogle

Ukiweza Install ROM mpya kama vile

Paranoid Android

Pambana na wadukuzi Android - Platforms - PRISM Break

Na kadhalika.
 
juzi nikajisema wacha niwe mzalendo,nikasajiri line ya TTCL,kuweka vocha kupitia vodacom,wakanitumia sms kwamba sms vocha imefika,nikajiunga kifurushi cha watumishi,na salio likalimwa.

baadae sion mbs,dakika wala salio la sms,naangalia salio kuna shilingi 40 nauliza salio naambiwa hujajiunga kifurushi chochote,nikabaki sielewi nini kimetokea,mpaka sasa niko zangu voda sitaki kuwa na kiherehere tena.
 
Utaalamu wa kuifanya hii kitu kwangu ni ngumu
 
TTCL ni wezi aisee. Bundle zao hazina uhalisia na ukiwafuata wanakuwa na maelezp ambayo hayana maana yoyote. Niliachana na line ya TTCL baada ya kuliwa GB zaidi ya 15 kwa masaa. Nikanunua tena zikaliwa. Nikanunua tena zikaliwa. Nikawauliza inawezekanaje ndani ya masaa machache GB zaidi ya 15 zinaisha wakasingizia eti modern yako umeconnect watu wengi, nikasema hata kama wangekuwa 10.., fb, whatsApp na mitandao ya kijamii ndo ile hela mingi kiasi hicho.
Nikaachana nao. Nilijaribu kuwa mzalendo lkn Wanisamehe kwa kweli.
 
Utaalamu wa kuifanya hii kitu kwangu ni ngumu
Ni TTCL tu??? Mbona mitandao mingine haifanyi hv. Hv unafikiri nikinunua line ya TTCL nakuwa sina mitandao mingine?
 
Pole sana kwa kiherehere mkuu!
juzi nikajisema wacha niwe mzalendo,nikasajiri line ya TTCL,kuweka vocha kupitia vodacom,wakanitumia sms kwamba sms vocha imefika,nikajiunga kifurushi cha watumishi,na salio likalimwa.

baadae sion mbs,dakika wala salio la sms,naangalia salio kuna shilingi 40 nauliza salio naambiwa hujajiunga kifurushi chochote,nikabaki sielewi nini kimetokea,mpaka sasa niko zangu voda sitaki kuwa na kiherehere tena.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom