Tetesi: TTCL kuuza hisa zake DSE

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Inasemekana baada ya serikali kununua hisa zote za airtel ndani ya TTCL.. uongozi wa TTCL umepanga kuanza kuuza hisa zake DSE.. kama ni kweli basi TTCL itakua kampuni ya kwanza ya simu hapa tz kufanya hivyo.

Wataalam wanasema kama ikifikiapo hapo kuna uwezekano mkubwa TTCL kuwa kampuni Tishio ukizingatia ina miundo mbinu mizuri na pia inapendwa sana na watanzania wengi ambao wamekua na kiu ya kutumia huduma za zake..
 
Wauze tu, tuatwaunga mkono sana tu, tunachotaka kuona pesa za kampuni zinatumika kuboresha huduma, na kuwapatia wananchi huduma nafuu na zenye tija
 
Nilipata kusikia kuwa kuuza hisa kwa public kwa kampuni iliyopo ni lazima waonyedhe historia au rekodi ya faida ya miaka mitatu iliyopita. TTCL wataitoa wapi rekodi hiyo?
 
Mh! hapo wakitaka wabinafsishe management. Mashirika mengi ya serikali yanakufa sio kwa kukosa pesa wala vitendea kazi bali utendaji mbovu na kukosa usimamizi.
 
wauze hisa sawa na tuone mabadiliko sasa hili shirika lina hitaji kufumuliwa watumishi waliopo hawaendi na kasi ya mashirika ya simu tanzania ,
 
Hizi ni habari njema kwa wazalendo wa kweli....lakini kabla ya kufanya hivyo wabadili menejimenti yote....ili kuendana na kasi ya ushindani uliopo katika sekta ya mawasiliano....
 
Back
Top Bottom