Kabla ya kuiondoa TTCL iruhusuni ipange bei ya shughuli zake

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
862
1,097
Ni uonevu mkubwa ikiwa TTCL itaondolewa katika biashara wakati inalazimishwa kupandisha bei ya bidhaa zake ili zilingane na washindani wake.

Iwapo TTCL itaachwa ifanye kazi kibiashara hakuna kampuni itakayokuwa na unafuu kuliko TTCL na TTCL inasaidia sana kudhibiti ongezeko la bei kwa watoa huduma wengine.

Kuondoka kwa TTCL ni maombi ya watoa hudumq wengine na hasa baada Rostam Aziz kununua kampuni ya Tigo Zantel.

Serikali iangalie vizuri suala hili
 
TTCL hata vocha weshindwa kusambaza, sembuse kusema walikuwa wanazuia bei kupanda? Tuwe realistic, Unadhani CEO wa Voda anawaza TTCL kama mshindani wake ? Mtu mwenye 0.05% market share

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Soma vizuri mada hii utaelewa ninachokizungumza na hatari ya kuiondoa TTCL katika soko..TTCL siyo mbovu bali inafanywa hivyo na watu walio ndani na nje ya kampuni kwa maslahi ya makampuni binafsi....serikali iingilie kati TTCL itakuwa bora kama zilivyo taasisi nyingine kama NMB na CRDB ambazo zilipingwa kibiashara hapo mwanzo.
 
TTCL ameambiwa asimamie mkongo tu, ikiwa na maana yeye atakuwa anawauzia data za jumla kwenye makampuni mengine kama vile Tigo, VodaCom na wengineo.
TTCL itajikita zaidi kwenye Faiba tu.
Another question?

LUS0MYA
 
Ni uonevu mkubwa ikiwa TTCL itaondolewa katika biashara wakati inalazimishwa kupandisha bei ya bidhaa zake ili zilingane na washindani wake.

Iwapo TTCL itaachwa ifanye kazi kibiashara hakuna kampuni itakayokuwa na unafuu kuliko TTCL na TTCL inasaidia sana kudhibiti ongezeko la bei kwa watoa huduma wengine.

Kuondoka kwa TTCL ni maombi ya watoa hudumq wengine na hasa baada Rostam Aziz kununua kampuni ya Tigo Zantel.

Serikali iangalie vizuri suala hili
Tatizo mashirika ya umma hakuna mwenye uchungu mradi wanapata mshahara kama Tanesco tu
 
Hayo mashirika yanasimamiwa na watu washenzi sana. Hivi tunashindwaje kuajiri wazungu wakayaendesha hayo mashirika?
 
Back
Top Bottom